Communism, capitalism and islamism mfumo upi wafaa?

Jindal Singh

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2015
Posts
1,857
Reaction score
1,541
Kuanguka kwa muungano wa Jamhuri za Kisovieti (USSR) mwanzoni mwa miaka ya tisiini, haikuwa tu ni kuanguka kwa dola, bali kulikuwa ni kushindwa kwa mfumo, na mwisho wake kimataifa na kiulimwengu.

Mapambano ya (vita baridi) yaliyotokea baada ya vita vya pili vya Dunia baina ya upande wa Magharibi ukiongozwa na Marekani, na upande wa Mashariki ukiongozwa na muungano wa Jamhuri Kisovyeti, hayakuwa tu ni mpambano ya Kimataifa baina ya kambi mbili, bali pia yalikuwa ni mapambano ya kimfumo wa ki-?aqida baina ya mifumo miwili; Ubepari (Ukapitalisti) na Ujamaa(Ukomunisti).

Uwanja wa mapambano haya ulikuwa sio tu bara la ulaya pekee, bali yalienea ulimwengu mzima, na mapambano haya yaliendelea na hayakumalizika hadi kuanguka kwa muungano wa Jamhuri za umoja wa Kisovieti na kusambaratika vipande vipande kuwa vijidola, kwa hivyo mfumo wa ujamaa Ujamaa wa Ki-marxi ulishindwa kama mfumo na njia ya kimaisha [twariqa] kwa dola zilizokuwa zikiuunga mkono na watu wake,hivyo basi Ujamaa wa Ki-marxi ukashindwa kimataifa na kilimwengu.

Kwa hivyo likawa ni jambo la kutarajiwa kwa Marekani na kambi ya kimagharibi kwa ujumla kuchukulia kuanguka kwa Muungano wa Jamhuri za Kisovieti na kuanguka kwa Ujamaa kama ushindi wa mfumo wa kibepari kama mfumo na njia ya Maisha. Na likawa jambo la kutarajiwa kwa wafuasi wa Ubepari kufurahi sana katika kushereherekea ushindi huu hadi kufikia kiwango kwa mwanafalsafa wa kimarekani mwenye asili ya kijapani anaeitwa Fukiyama kuunasibisha ushindi huo kuwa ni, ?Mwisho wa Historia?.

Mifumo hamaliziki kwa kuanguka tu kwa dola zinazobeba mifumo hiyo, hata kama kuanguka huko kutasababisha kuvunjika na kugawanyika kwa dola zake, bali mifumo humalizika pindi mataifa yao na watu wao kuiipa mgongo na kuelekea kwenye mfumo mwengine na kuanza kuendesha maisha yao kwa msingi wa mfumo huo mwengine.

Hivi ndivyo ilivyotokea kwa Ujamaa wa Ki-marx, mataifa yote na watu waliokuwa katika kambi ya mashariki waliutupilia mbali mfumo huo na kuelekea kwenye ubepari na kuanza kujenga maisha yao kwa msingi huo. Hata hivyo kwa upande mwingine, Uislam kama mfumo umebakia kuwepo kiulimwengu hata baada ya kuvunjwa kwa dola yake, ?Dola ya Khilafah ya Uthmani? mwaka 1924 (mwaka wa kikiristo) kwa sababu umma wa kiislamu na watu wake wote tofauti wanaedelea kushikamana na mfumo huo licha ya kuondolewa kwake katika maisha yao ya kila siku(kivitendo) na kuondolewa katika uwanja wa kimataifa. Mfumo unabakia katika ulimwengu madam kuna umma [watu] wanaoubeba, hata kama umma huo hauutekelezi mfumo wake kutokana na sababu za kutenzwa kwao nguvu kinyume na matakwa yao. Hata hivyo (mfumo) unamalizika kuwepo kimataifa ikiwa hakuna dola ya kuueneza na kupeleka misimamo yake kimataifa kwa msingi wake (huo mfumo).

Kama inavyoeleweka mfumo wa kiislam ulikuwepo katika ulimwengu tangu wakati wa umma wa kiislam ulipoundwa kwa msingi wa mfumo huo, baada ya hijra ya bwana Mtume(SAW) kwenda Madina iliposimamishwa dola ya kwanza ya kiislamu. Na iliendelea kuwepo kimataifa dola hiyo tangu wakati huo (Hijra) mpaka wakati wa Dola ya Khilafah ya Kiuthmani ilipoanguka katika robo ya kwanza ya karne hii (karne ya ishirini miladi).

Ama kuhusu ujamaa ulianza katika ulimwengu kuelekea mwisho mwa karne ya 19 miladi pale ulipopata kuungwa mkono na miongoni mwa watu wa Ulaya. Ulikuwepo kimataifa tangu mwaka 1917 miladi pale dola ya Urusi iliposimamishwa na kuungwa mkono na nchi jirani, ambazo mwisho zikajuulikana kama Muungano wa Jamhuri za Kisovieti. Ujamaa uliendelea kuwepo kimataifa mpaka mwaka 1991 pale Muungano wa Jamhuri za Kisovieti ulipoanguka na watu wake kutupilia mbali ujamaa. Na kwa hivyo ujamaa wa ki-marx ukamalizika kimataiafa na kiulimwengu.

Kwa kuanguka kwa ujamaa, Ubepari ukabakia pekee katika uwanja wa kimataiafa kwa sababu haaukuweko tena na dola yoyote katika ulimwengu inayobeba mfumo mwengine iliyoweza kujenga misimamo ya kimataifa kwa msingi wa mfumo wake. Kwa upande wa kuilimwengu mifumo miwili imebakia, Uislamu na Ubepari. Kwa kuwa ubepari ndio unaotawala kimataifa, nidhamu mpya ya kiulimwengu, ikaibuka, kwa hivyo kauli mbiu yao ?Nidhamu mpya ya kiulimwengu?[New world order] ni sawa kwa mtazamo huu. Hivyo likawa ni jambo la kimaumbile kwa Raisi wa Marekana George Bush [wa mwanzo] kutangaza kuzaliwa kwa ?nidhamu mpya ya kiulimwengu? kwa sababu Marekani ndio dola kuu, na inayoongoza dola za kibepari, na inabeba bendera ya kueneza mfumo wa kibepari.

Marekani ilianza kuendeleza Ubepari tangu wakati ilipojitokeza katika ulimwengu kama dola ya kikoloni, kwa sababu ukoloni wote ule, wa kizamani ama wa kisasa ndio njia ya kueneza mfumo huu. Hata hivyo, kile kilichojitokeza hivi karibuni ni kuwa toka kutawala mfumo wake kimataifa, Marekani imeaza kufanya harakati (kampeni) ili kuufanya mfumo huu usimame ulimwengu mzima. Na vile vile kama ilivyofaulu kwa msaada wa dola nyengine za kibepari katika kufanya ubepari ndio msingi wa mahusiano ya kimataifa na maelewano, leo inataka mfumo huu uwe ndio njia ya kimaisha kwa mataifa yote na watu wote katika ulimwengu. Kulingana na mpango huu, watu haitoshi tu kutekeleza Ubepari kama mfumo na kanuni bali ni lazima pia kuamini ?aqida yake pamoja na ufahamu, vipimo na misimamo yake katika kila nyanja ya maisha na sio tu kuridhika kwa kutekelezwa kwake.

Marekani imefanya bidii kufanya mfumo wa Kibepari kuwa msingi wa maingiliano ya kimataifa, desturi na kikanuni kutoka kusimamishwa kwa umoja wa mataifa pale ilipofanya maadili ya kirasilimali kuwa ndio katiba ya taasisi hiyo ya kimataifa. Lakini kivitendo Marekani haikuweza kufikiwa lengo hilo kwa vile Muungano wa Jamhuri za Kisovieti ulikuwa bado ukiendelea kuongoza kambi ya mashariki juu ya msingi wa ujamaa na kulazimisha kuwepo kwa mfumo wake kimataifa na kilimwengu.

Kwa hivyo Moscow iliweza kuzuia utawala kikamilifu wa kibepari kimataifa kwa kutumia kisingizio ch maisha magumu na utumwa wa watu wa nchi zilizotawaliwa ambazo zilitokana na unyanyasaji, dhulma na ulafi wa dola za kikoloni za kimagharibi. Kwa hivyo (Moscow) ilifanya kampeni kali ulimwengu mzima ambapo kampeni hiyo iliuonyesha ukoloni kwa sura yake halisi ya uchafu, kwa kuuafanya ukoloni na ubepari ni kitu kimoja na kufafanua zaidi kuwa njia ya kujikomboa kutokana na ukoloni ni kupitia mapinduzi ya kiujamaa. Kampeni hii ilifaulu sana kufika hadi kuwa watu wakaanza kuvutiwa na ujamaa, na mataifa yaliopata uhuru na kujikomboa wenyewe kutoka ukoloni kwa ile sura yake ya kizamani, wakaitikia mwito wa ujamaa.

Juu ya hivyo, Marekani ilitambua kuwa ile sura ya ukoloni ya zamani itakuwa ni hatari kwa nguvu za kimataifa ya magharibi, na vile vile kwa Ubepari kama mfumo. Hivyo basi, ikafanya kazi kijanjajanja kuzidhibiti shauku na maatakwa ya watu na mataifa yaliyouelekea ujamaa, Marekani yenyewe ikaanza kusaidia mataifa haya na watu hawa kujikomboa kutokana na ukoloni wa kiwazi kutoka nchi za Ulaya, na kuanza kuyabana mataifa huru haya kwa aina ya ukoloni mpya ulio mbaya zaidi uliojengwa juu ya kumiliki na kutawala usiokuwa wazi kwa upande wa kiuchumi, kisiasa na kihadhara ambao uliwakilishwa kwa makubaliano ya mashirikiano ya kijeshi, makubaliano ya ulinzi , ushirikiano wa mipango ya kiuchumi, misaada ya kifedha na kihadhara.

Kwa hivyo basi, chini ya bendera za uhuru na ukombozi ukoloni mpya ukachukuwa nafasi ya ukoloni wa zamani. Juu ya hivyo, kwa kuanguka kwa Muungano wa Jamhuri za Kisovieti na ujamaa, uwanja wa kimataifa ukawa mweupe kwa ubepari na kukawa hakuna tena upinzani kwa utawala wa Ubepari kimataifa.

Umoja wa mataifa ambao tokea miaka ya 1940 (mwaka wa kikristo) ulikuwa ukitumika tu kama jukwaa la mazungumzo, pasi na kuwa na nguvu kwa sababu ya kura ya turufu (veto) ya Muungano wa Jamhuri za Kisovieti, sasa ukabadilika kuwa chombo kikubwa cha kimataifa kinachobariki ubwana wa kimataifa. Na kikawa chombo muhimu katika kulazimisha utawala wa Marekani kwa upande mmoja na kumakinisha maadili ya Ubepari kwa upande mwengine.

Kampeni ya Marekani kuufanya Ubepari kuwa ndio mfumo kwa mataifa yote na watu wote ulimwenguni, haipati upinzani wowote isipokuwa katika ulimwengu wa kiislamu. Hii ni kwa sababu watu wote na mataifa yote yaliyobakia imma tayari wameubeba Ubepari kama ilivyo kwa Marekani, Ulaya magharibi na wafuasi wao kama Kanada, Australia na New Zealand, amma nyengie kama Urusi na mataifa ambayo mwanzo yalitambulika katika kambi ya mashariki sasa yameupa mgongo ujamaa na kuanza kuyapeleka maisha yao kwa msingi wa ki-bepari. Am mataifa mengine kama Uchina, Korea ya kaskazini, Vietnam na Cuba ambayo bado kwa maneno hubeba kaulimbiu ya ujamaa, lakini kihakika si waumini tena wa mfumo wao huo na taratibu wanaelekea kwenye Ubepari bila ya kutangaza hivyo kirasmi. Na mataifa mengine na watu wengine ambao kimsingi hawakuwa na mfumo na kwa hivyo hawauchukui Ubepari kama upinzani wa kifikra ni Marekani ya kusini (Latin America), Mashariki ya mbali, kusini mwa Asia mashariki, na baadhi ya nchi na kabila za Afrika.

Umma wa kiislamu ndio umma pekee miongoni mwa mataifa yasiokuwa katika ulimwengu wa kibepari ambao una mfumo unaouamini licha ya kuwa hivi sasa hauishi kulingana nao wala kuubeba kiulimwengu.

Kwa hivyo kampeni ya Marekani ya kuutawalisha Ubepari ulimwengu mzima haupati upinzani wa kweli isipokuwa katika ulimwengu wa kiislamu.

Serikali zote zilizopo hivi sasa katika ulimwengu wa kiislamu hazitekelezi uislamu-hata kama baadhi yao hudai kufanya hivyo-lakini wanatabikisha Ubepari wa kimchanganyiko usiokuwa wa kihalisi. Lakini umma wa kiislamu, ambao haukupotea hata baada ya kuangushwa kwa dola ya Khilafah, ulianza katika miaka ya 1950 (mwaka wa kikristo) kuhisi njia yao ya kuinuka kwa msingi wa Uislam. Ulianza kuchukuwa Uislam kama njia ya kurudi kuishi kwa msingi wake, na kuangalia mbele kusaidia ulimwengu kwa msingi huo, licha ya migawanyiko ambayo makafiri wameitengeza ndani yake kabla na baada ya kuvunjwa kwa dola ya Khilafah, na licha ya kuwa watawala wake ni vibaraka wa makafiri wanaolinda utawala wa ukafiri uliosimamishwa na wamagharibi katika biladi za Waislam. Watawala hawa wanachunga maslahi ya wamagharibi, wanaimarisha athari zao na kupeleka mambo yao yote ya ndani na ya nje kulingana na maelekezo na matakwa ya wamagharibi.

Ijapokuwa mwamko katika umma haujakamilika, na unaendelea taratibu kwa sababu ya ukandamizaji na mateso dhidi ya wale wanaofanyia kazi (mwamko huo), kutoka watawala vibaraka, na pia kwa sababu ya watawala kueneza hali ya ukandamizaji na ugaidi dhidi ya waislam pamoja na mipango ya makafiri inayotekelezwa na vibaraka hawa dhidi ya watu wao ili kuwafanya waungue chini ya moto wa ukafiri. Licha ya yote haya wamagharibi makafiri wakiongozwa na Marekani wanaogopa umma wa kiislam kukamilisha mwamko wao na kurudi kwa waislam kuwa ni umma wa pekee miongoni mwa watu wote, ambao wanaishi katika kiungo kimoja yaani dola ya Khilafah. Dola ambayo itarudia kufikisha ujumbe wa Uislam ulimwenguni ili kuukomboa kutoka mashaka, fujo na mporoko wa maadili ambao leo dunia imezama kutokana na mabavu ya ubepari na maadili yake ya maslahi ya vitu, maadili yaliobadilisha ulimwengu kuwa mbuga isiyokuwa na usalama wala utulivu, licha ya matunda ya kisayansi na kiteknolojia ambayo mwanadamu ameyafikia .

Hivyo makafiri wamagharibi bado wanakumbuka namna Uislam ulivyoweza kuwabadilisha waarabu kutoka kuwa makabila ya kupigana pigana wasiotambuliwa kihistoria mpaka kubadilika na kuwa umma maalum wa aina yake uliostaarabika na hadhara iliyoangaza uliwengu mzima, umma ambao uliweza kuwa bwana wa ulimwengu kwa muda mfupi mno na kuendelea kuwa hivyo kwa karne kumi, huku ukieneza uadilifu, usalama, maadili ya daraja ya juu na ufanisi katika kila mahali ambapo bendera za Khilafah zilipepea.

Kwa hivyo Magharib inahofia umma wa Kiislam kurudia tena hali yake ya asiii kiasi cha kuharibu maslahi na taathira zake sio tu Marekani bali ulimwengu mzima. Kwa Marekani na Magharibi kutambua jambo hili, kampeni ya Marekani imeelekezwa kimsingi dhidi ya umma wa Kiislamu licha ya kuwa kampeeni hiyo inafanywa ulimwengu mzima.

Kampeni hii ina malengo mengine kama ulafi wa kirasilimali, tamaa ya Marekani na wamagharibi juu ya utajiri katika biladi za Waislamu, pamoja na nchi hizi kuwa ni maeneo muhimu ya ki-statejia (geo-strategic), na nchi hizi kuwa soko kubwa kwa bidhaa za Magharibi na chimbuko la malighafi muhimu kwa viwanda vyao, na vile vile nchi hizi kumiliki hazina ya visima vya mafuta yalio na umuhimu wa kufa na kupona kwa maisha ya wamagharibi. Pamoja na haya yote, lengo msingi nyuma ya kampeni hii ni hatari wanayoiona kutoka kwa umma wa Kiislamu dhidi ya maslahi ya kimagharibi na athari yake kimataifa bali hata uhai wake pindi umma wa Kiislamu utakapoamka na kuinuka, na kubeba ulinganizi wake kwa ulimwengu mzima.

NGUZO ZA KAMPENI YA MAREKANI.

Marekani inategemea, katika kuendesha kampeni yake dhidi ya ulimwengu wa Kiislamu, juu ya nguzo zifuatazo:-

Nguzo ya kwanza: Uzito wake kimataifa na athari yake katika ulimwengu wa Kiislamu, hususan baada ya vita vya pili vya Ghuba ambavyo vilipelekea kuimarika athari ya Marekani katika eneo lote la ulimwengu wa kiislam. Kwa sababu ya uzito huu na athari hiyo, dola nyingi katika uliimwengu wa Kiislam zikaitikia zaidi shinikizo la Marekani na mipango yake inayolenga kukandamiza Uislamu kwa kuwalazimisha Waislamu kuukubali Ubepari.

Nguzo ya pili: Uongozi wa Marekani juu ya dola za kibepari na ghera yake kuwashirikisha katika kampeni hii ili kutumia athari zao na vibaraka wao katika ulimwengu wa Kiislamu kufanikisha kampeni hii hususan kuwa nchi hizi hazitofautiani na Marekani katika kuuangalia Uislamu kama hatari kwao, kwa athari zao na maslamhi yao.

Nguzo ya Tatu: Inayoitwa sheria za kimataifa na taasisi zake inayowakilishwa na Umoja wa Mataifa (UN), katiba yake na mipango yake na kujificha nyuma ya vazi la kanuni ya kimataifa ili kuchukua hatua inayoona ni muhimu kuchukuliwa sawa sawa iwe masuala ya kisiasa, kiuchumi, kijeshi na kadhalika.

Nguzo ya Nne: Vyombo vya habari vya kiulimwengu ambavyo vimetawaliwa na Marekani na washirika wake, vinavyotumiwa kama silaha miongoni mwa silaha za hatari zaidi katika kampeni yake kwa kuvitumia kupigia debe miito yake. Vyombo vya habari hutumiwa kuharibu sura ya Uislamu na kushajiisha uliwengu dhidi ya wale wanaoshikamana na Uislamu kwa kuwaonesha kama ni watu wenye siasa kali, wanaovuka mipaka, wenye hamasa na magaidi. Silaha hii si ya kudharauliwa hasa baada ya mapinduzi katia sekta ya mawasiliano yaliyotokea katika nusu ya karne hii ambayo yameubadilisha ulimwengu kiasi cha kuwa kijiji kidogo ambapo kila kinachoandikwa, kusikika na kuonekana kimawasiliano kinapatikana katika kila nyumba.

Nguzo ya Tano: Pengine mbaya na ovu zaidi na ya hatari zaidi katika nguzo hizi ni watawala vibaraka na wale waliwazunguuka miongoni mwa mamluki wanafiki, watu wa maslahi na wenye kuwaunga mkono miongoni mwa waliovutiwa na hadhara ya kikafiri na kufitinishwa na mtindo wake wa kimaisha, bali hata baadhi ya wale wanaodhihirisha hamu na Uislamu sawa sawa wawe miongoni mwa wanavyuoni wa kiserikali au amma wale wanaotangulizwa kwa watu kama wasomi wa kiislamu au baadhi ya watu wa harakati za Kiislamu ambao kwa hakika si wengine ila ni wenye kuamini ilmaniyya (secularism) na kulingania kutenganisha dini na maisha.

Yote haya yanamsaidia Mmarekani katika kuwapotosha Waislamu mbali kabisa na dini yao na kuwapeleka katika Ubepari kwa njia na mbinu aina kwa aina: Mfano ni kupotosha kupitia vyombo vya habari, kupotosha fahamu na hukmu za Uislamu, kutabikisha nidhamu za kikafiri pamoja na kuandaa sheria na hatua mwafaka kuziwezesha utekelezaji wa nidhamu hizi za kikafiri, Pia kuzitenza nguvu nchi katika ulimwengu wa Kiislamu kwa mikataba mbali mbali miafaka na vikwazo tofauti ili kuziweka chini ya taathira za makafiri na kukamilisha lengo lao katika kutekeleza mipango ya makafiri ya kuufakirisha Umma ili kutupilia mbali maadili yao ya Kiislamu. Mbali na uvamizi dhidi ya wanaharakati wakweli miongoni mwa Umma wanaojifunga na Uislamu kidhati kwa kuwanyamazisha, hivyo basi kueneza hali ya unyonge na maonevu na wasiwasi (khofu) juu ya watu ili kusiwe na mtu wa kuzungumza haki. Yote haya ni kwa ajili ya kudhalilisha Umma na kuwalazimisha kuukubali ukafiri na makafiri.

Hizi ndizo nguzo muhimu ambazo Marekani inazitegemea katika kampeni yake dhidi ya Uislamu na waislam, kwa lengo la kukandamiza Uislamu kwa kulazimisha Waislamu kuukubali Ubepari. Kampeni hii inajitokeza katika miito [slogans] minne ambayo ndio kiini cha Ubepari: Demokrasia, Vyama vingi, Haki za binadamu na Sokohuria.

Kabla hatujaitizama miito hii na kuifafanua kimakini, ni lazima kwanza tufahamishe ule uo msingi uliojengewa juu yake miito hii. Msingi huu ni ?aqeeda ya kibepari, nayo ni ?aqeeda ya kutenganisha ?dini na maisha?[secularism].

?Aqeeda hii haikujengwa juu ya hoja ya kiakili wala ya kimantiki, bali ni mawafikiano ya kati na kati baina ya fikra mbili zinazogongana. Fikra ambayo makasisi walikuwa wakiilingania huko Ulaya katika zama zinazoitwa ?miaka ya kale?[Medieveal Ages] nayo ni kukisalimisha kila kitu katika maisha haya kwa ?dini? na ile fikra ambayo baadhi ya mufakirina [thinkers] na wanafalsafa wakiilingania nayo ni kukataa kuwepo kwa Muumbaji.

Kwa hivyo fikra ya kutenganisha ?dini? kutoka maisha ni suluhisho la mapatano baina ya pande hizi mbili.

Suluhisho la mapatano linawezekana baina ya mitazamo miwili ambayo hutofautiana kidogo lakini haiwezekani kuwepo baina ya mitazamo miwili inayogongana. Kwa hivyo imma yupo Muumbaji ambaye amemuumba mwanadamu, ulimwengu na maisha na hivyo basi mjadala utakuwa-kuhusu ikiwa Muumbaji huyu amemuwekea mwanadamu nidhamu ambayo hana budi kuifuata katika maisha haya yake ya dunia, na hatimaye kama Muumbaji atamuhisabu mwanadamu baada ya kifo chake kuhusu kujifunga kwake na nidhamu hiyo. Au hakuna Muumbaji na hivyo dini si tu iondolewe katika maisha ya dunia bali itupiliwe mbali kabisa !.
Lakini kusema kuwa hakuna umuhimu kujadili katika kuwepo amma kutokuwepo kwa Muumbaji, hilo ni jambo lisilokinaisha akili wala kutuliza nafsi.

Kwa hivyo ?aqeeda ya Kibepari ikawa ni matokeo ya muwafaka wa mapatano katika jambo ambalo lisilokubali mapatano, na hilo pekee linatosha kuikataa ?aqeeda hii kwa kambi zote mbili wale wanaomini kuwepo kwa Muumbaji amma wale wanaokataa kuwepo kwake.

Dalili wazi za kiakili hukinaisha kuwepo kwa Muumbaji ambaye kwamba amemuumba mwanadamu, ulimwengu na maisha na kwamba huyo Muumbaji amemuwekea mwanadamu nidhamu ili aifuatilie katika maisha yake na kuwa yeye (Muumbaji) atamuhisabu baada ya kifo chake juu ya kujifunga nayo kwake.

Hata hivyo, suala letu hapa sio kujadili kuwepo kwa Muumbaji wala huo mfumo aliouweka kwa ajili ya mwanadamu, bali ni kujadili juu ya ?aqeeda ya kibepari na kudhihirisha uongo wake. Kwa hayo hutosheleza kubainisha uongo huo kwa hakika yake, kuwa ni ?aqeeda ya mapatano baina ya fahamu mbili zinazogongana na kwa msingi huo haikujengwa juu ya akili.

Kwa kubainisha uongo wa ?aqeeda ya Kibepari inatosheleza kabisa kuukataa mfumo wote wa kirasilimali kwa sababu kitu chochote kilichojengwa juu ya uongo chenyewe huwa ni uongo. Hii humaanisha kuwa hakuna haja ya kujadili urefu misingi ya mifumo hiyo. Isipokuwa kwa sababu baadhi ya fahamu hizi zimefaulu kuenezwa ulimwengu mzima na kukubaliwa na baadhi ya Waislamu na pia kwa sababu fahamu hizo ndizo miito ya kampeni ya Marekani katika uvamizi wake wa kikatili dhidi ya Waislamu na Uislamu, hakuna budi basi kuzielewa kuonyesha uongo wake pamoja na kugongana kwake na Uislamu. Hivyo basi Waislamu wameharamishwa kuzichukuwa na ni wajibu kuzikataa na kupambana na yeyote yule anaezipigia debe.
 
Hii kitu itafutwaje naona jitihada nyingi zimefanyika.
 
Je suit Christian wewe!!!!
 
Kabla hujafika mbali konda nishushe kimara mwisho..... Kwenye mfumo Wa kiislamu umedanganya umma asee..... Uislamu ni utaratibu Wa maisha na Imani sio mfumo Wa maisha..... Kwa hiyo
1.communism
2.slavery
3.feudalism
4.capitalism
5.socialism
6.islamism!!!???
Umetuuzia kahawa kwenye vifuki vya barafu
 
Kwani Communism sio imani mbona watu walikufa kwa kuueneza ukomunist, tafuta hii kitu inaitwa Ottoman Empire.
 
Communism creates God haters

Capitalism creates prosperity and respect of true God.

Islamists/ism as you said it causes Islamists and killing through ISIS.

Jesus is God
 
Kuna siku katika pitapita zangu nikagumiana na washkaji wakidai et wapo ktk harakati ya kutaka kurudisha ukomunisti maishani, kweli watu wamedata.
 
Back
Top Bottom