Comedy za bongo na vichekesho vya wanaume kuigiza wanawake.zinaboa

Comedy za bongo na vichekesho vya wanaume kuigiza wanawake.zinaboa

dr.malulu

Senior Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
133
Reaction score
60
SALAM
Napenda sana comedy kwa sababu ukicheka inasaidia kukimbiza some stress.Nilikua mfuatiliaji sana wa comedy ya kina masanja enzi hizo wakiwa east africa,na mwanzoni mwa TBC 1 Kipindi ikiwa alhamis.sikua tayr kukosa baadae Tbc nayo ikiwa mambo mengi mara bunge mala report maalumu mpaka network yangu ikakataa kabisa.MAra Bambo nae akaingia kazini(east africa tv) mwanzon mwanzoni mambo yalikua mazuri,ubunifu ulikua wa hali ya juu,nikaaenda nao mpaka kipindi fulani hivi mnara ukapoteza signal.Full upuuzi mwanzo mwisho,awe shabani saa hv ni demu mda wote.

KINACHONIKELA SASA HIVI comedy nyingi zinahisi wanaume wakivaa nguo na kujiremba kama wanawake inachekesha lakini ukweli ni kwamba INABOA TU.utakuta mwanaume kaweka matiti na kubadilisha sauti daaah mara anaingizwa gest house hata maadili hakuna tena.Wanasahau kama vipindi vyao hata watoto wanaweza kuangalia.tafuteni mbinu nyingine au muajiri wanawake kama wenzenu wa futuhi mwanaume anabaki kua mwanaume na mwanamke anasimama nafasi yake pia.

NAWAZA SANA
 
waache tabia zenye element za ushoga zinaharibu jamii badala ya kujenga,
 
Subiri Bunge Lianze,
Never miss.
very sorry kuna mmoja leo kapungua.
 
Kama wale wa channel ten , wanaigiza mara vilema , mara kigugumizi hadi wanaboa, najiuliza kwani hawawezi kuchekesha bila ya kujifanya walemavu???
 
Naunga mkono mada;mpaka sasa kipindi bora cha vichekesho ni cha Futuhi.nafasi ya mwanamke ni mwanamke na kinyume chake.Kipindi kina muda wa kutosha pamoja na vipengere vingi.
 
Yaani wanaigiza wao aibu unaona we mtazamaj... Inakera sana, izo mbinu hazina mashiko now days.
 
Yaani mi nilishaacha kuangalia comedy za bongo. Hivi kuchekesha lazima uigize mwanamke? Ina maana wanawake wetu ni vichekesho kiasi hicho? Mbona tunashinda nao makazini na mitaani lakini hatushindi tukicheka? Yaani Joti akiigiza mwanamke basi makundi yote lazima yawe na segment ya dume linaloigiza dem? Very boring.
 
Si comedy tu. Ni movies genres za aina zote bongo zinaboa.. Hakuna uhalisia ktk mambo mengi sana. Kila movie ni mapenzi tu. Maybe sababu ya poor capital, technology& lack of education
 
Yaani mi nilishaacha kuangalia comedy za bongo. Hivi kuchekesha lazima uigize mwanamke? Ina maana wanawake wetu ni vichekesho kiasi hicho? Mbona tunashinda nao makazini na mitaani lakini hatushindi tukicheka? Yaani Joti akiigiza mwanamke basi makundi yote lazima yawe na segment ya dume linaloigiza dem? Very boring.

unaangalia comedy za wap?
 
Munapotaja majina muweke na picha basi mana wengine hatuwajui.nilijilazimisha siku 1 kuangali
 
Tcra inasubiri wapige ban Kenya halafu ndio waige. Kama 50 shades of grey.
 
Wataka kucheka? Angalia vpind vya commedy vya wakenya, offside ntv, mahakaman, hapa kule etc etc etc
Wabongo tumeishiwa ubunfu
 
Back
Top Bottom