Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Vita baridi vilivyodumu kwa Kati ya mwaka 1945-1990 vinaonekana vimerudi rasmi.
Serikali ya Marekani na Urussi zilipambana sana kugombea maslahi ya kisiasa, kijeshi, na kiuchumi, sehemu mbalimbali duniani. Marekani majuzi ililaumu Urussi kwa kuwapa silaha wapiganaji wa Talbani huko Afghanistan wakati hawa hawa watalabani ndio waliotumika kuwaondoa kivita hao warusi kutoka Afghanistan mwaka ya 90. Huko Syria Marekani inajaribu kuendeleza sera zake za Regime Change lakini Urussi imetoa msaada mkubwa wa kijeshi kwa serikali ya Syria ili mpango huo usifanikiwe.
Kwa Afrika kuanza kwa vita baridi itakuwa pigo kubwa sana kwani nchi nyingi za kiafrika ziliingia kwenye Demokrasia ya vyama vingi vya kisiasa na utawala bora baada ya vita baridi kwisha Viongozi wengi kama Mobutu, wa Congo, Said Barre wa Somalia Moi wa Kenya, Mengistu wa Ethiopia Kaunda wa Zambia etc Waliodumu kwa miongo mingi waliondoka madarakani. Kurudi kwa vita baridi kunauwezekano wa utawala wa kimabavu kurudi Afrika.