Deadbody
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 4,291
- 6,693
TWIN BOYS,TWIN LIVES
Maisha ya duniani yapo tofauti kabisa na unavyofikiria.Wengine wanaweza sema kuna kundi la watu wachache wanapangilia kila kitu kinachofanyika duniani na ndio hao hao wanajua kwanini kitu hiko kifanyike.
La hasha!,DUNIA NI TOFAUTI NA UIFIKIRIAVYO
Leo naongelea tukio la Mapacha wawili walioishi maisha sawa kabisa tena bila kujuana
Mapacha hawa walizaliwa Huko OHIO,USA na waliishi maisha ya kufanana kila kitu pasipo wao wenyewe kujua kuwa walikuwa mapacha.
Mapacha hawa wakati wa kuzaliwa walitenganishwa hivyo mmoja aliuzwa kwa mama tofauti kabisa na wakawa hawajuani kabisa na maisha kuendelea.
Nasisitiza kuwa mapacha hawa hawakujuana kabisa enzi za utito wao na hata utu uzima hawakujuana maana waliishi mbalimbali sana , familia zote ziliamua kuwaita watoto hawa jina James.
Na hapa ndio utata unapoanzia .Pasipokujuana hawa mapacha wakajikuta wote wamesomea sheria na kuwa wanasheria wazuri sana , mapacha hawa kwa pamoja wote wawili walikuwa na uwezo mkubwa wa kuchora na pia walikuwa mafundi selemala, pia mapacha hawa pasipokujua wakaoa wake wenye majina ya kufanana.Wanawake hawa waliitwa Linda..
Wake zao walizaa wa kiume na majina ya watoto hawa waliitwa Alan,yani mtoto wa pacha wa kwanza aliitwa Alan na mtoto wa pacha wa pili aliitwa Alan .
Mapacha hawa wawili waliachana na wake zao kwa wakati tofauti ndani ya mwaka mmoja.Mapacha hawa pasipo kujua kila mmoja alioa mke aliyeitwa Betty.
Na wote wawili walimiliki mbwa ambao waliwaita Toy.
Miaka arobaini baada ya kutengana tangu utoto wao, mapacha hawa wawili walikuja kukutanishwa tena na kuanza kusimuliana maisha yao jinsi yanavyofanana .
HAYA YOTE YAMETOKEA HAPA HAPA DUNIANI TUNAPOISHI
=====
SENGWILE MAKAMANDA