Code zinaanza kufunguka

Hakuna mtu anayeudharau uwezo wa watanzania, ni sisi wenyewe tunajidharau kwa kuendekeza tabia za ufisadi na wizi wa kila aina.
Sasa kweli unataka jambo kama hili nalo nirudie rudie kueleza kwa nini inaonekana hivyo hapa kwetu na huko kwingine kukawa ni tofauti?
Nimeeleza mara ngapi, jambo hili hili; na wewe unarudia rudia tu vile vile!

Hii haiwezi kuwa mbinu ya kunyamazisha mjadala, bali inakufanya uonekane kuwa mpuuzi tu.
Kwa hiyo kazi yangu kwako nimeimaliza.
 
Mpuuzi ni wewe unayechukulia ni kitu kipya kwa mwekezaji wa kigeni kuja kufanya kazi nchini tena kwa mkataba ulioandikwa na wataalam kwa miezi kadhaa ya majadiliano.
 
Dunia halisi haibembelezi mtu au nchi fulani, tuwekeze kwenye elimu za aina mbalimbali au tukubali kupelekeshwa na wageni wanaokuja kuwekeza kwetu, uchaguzi ni wetu kusuka au kunyoa.
 
"... alikuwa loyal" royal ni kitu kingine kabisa
 
Dunia halisi haibembelezi mtu au nchi fulani, tuwekeze kwenye elimu za aina mbalimbali au tukubali kupelekeshwa na wageni wanaokuja kuwekeza kwetu, uchaguzi ni wetu kusuka au kunyoa.
Haya maneno nenda kamwambie Samia, kwani ndiye sasa anayetupeleka waziwazi kabisa kwenye hali hiyo. unayo ieleza hapa.

Katika mambo yooote anayo yafanya kama kiongozi, hili la kuua moyo wa waTanzania kuamini kuwa na uwezo wa kujenga nchi yao ndilo la kwanza kabisa katika kumwondolea sifa za kuwa kiongozi wa nchi.
 
Mpuuzi ni wewe unayechukulia ni kitu kipya kwa mwekezaji wa kigeni kuja kufanya kazi nchini tena kwa mkataba ulioandikwa na wataalam kwa miezi kadhaa ya majadiliano.
Unaelewa kwamba hicho siyo ninacho pinga, na nimekwisha rudia mara elfu na zaidi humu.
Hakuna mahali popote ninapo pinga uwekezaji unaofuata taratibu na kuzingatia maslahi ya nchi. Wewe unapindisha ionekane napinga uwekezaji, bila kujali maelezo ninayo toa kwa sababu una tetea maslahi maalum katika uwekezaji huo. Hili ndilo limeteka akili yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…