Clouds FM wanavyovurunga akili za watu katika Ukombozi

Status
Not open for further replies.
Jul 14, 2011
22
2
Nimekuwa nikisikilize hiki kituo kwa muda sasa na kitu nilichogudua ni kwamba sio management yake wala wafanyakazi wengine wote hawako na nia ya kitufikirisha kuhusu maswala makubwa yenye maslahi mapana ya watu kama wao wanaojitambulisha na wanavojipambanua; zaidi ni kupromote mambo yasiyo ya msingi kabisa mara Wema, Diva sijui gossip na fiesta yaan basi tu almradi wawakamue wamachinga vielfu kumi vyao.

Kifupi wanatumia mwavuli wa burudani kuwatoa watu kwenye malengo, ingawa burudani yenyewe ni uhuni tu na watz tusivyo na akili wanatusomba huku Rais akiendelea kuuza nchi.

MASKINI TZ
 
si Clouds FM bali ata Clouds TV nayo ni magumashi hakuna kitu kabisa cha maana zaidi zaidi ni kuupotosha umma tu; siku kadhaa zilizopita nilimsikia Shafhi Dauda kupitia Sports Bar akiongelea sakata la Kelvin Yondani kutoka Simba kuamia Yanga nilishindwa kabisa kumuelewa kama akili yake hiko sawasawa ama la. kwa ujumla Clouds nzima ni mzigo kwa Umma wa watanzania.
DEO MAFURU hujakosea kwakweli.
 
kama watangazaji ni KIBONDE na DIVA unategemea nini??

mbona kuna media nyingi tu zimejikita katika burudani ila hazina uropokaji na upotoshaji wa namna hii
 
Well said Mafuru,

Kwanza watangazaji wake wana upeo mdogo wakufikiri alafu wanajadili mambo na kutoa msimamo kanakwamba wao ndio wanajua kila kitu.

Huwa najisikia mjinga sana kusikiliza hii redio na naishia kubadilisha stesheni.

Mfano: Mh mwakyembe kamuachisha kazi chizi. Ungesikia mjadala wake asubuhi kwenye power breakfast ungetapika. Gerlad Hando alivyokuwa akiendesha mjadala kamavile ana uhakika na anayoyasema! Wao walikuwa wanajadili kwamba Chizi kaonewa bila hata ya kuhoji wahusika.

Kwamba aliyepewa nafasi ya Chizi ni Binamu yake Mh. Mwakyembe!

Njoo kwa Kibonde wetu. Maranyingi yeye shughuli yake kutetea serekali na kuisifia kwa vijimambo vidogo vidogo wanavyofanya baada ya migomo na maandamano ya umma kuwazidia.

Kwa kifupi vijisent wanavyopata kwenye system hii mbovu vinawafanya washindwe kufikiria kabisa. Aibu kwao.
 
yani bado mnaisikiliza hiyo redio?...........niliacha toka 2009 aisee and it was too late!!!!!
 
klauz ni genge la wapaka poda na wanaume wa kujishauashaua kama madem na madem wao ni ma-cd
 
Tangu wamtimue Masoud na Fina kile kituo ni kinyaa, gerald nilijaribu kumsiliza nikajikuta nasikiliza ma#^&7shi, yaani sijaona kituo cha kutune, mwenzenu nimerejesha redio kwenye box.

Unajua masoud uzuri wake alikuwa anatoa mwelekeo wa kupata vipaji kwa namna tofauti sana, mtu wa kawaida huwezi ukagundua, bahati mbaya hakuipenda serikali, hamtetei mtu kipuuzi, Fina kalikuwa bendera
 
Hivi ni lazima uisikilize mbona mimi sisikilizi kabisa hii redio waatu mmekalia kulalamika tuu kwani una ndoa nayo...hata ndoa huvunjika ukiona mwenendo wa mwenzako siyo.....acheni kulialia kijinga
 
Hivi ni lazima uisikilize mbona mimi sisikilizi kabisa hii redio waatu mmekalia kulalamika tuu kwani una ndoa nayo...hata ndoa huvunjika ukiona mwenendo wa mwenzako siyo.....acheni kulialia kijinga

kwa namna fulani kuna mantiki ktk mchango wako: lakini si vizuri kuacha watu wenye ni mbaya wakaendelea kupotosha umma ni lazima mara moja moja usikilize na kama kuna upotoshaji ukemewe mara moja. Clouds hawajui Media Ethics zikoje.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom