Clouds FM na unazi wao kwa CCM

Clouds FM na unazi wao kwa CCM

mpingauonevu

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
621
Reaction score
434
Nilikuwa busy usiku kucha. nikalala saa kumi na nusu alfajiri kushtuka nikakuta PB on saturday ambayo wanapitia mambo yote muhimu ya wiki.Nilipoamka ili kusikiliza & nikakuta wameipa coverage hotuba ya merry Nagu kwenye kampeni za arumeru mashariki. Merry anavyojinadi kwa mambo aliyoyawezesha wakati akiwa waziri wa viwanda na biashara.

Baadae wakampa coverage Sioyi Sumari akajinadi nikategemea kumsikia Nasari na Vicent wapewe nao ola. Labda kama walianza nao ndipo nitawaelewa! Sasa nilipojua kwamba sio bahati mbaya kwenye mapitio ya magazeti wakadai wamepata matatu tu! JAMBO LEO, MAJIRA na MTANZANIA! sasa Jambo leo si ni la magamba! habari iliyosomwa kwa kirefu ni propaganda za jambo leo!Kwamba CCM wameshamaliza kazi!

My take:
Kwanini tunailalamikia clouds? kwa miaka mingi tumekuwa tunaiheshimu kwa uwezo wao wa kutoa burudani na ubunifu. Leo Peoples station mtakubalije kuwa CCM Station? Hivi kweli SUPER BRAND mnaweza kuamua kutuvunja moyo vijana kiasi hiki? Tunajua magamba wanaweza kuwavamia kwa kuwa wanajua mnainfluence ya vijana lakini kwani si wote tunajua vijana wa sasa hawataki kufanywa wajinga?

AU MMEJISAHAU?
 
Kusaga amekubali kutumika na wanasiasa itamcost!! Clouds = Radio Uhuru = TBC!! Kuwa oppurtunist lazima uwe kichwa kweli otherwise utajuta!
 
U must be an a intelligent person.Mimi nilisikiliza PB on Saturday yote ila baada ya hiyo coverage nilituma sms kwenye no yao walioitoa 15678, nikawauliza mbona coverage ilikuwa kwa CCM pekee je kwa vyama vingine vipi?.Kwa kweli nilitegemea hata angesoma sms yangu ila duuuuuuuu..Kwa ujumla Clouds sio entertainment Radio labda ilipoanza early 2000.Kwa sasa wamenunuliwa na CCM au labda hawalipi kodi kama mdau alivyosema..Sijui ila kama ni redio ya watu lazima iwe mfano.Hata vipindi vyake fulani fulani siku zote ukisikiliza ni KCCM ccm tu..Inabidi wabadilike au tuseme basi na wenyewe wako kama radio Uhuru aka CCCCCCMMMMMMM
 
Vipi Cloud ingetoa hotuba ya Vincent Nyerere na Mgombea Nasari kisha ikasema gazeti lililopatikana ni Tanzania Daima pekee. Ungekuja kulaumu kwa kuipendelea CDM? bila shaka sivyo ndivyo.
 
Wacha tu walambe viatu vya mafisi adi.watajibeba tu muda c mrefu!
 
Vipi Cloud ingetoa hotuba ya Vincent Nyerere na Mgombea Nasari kisha ikasema gazeti lililopatikana ni Tanzania Daima pekee. Ungekuja kulaumu kwa kuipendelea CDM? bila shaka sivyo ndivyo.

niukweli ambao hauhitaji mjadala kwamba clouds fm wanatumika kwa sasa na ccm.
 
Vipi Cloud ingetoa hotuba ya Vincent Nyerere na Mgombea Nasari kisha ikasema gazeti lililopatikana ni Tanzania Daima pekee. Ungekuja kulaumu kwa kuipendelea CDM? bila shaka sivyo ndivyo.

Hiyo sio sababu, tunachosema unapotoa taarifa kwa jamii lazima uangalie mfumo wa vyama vingi uliopo.Sasa kama ni radio ya jamii lazima kuwa na mawazo chanya ili sie tunaosikiliza tuweze kipima.Kwani CCM leo hii ndiyo imejua swala la ardhi ni tatizo kwa Wameru ama.Hoja ya Nagu ni kuwalaghai wananchi kwani kwa miaka 50 CCM ndiyo ilikuwa mwakilishi wa lile jimbo halafu ukuizingatia tatizo wanalijua.Mikataba iliyoingiwa wenyewe wanaijua sasa ni vipi wanataka kuwalghai wananchi eti wameliona na swala la uwekezejai litaanagaliwa ili ardhi iliyo mikononi mwa watu wachache ichukuliwe na kugawiwa wananchi.Hii ni hoja finyu, tumeona katika sera na ahadi nyingi za CCM ni nyakati za campaighn tu, baada ya hapo yaani usahau kupata ufumbuzi.Yaani hii hoja ya Nagu haina mashiko ni ulaghai kwa Wameru na kwa kuwa wameona maji yamewafika shingoni.
 
Vipi Cloud ingetoa hotuba ya Vincent Nyerere na Mgombea Nasari kisha ikasema gazeti lililopatikana ni Tanzania Daima pekee. Ungekuja kulaumu kwa kuipendelea CDM? bila shaka sivyo ndivyo.

Hapa mtoa maada kasema wamechukua nafasi ya radio uhuru badala ya radio ya watu wote kama wanavyojinadi.
 
Wamesahau kuwa uma ndo umewafikisha hapo walipo na pindi uma ukiamua utairudisha "ALFA"
 
U must be an a intelligent person.Mimi nilisikiliza PB on Saturday yote ila baada ya hiyo coverage nilituma sms kwenye no yao walioitoa 15678, nikawauliza mbona coverage ilikuwa kwa CCM pekee je kwa vyama vingine vipi?.Kwa kweli nilitegemea hata angesoma sms yangu ila duuuuuuuu..Kwa ujumla Clouds sio entertainment Radio labda ilipoanza early 2000.Kwa sasa wamenunuliwa na CCM au labda hawalipi kodi kama mdau alivyosema..Sijui ila kama ni redio ya watu lazima iwe mfano.Hata vipindi vyake fulani fulani siku zote ukisikiliza ni KCCM ccm tu..Inabidi wabadilike au tuseme basi na wenyewe wako kama radio Uhuru aka CCCCCCMMMMMMM

Lakini mbona wametoa mchango mkubwa sana katika kuhamasisha uchangiaji wa CHADEMA kule ausha katika tangazo lao?
 
  • hakuna cha kujadili hapa...me nafikiri bwana mkubwa umechelewa tu kujua hilo, siku nyingi inajulikana clouds ni kituo cha magamba, isipokuwa mara chache sana huwa wanajishebedua tu
 
Nawasikitikia wale vijana shababi wote wasikilizao clouds radio ya ccm. Miliacha siku nyingi sana kuisikiliza hiyo radio from 2010. Pale ambapo kibonde alipoonyesha kuipendelea wasiwasi ccm na kuiponda waziwazi cdm hewani tena kwenye redia inayodaiwa kuwa ni ya wat na siyo ya ccm. Nilikipenda sana kili=e kipindi cha jahazi, siku yangu ilikuwa haipiti bila kusikiliza na nilikuwa lazima nicheke kwa utangazaji wao. Lakini kwa dosari hile aliyoionesha kibonde. Sijawahi kusikiliza tena.

Its better tukaanzisha kampeni ya zuia kusikiliza clouds ccm radio. Nyumbani, ofisini, kwenye daladala na kwingineko.
 
Just a charcoal dont expect anything white

Cha muhimu ni kuwa vyama vya upinzani kuwa na media zao.Tutabaki tukilalamika kila siku lakina hilo jambo la ccm kubebwa na vyombo la habari halitakwisha leo wala kesho.Mbowe kama ana gazeti la Tanzania Daima ,hashindwi kabisa kuanzisha redio yake na Tv,kama sio yeye mwenyewe Chadema wanaweza kuanzisha Redio na TV,wakiomba kibali wakinyimwa wawashitaki TRCA kwa umma.Media is power hii inajulikana dunia kote,C'm on wapinzani time is now hao clouds wako kwenye pay roll ya ccm na kupata matangazo ya biashara wanahitaji sana baraka za serikali kwa hiyo hawawezi kuwatupa
 
Nawasikitikia wale vijana shababi wote wasikilizao clouds radio ya ccm. Miliacha siku nyingi sana kuisikiliza hiyo radio from 2010. Pale ambapo kibonde alipoonyesha kuipendelea wasiwasi ccm na kuiponda waziwazi cdm hewani tena kwenye redia inayodaiwa kuwa ni ya wat na siyo ya ccm. Nilikipenda sana kili=e kipindi cha jahazi, siku yangu ilikuwa haipiti bila kusikiliza na nilikuwa lazima nicheke kwa utangazaji wao. Lakini kwa dosari hile aliyoionesha kibonde. Sijawahi kusikiliza tena.

Its better tukaanzisha kampeni ya zuia kusikiliza clouds ccm radio. Nyumbani, ofisini, kwenye daladala na kwingineko.

kibonde alipewaga kasuti na jk nayeye akawa magamba hakuwaga hivyo pomba ni hando na pj tuu.wengine wote magambaziii!!!
 
Nawasikitikia wale vijana shababi wote wasikilizao clouds radio ya ccm. Miliacha siku nyingi sana kuisikiliza hiyo radio from 2010. Pale ambapo kibonde alipoonyesha kuipendelea wasiwasi ccm na kuiponda waziwazi cdm hewani tena kwenye redia inayodaiwa kuwa ni ya wat na siyo ya ccm. Nilikipenda sana kili=e kipindi cha jahazi, siku yangu ilikuwa haipiti bila kusikiliza na nilikuwa lazima nicheke kwa utangazaji wao. Lakini kwa dosari hile aliyoionesha kibonde. Sijawahi kusikiliza tena.

Its better tukaanzisha kampeni ya zuia kusikiliza clouds ccm radio. Nyumbani, ofisini, kwenye daladala na kwingineko.

mbona ishaanza, vinega wote hawasikilizi wafu fm.
 
Walianza taratibu lakini sasa naona unafki wao unaaanza kijipambanua! Jana kwa masikio yangu nimemskia mmoja wao pale sijui anaitwa gerad hande anawahamasisha watu wa mwanza wakamsikilize mgombea udiwani wa kirumba kwa ticket ya magamba na akawa anamsifia kimtindo, huyu najua ni njaa tu labda baadae alitumiwa kivocha kwa promo maana maisha ya mjini nayo yanawafanya watuwazima watumike vibaya! Natangaza rasmi kuacha kusikiliza hiki kiredio maana kuna radio stations kibao tu mjini hapa. Majuzi kati wamemzushia mheshimiwa Mnyika wakiwa wamesahau kuwa kila mtu anahaki ya kuuliza swali but pia kila mtu anahaki ya kuamua ajibu lipi na kuacha anayoona niyaki.pu.mba.vu
 
Back
Top Bottom