Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,809
- 34,193
Bi. Hillary Clinton
Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Democratic, Bi. Hillary Clinton amesema endapo ataingia madarakani, linaweza kuwa wazo zuri sana kumteua Rais wa sasa wa nchi hiyo, Barack Obama kuwa Jaji wa Mahakama Kuu nchini humo.
Bi. Hillary Clinton ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali aliloulizwa na mpiga kura katika mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na watu takribani 450 Jimbo la Iowa, ambapo raia hyo alimtaka Clinton aeleze iwapo baada ya kuwa rais wa nchi hiyo, anaweza kufikiria kumteua rais Obama kuwa Jaji wa Mahakama Kuu kwa sheria za nchi ya Marekani zinaruhusu rais atakayeingia madarakani ana kuteua majaji watatu wa Mahakama Kuu, shirika la habari la ABC News limeripoti.
Rais Barack Obama
“Lo! Hilo ni wazo zuri sana. Hakuna mtu amewahi kupendekeza hilo kwangu,” alisema Bi. Clinton.
“Nalipenda sana wazo hilo. Anaweza kuwa na mambo mengine kadha ya kufanya, lakini nakwambia hilo ni wazo zuri sana.”
“Ni mwerevu sana, na anaweza kutetea hoja vyema, na alikuwa profesa wa sheria, kwa hivyo amehitimu,” alisema.
“Sasa, tunahitaji kuwa na Bunge la Seneti linalodhibitiwa na Chama cha Democratic ndipo aweze kuidhinishwa, kwa hivyo mtanisaidia kufanya hilo, tumekubaliana?”
Bi Clinton, alishindana vikali na Obama kuwania tiketi ya kupeperusha bendera ya urais mwaka 2008 lakini akashindwa na baadaye Obama alipoingia madarakani akamteua kuwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni.
Clinton: Naweza Kumteua Obama Kuwa Jaji Mahakama Kuu