Mwanamitandao Clemence Mwandambo amesema amekuwa akitumia video anazochapisha mtandaoni katika kuwashauri wanasiasa na kuwasilisha mawazo yake, lakini mara nyingine wanasiasa wamekuwa hawataki kuambiwa mawazao tofauti na wakiambiwa hivyo wanaona kama wanaowaambia wana kiburi.
"Kwa bahati mbaya sana tuna wanasiasa machifu hawataki ni watu ambao hawataki kusikia wazo kinyume na wanavyofikiri wakiona unatoa wazo kinyume na wanavyofikiri wanakuona kama una kiburi"
Ameeleza kuwa kutokana na kuwa hayupo kwenye mfumo wa kufanya maamuzi serikalini yeye video zake ndiyo njia ya kufikisha ujumbe.
"Mimi sipo kwenye 'system' ya serikali lakini nikipaza sauti kupitia simu labda naweza nikasikika lakini wanakua hawaamini maoni yangu" ameongeza Mzee Mwandambo