Class of 1999 - 2015 Je ni specimen ya majaribio?

Class of 1999 - 2015 Je ni specimen ya majaribio?

DENLSON

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
957
Reaction score
1,281
Huwa najiuliza sana bila kupata majibu kwa nini hili darasa limekuwa likipitia changamoto nyingi sana. Wengi wao ni vijana walizaliwa kati ya mwaka 1988-1993 ambao walianza shule ya msingi yaani darasa la kwanza(Standard I) mwaka 1999.

Darasa hili limekuwa likipitia changamoto nyingi ntazitaja chache kati ya hizo.

1.Mwaka 2005 huu ndio mwaka ambao hawa vijana walikuwa wakimaliza elimu ya msingi. Huu ndio mwaka ambao idadi ya mitihani iliongezeka kutoka 3 mpaka 5. Ikumbukwe hapo awali mtihani wa kuhitimu darasa la saba ilikuwa ni Hisabati, Lugha (Uswahili +English) Maarifa (Sayansi, Uraia na Sanaa)

2. 2006 wakati vijana wakiwa form I Selikari kupitia wizara ya elimu walibadilisha mtaala wa elimu walikuja na Physchemistry lakini wao ndio wawe waanzilishi wa huo mtaala mpya hapa waligroup physics pamoja na chemistry kama somo moja. Hili swala lilileta mkanganyiko sana ilibidi baadae liondolewe.

3. 2010 hapa pia Selikari kupitia wizara ya elimu walileta mtaala mpya kwa wale wa waliosoma masomo ya sanaa maswali yalipunguzwa toka 15 mpaka kumi yaani walipunguza choices na options za maswali kwa kuwa mtu alitakiwa kujibu maswali 5 kati ya 10 tofauti na zamani ambao mtu anajibu 5 kati ya 15.

Pia kwa baadhi ya masomo hasa ilikuwa ni lazima usome topic zote kwani kila topic ina swali hili jambo halikuwepo miaka ya nyuma.

4. 2015 Baada ya kuhitimu chuo kikuu wakakumbana na kisanga cha "NO JOB" Hapa kwa waliosoma Education wanaelewa vizuri kitu ambacho hakikuwepo huko nyuma ambapo ilikuwa ukimaliza chuo umesoma education unajua tayari ni muajiriwa.

I am too sad to be one of them [emoji25] [emoji25] [emoji25] [emoji25]
 
Pole sana dogo. Ni jambo la kawaida vitu kubadilika. Chukulia kama changamoto ya kukabiliana nayo,
 
Back
Top Bottom