Civil engineering VS Mechanical engineering(kwa level ya diploma)

Civil engineering VS Mechanical engineering(kwa level ya diploma)

IWAMBI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2018
Posts
730
Reaction score
624
Wakuu habari zenu,naombeni msaada kati ya course mbili hapo juu ipi unafikiri ni nzuri na ungependa kumshauri mtu asome..naomba mtu anayezijua vizuri hizo course anichambulie katika maeneo yafuatayo kwa makini ili niweze kufanya maamuzi

1.Civil engineering na Mechanical engineering zinahusu nini na zinajikita katika nyanja zipi za uhandisi

2.Mtu akisoma civil or mechanical anaweza kufanya kazi maeneo yapi

3.Ipi inawigo mpana wa ajira haswa katika private sector

4.Ipi inayolipa sana kati ya hizo mbili na inawigo mpana wa kujiajiri

Wakuu naombeni nisaidieni hivyo vitu...mtu yoyote mwenye mchango kuhusu course yoyote nzuri ya engineering anaruhusiwa kuweka mchango na mtazamo wake
 
Ukisoma civil unaweza fanya kazi barabarani, ujenzi wa nyumba, kazi za maji...

Ila Zote ziko poa japo civil is the best of all.
Ahsante sana mkuu...kumbe civil hata kazi za maji unafanya na vipi kuhusu wigo wake wa ajira katika private sector
 
Jamani na engineer njooni huku
 
Civil na mechanical zote ni nzuri sana ...

Civil unaweza jiajiri kwa kufungua kikampuni cha ujenzi nyanja zote majumba,barabara ,maji hata designing za ramani ..

Mechanical unaweza jiajiri mwenyewe kwa kufunguni workshop za magari, air conditions and refrigeration, unaweza fanya uchongaji wa vipuri kwa fitting za aina zote (kwa kifupi mechanical inauwanja mpana sana kama ukisoma vizuri darasani na ukazielewa modules vizur theorical na practically.

Mwenyewe hapa nimesoma mechanical engineering pale DIT ,nimefungua tuviwanda tudogotudogo
 
Mainjinia wako busy sio kushinda kwenye mitandao kama wanasiasa
Mkuu wanaoshinda humu si wote wanasiasa kuna madaktari,walimu,wanasheria NK....wanasiasa wapo jukwaa lao kule
 
Ok...ahsante mkuu..vipi kuhusu fursa ya kuajiriwa haswa private sector..pia hizo course mtu anaweza fanya kazi katika maeneo gani
 
Back
Top Bottom