Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 169
- 287
Maonyesho ya 8 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yanafanyika mjini Shanghai. Ikiwa ni maonyesho ya kwanza ya kitaifa duniani yenye mada ya uagizaji, CIIE yanasaidia bidhaa za kilimo za Afrika kupata umaarufu katika soko la China.
Katika maonesho hayo yanayofanyika kila mwaka nchini China, maeneo ya bidhaa za Afrika huwavutia watu wengi. Kutoka siagi ya shea kutoka Afrika Magharibi hadi kahawa maalum kutoka Afrika Mashariki, kutoka divai ya Afrika Kusini hadi tende za Afrika Kaskazini, bidhaa hizo maalum za kiafrika zimeingia soko la China kupitia CIIE. Takwimu zinaonyesha kwamba thamani ya biashara kati ya kampuni za Afrika na wateja wa China inaongezeka kila mwaka, kati ya bidhaa hizo, bidhaa za kilimo zimechukua kiasi kikubwa zaidi.
Bidhaa nyingi za kilimo za nchi za Afrika zimekuwa na umaarufu nchini China kupitia CIIE katika miaka ya hivi karibuni. Bidhaa mbalimbali za kilimo za Afrika zikiwemo matunda kutoka Afrika Kusini, kahawa ya Ethiopia, pilipili ya Rwanda, korosho za Tanzania, asali ya Zambia, ambazo awali zilioneshwa kwenye CIIE, sasa ni maarufu sana katika soko la China. Tangu awamu ya kwanza ya CIIE, mauzo ya bidhaa za kilimo za Afrika nchini China yameongezeka kwa miaka saba mfululizo. Takwimu zinaonesha kuwa katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu, China iliagiza bidhaa za kilimo kutoka Afrika zenye thamani ya dola bilioni 3.6 za Kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 7.2 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki.
Wakati Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wa mwaka 2024 ulipofanyika Beijing Septemba mwaka huu, Rais Xi Jinping wa China alitangaza kwamba China imeamua kusamehe ushuru wa fordha kwa bidhaa za nchi zote zilizokuwa nyuma zaidi kimaendeleo ambazo zina uhusiano wa kibalozi na China, zikiwemo nchi 33 za Afrika. Pia kwenye mkutano huo, China ilisaini makubaliano mengi na nchi za Afrika kuhusu mauzo ya bidhaa za kilimo nchini China: yakiwemo makubaliano na Zimbabwe kuhusu mauzo ya parachichi nchini China, makubaliano na Zambia kuhusu mauzo ya soya, na makubaliano na Msumbiji kuhusu mauzo ya mbaazi, macadamia na korosho. Bidhaa hizi za kilimo za Afrika zinatarajiwa kuonekana kwenye CIIE ya mwaka huu na kuwa nyota ya kesho katika soko la China.
Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na China kufungua mlango zaidi kwa Afrika, bidhaa nyingi zaidi za kilimo za Afrika zimefanikiwa kuingia kwenye soko la China. Hadi mwishoni mwa Agosti mwaka huu, China imesaini Makubaliano 22 na nchi 14 za Afrika kuhusu kuuza bidhaa za kilimo katika soko la China. Licha ya hayo, majukwaa ya kuhimiza biashara yaliyoanzishwa na China ikiwemo CIIE yamesaidia bidhaa za kilimo za Afrika kuunganishwa moja kwa moja na soko la China, na kupata umaarufu kwa haraka nchini China.