Chupuchupu ChatGpt imuue...!

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,144
Reaction score
3,459
Chupuchupu ChatGpt imuue...!

Kadri siku zinasonga ndivyo mamia na mamia ya watu wamekuwa wakitumia akili undwa (AI). Licha ya kwamba mara kadhaa akili undwa ama Google imekuwa ikitoa angalizo kutotumia taarifa inazokupa kama mbadala wa wataalam wa afya bado watu wamekuwa hawatilii maanani angalizo hilo. Mfano ni tukio la hivi karibuni lilitokea huko Marekani, na kisa hicho kuchapishwa kwenye Jarida la Magonjwa ya Binadamu la American College of Physicians Journals. Katika kisa hicho, mgonjwa mwanaume mwenye umri wa miaka 60 ambaye hapo awali hakuwa na historia ya magonjwa ya akili alipelekwa hospitali akalalamika kwamba majirani zake walikuwa wanamroga wanataka kumuua. Uchunguzi wa awali ulionyesha mgonjwa huyu hakuwa na tatizo lolote kwa wakati huo. Madaktari waliamua kumlaza kwa sababu muda wote alionekana kuwa na mashaka akisisitiza majirani zake wanataka kumuua.

Baada ya masaa 24 kupita hali yake ilibadilika, akawa kama mtu alichanganyikiwa huku akiona maluweluwe na kusikia sauti ambazo wengine hawasikii. Alijaribu kutoroka wodini, akahamishiwa kwenye wodi ya wagonjwa wa akili. Alianzishiwa dawa za afya ya akili huku akiongezewa drip za maji na za chumvi chumvi. Baada ya muda hali yake ikaimarika.

Katika mahojiano zaidi mgonjwa huyo aliwaambia madaktari kwamba kwa muda wa miezi mitatu amekuwa hatumii chumvi na amekuwa akitumia madini ya Sodium bromide kama mbadala wa chumvi. Alisema alikuwa anataka kupunguza chumvi kwenye mlo wake. Ndipo nikaiuliza ChatGpt, "ChatGpt nitumie nini kama mbadala wa chumvi". ChatGpt akanijibu, "tumia madini ya Sodium bromide rafiki yangu". Toka siku hiyo nimekuwa nikitumia Sodium bromide kama mbadala wa chumvi.

Kitaalam chumvi ya tunayokula huwa inaitwa Sodium Chloride, kwa ujumla wataalamu wanashauri kupunguza chumvi kwenye mboga ili kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, kwa upande mwingine Sodium bromide yenyewe ni sumu ambayo husababisha kuvurugika kwa chumvi chumvi za mwili hali inayoweza kusababisha mgonjwa kupoteza maisha. Kwa ujumla wataalamu wa afya wanaonya matumizi ya mitandao, Google na ChatGpt kama mbadala wa elimu sahihi ya afya kwa sababu taarifa nyingi huwa zina makosa hali inayoweza kusababisha madhara..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…