Chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere kitainua mkoa"Mulongo"

Binda News

New Member
May 2, 2016
1
1
KUANZA kwa Chuo Kikuu cha Kilimo na Sayansi cha Mwalimu Julius K.Nyerere,kilichopo wilayani Butiama mkoa wa Mara kitaupandisha na kuuinua mkoa katika masuala mbalimbali pamoja na kuwasaidia wakulima katika kuinua kilimo.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Mara,Magesa Mulongo,alipotembelea sehemu ya majengo ya iliyokuwa shule ya Osward Mang'ombe High School ambayo yatatumika kama "campas"ya chuo hicho kinachotarajiwa kuanza kupokea wanafunzi oktoba mwaka.

Amesema chuo hicho ambacho kitatoa shahada na stashahada za fani mbalimbali licha ya masuala ya kilimo itakuwa chachu kubwa ya maendeleo ya mkoa wa Mara na wananchi watakaokuwa wanazunguka mazingira ya chuo na kuwataka wananchi kujiandaa kukipokea.

Mulongo ambaye alikuwa ameongozana na viongozi wa ngazi ya wilaya,alisema cha kwanza ambacho kinapaswa kuangaliwa ni kuhakikisha migogoro ya aina yoyote baina ya chuo na wananchi haipatikani yakiwemo masuala ya ardhi ili uongozi wa chuo ufanye shughuli zake bila kubugudhiwa.

"Kwanza ni heshima kubwa kuwepo na kuletwa kwa chuo hiki mkoa wa Mara na hususani kwenye wilaya ya Butiama katika kumuenzi mzee wetu Mwalimu Julius Nyerere na ni muhimu kinapokwenda kuanza kusiwepo na vikwazo vya aina yoyote.

"Lakini chuo hiki kitaupandisha na kuuinua mkoa wa Mara maana mahala popote palipo na vyuo au chuo kikuu licha ya mkoa kunufika lakini pia wananchi wananufaika kutokana na fursa mbalimbali ambazo watazipata kutoka kwa wanachuo,"amesema Mulongo.

Amesema kutokana na taarifa ambazo amepewa na uongozi wa chuo hicho,wananchi wakulima wa kawaida pia watapata fursa ya kupata kozi fupi ambazo zitawasaidia kuboresha shughuli zao za kilimo na kuwaomba wananchi kujiandaa na hilo.

Akitoa taarifa ya chuo hicho baada ya kuteuliwa na Rais wa awamu ya nne,Jakaya Mrisho Kikwete,kuanza mchakatato wa chuo hicho,Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaruma,profesa Lesakit Mellau,amesema wameshafikia hatua kubwa ya kuanza kwa chuo hicho ikiwemo kuanza kuajili wahadhiri.

Amesema bado kuna masuala ya fedha kutoka serikalini yasubiliwa kutokananza kupokea na bajeti na mambo yakienda vizuri kufikia oktoba wataanza kupokea wanafunzi.

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Butiama waliozungumza na Mtanzania kuhusiana na chuo hicho walisema wapo tayari kutoa ushirikiano kutokana na manufaa ambayo watayapata kutokana na kuwepo kwa chuo hicho katika maeneo yao.
 
Mwaka huu material ya chuo ni ghali sana waambie waanze na stashahada kwani wanafunzi watakaoenda chuo ni wenye one na two sasa hao wanafunzi wa degree WAENDE mara chuo kipya waache SUA? Ngoja tuone mwaka huu vyuo vitaruka sarakasi gani.
 
KUANZA kwa Chuo Kikuu cha Kilimo na Sayansi cha Mwalimu Julius K.Nyerere,kilichopo wilayani Butiama mkoa wa Mara kitaupandisha na kuuinua mkoa katika masuala mbalimbali pamoja na kuwasaidia wakulima katika kuinua kilimo.

"Kwanza ni heshima kubwa kuwepo na kuletwa kwa chuo hiki mkoa wa Mara na hususani kwenye wilaya ya Butiama katika kumuenzi mzee wetu Mwalimu Julius Nyerere na ni muhimu kinapokwenda kuanza kusiwepo na vikwazo vya aina yoyote.
Tuache sarakasi. Chuo Kikuu kuia sehemu? Rasilimali watu iko wapi? Vilivyopo vinatosheleza mahitaji? Nionavyo miye tunakoelekea Tanzania itapoteza kabisa hadhi ya elimu ya juu hasa ile ya Chuo Kikuu! Kwa maoni yangu, Mwalimu Nyerere angekuwa HAI ASINGEKUBALI Chuo hicho (i) Kuitwa kwa Jina lake (kama alivyo fanya kwa SUA na Uwanja wa Nelson Mandela-Sumbawanga) na (ii) Asingependa Chuo hicho kijengwe Butiama....
 
Asante sana Mkuu Wa mkoa wetu magesa mulongo tunaomba ukipe chuo hicho maximum supervision tuko pamoja na wewe sisi wana ambao tuko nje ya mkoa huo.tunapata faraja kusikia habari nzuri toka ktk mkoa wetu maana tumechoshwa na habari mbaya za mauaji kutoka mkoani kwetu.kwa habari hii tunafarijika sana
 
Chuo cha Siasa na Kilimo..hakitakuja kuisha kwa awamu hii ya kukurupuka! Poleni sana Mulongo na wana Mara
 
Back
Top Bottom