Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hii si haki kabisa!

Guus

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
1,131
823
Leo nimejikuta nacheka kama vile ni mazuri, kiasi kwamba nikamkwaza muhusika aliyekuwa anasimulia.

Iko hivi: Kuna jamaa yangu ofisini aliomba "admission" chuo kikuu cha Dar es Salaam ili aanze masomo ya Uzamivu mwaka huu wa masomo (2018/19). Ametuambia kuwa utaratibu wa UDSM ni kuwa maombi yote yalikuwa yakifanyika "online". Alichostaajabisha ni pale alipotuambia kuwa hadi sasa akiingia kwenye "portal" inaonesha "Application status: On Process" wakati kiuhalisia ni kuwa shule imekwisha-anza!

Binafsi nilicheka lakini naona hii si sawa kabisa, hasa pale unaposikia kuwa muombaji alilipia! Hii si sahihi kabisa kwa taasisi inayotengeneza "wataalamu" kushindwa kuwa na utaratibu mzuri wa kuhudumia wateja wake. Nimejiuliza tu kama "wabobezi" wenyewe hawalioni hili vipi wale wanaofundishwa masomo kama "marketing"!! Ama ndiyo "chema chajiuza..."!!
 
Yawezekana tatizo lipo kwangu.
Labda wengine wataelewa kilichokuchekesha.
 
Back
Top Bottom