Chuo cha urubani Tabata?

Kutoa taarifa hapa JF ni namna mojawapo pia ya kufikisha ujumbe kwa wahusika kwani naamini baadhi ya informers wao ni members wa JF. Kumbuka hata swala la Lwakatare inasemekana source yake ilikuwa JF.

sio mbaya kuja kutoa taarifa humu ila ingekuwa bora zaid angeanza kuripoti polisi kwanza
 
Kwa Wana Jamii wote,
Pale kwenye kile chuo hawatoi kozi za urubani never never.Hawana hata nusu ndege.Kile chuo kimesajiliwa na TCAA,na wana ruhusa ya kufundisha Flight Operation Officer au kwa jina lingine Dispatchers.Ni Approved Training Organization for hiyo kozi tu.Ila huyo mjomba anawahadaa watu kuwa kuna kozi ya urubani ili kushawishi wanafunzi wengi.Kusoma urubani ni zaidi ya dola 60,000.Pale hamna mwanafunzi alietoa hiyo ada.
Tatizo ni kudanganya kuwa kuna kozi ya urubani,sijui kwa nini asiseme ukweli kuhusu hili.
TCAA has never approved the chuo to train Pilots,hana vigezo kwa sasa,labda mbeleni akitimiza.
Thats the truth and only truth..period.
 
umeongea vizurisana zamani nilikuwa na wazo la kuwa rubani na his kama umenikumbusha kitu?vp wanachukua degree ya aina gani kuwa urubani.

Siku za ajabuurubani hauna awards ya degree/ diploma wala hauna graduation(mahafali)! Urubani ni udereva hivyo baada ya kuhitimu mafunzo hupewa Leseni ya kukutambulisha sehemu yoyote ile. Kwa msingi huo basi, mtu yoyote yule wa degree yoyote anaweza kuwa rubani so far kama ametimiza vigezo na masharti. mf. Mtu makini, mwenye uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka sana even within fraction of seconds, n.k Pia hii kazi inahusu mambo ya usalama ,ni kazi nyeti na malipo yake yapo juu sana lakini pia ni kazi ambayo unaifanya kwa masaa tu! Yaani kuwa rubani ni raha kweliii!!
 
Hivi hiki chuo siku hizi kimefungwa pale Tabata? Sioni billboards zao kwenye lile jengo ilipo CRDB Bank kwa muda mrefu sasa.
 
Wajinga ndo waliwao kwani hao wazazi na wanafunzi ni matahira??
 
Hiki chuo kweli ni cha kitapeli! Niliwahi kuwa na mahusiano na ndugu wa huyo mwenye chuo, wote ni wasabato, LAKINI JAMAA huwa hataki hata mke wake afike hapo chuoni. Kwa sababu ya tabia zake za kizinzi

Hata ndugu zake wanamsema sana kwa iyo tabia yake.
 
Mimi natokea Tabata! Nasari pia kabisa katoliki Kristo Mfalme Magengeni pale.Nimewai kwenda na kuchukua fomu pale, kiufupi wana idea nzuri sana lakini Mazingira yanawatupa mkono.Kozi zina bei, ada ndogo kabisa ni million 1 na lakin sita, lakini mazingira ya kusomea ni finyu sana. Mimi naona ajipange zaidi, kwa kuwa nimeona kipo katika mfumo wa theory(nasharia) zaid kuliko Vitendo.Tumpe Moyo!
 
Raha sna sema tatizo ni ISIS, wanatudungua huko huko juu
 
Mi najua kozi ya urubani inanzia million 50 mpaka million 60 kwa mwaka kwa wenzetu na sasa sijui bongo imekaaje na ni kozi ngumu kweli kweli yenye kutaka mtu awe ameiva vizuri kwenye geography, physics na mathematics.otherwise tunajidanganya.
 
Tatizo sio chuo kua Tabata ,tatizo ni kweli wanafanya hayo mafunzo na taratibu za nchi zimefuatwa ??? Kuna chuo sijui KIU wanafunzi wapo tokea sijui mwaka gani kumbe hakina usajili ,aliyeleta mada ametahadharisha tu maana hakuna kisochowezekana Tanzania,unaweza ukaambiwa kuna kiwanda cha kutengeneza Submarines kipo Dodoma unabaki tu kushika mdomo
 
Reactions: bdo
kweli watanzania wana matatizo ya akili , yaani hawajashituka kuwa jamaa anawapiga hela na wanafunzi kapata.
 
Lile bango lao la kunadi school of aviation silioni hapa kwenye jengo (tabata magengeni) inawezekana kimetumbuliwa tayari
 
peleka
ushahidi kwenye taasisis za Polisi , Takukuru uone rungu litakavyomshuki pia usisahahu kuwakumbusha NACTE humu jf yatakuwa majungu mkuu halafu jamaa atazidi kutamba tu.
 
Aviation...aeronautical engineering..in tanzania!! Ila sishangai wakubwa wezi watoto wataacha kua wezi??
nao hao wanaopeleka wanafunzi na kulipa ada wameuliza accreditation za chuo hiki kabla?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…