Chuo cha ualimu Kleruu kukatiwa huduma za umeme na maji ni halali?

Kwatozakuku

Member
Oct 4, 2015
24
14
Chuo cha Ualimu Klerruu kiko mjini Iringa chenye kutoa mafunzo ya Ualimu kwa ngazi ya cheti na diploma ambacho pia chuo kikongwe hapa nchini na kimetoa walimu wengi sana wa masomo ya sayansi. Lakini chuo hiki ni kwa muda mrefu kimekuwa kikikatiwa huduma za umeme na maji na kwa muda huu chuo kimekatiwa umeme takribani mwezi sasa hadi kulazimika chuo kufungwa kwa wanafunzi wa diploma.

Na leo hii chuo huenda kikakatiwa huduma ya maji. Nashindwa kuelewa kunashida gani hadi chuo kikatiwe huduma hizi. Kwasas bado kuna wanachuo wachache wa ngazi ya cheti lakini usalama wao na chuo kwa ujumla ni shida maana usiku ni gizi totoro na chuo ni kikubwa ambapo pia hali ya ulinzi ni mbaya.

Natumai wahusika wanataarifa na hili tatizo kama hawana basi ni vizuri wakalishughulikia kwa maendeleo ya taifa.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom