Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,874
Chuo kikuu cha shenyang kutoka nchini China kimeahidi kutoa ushirikiano na Shirika la ndege la Air Tanzania kwa kutoa msaada wa kuwasomesha wafanyakazi wa kampuni hiyo,ili waweze kumudu ushindani wa soko la kimataifa.
Hayo yamesemwa na mwalimu wa malezi wa chuo cha Shenyang, Shi Guangda katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Global Education Link kwa wazazi ambao watoto wao wanasoma urubani na Masuala ya anga katika chuo hicho.
“Tangu Rais wetu wa China alipofika hapa tumekuwa na mahusiano makubwa na nchi hizi mbili, hivyo kwa kuanza kama chuo chetu tutatoa ufadhili kwa wafanyakazi wa shirika la ndege la Air Tanzania na kubadilishana mafunzo katika chuo cha usafirishaji cha NIT na Shenyang” Amesema Guangda .
Kwa upande wa Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Air Tanzania,Ladislaus Matindi ameishukuru tasisi ya Global Education Link kwa kuwaunganisha na chuo hicho ambacho kwa sasa kimekuwa msaada mkubwa kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
Matindi ametaja kuwa upatikanaji wa nafasi hiyo itasaidia kutoa motisha kwa vijana wetu ambao wanafanya kazi katika shirika hilo na wengine ambao wako nje kuwa na hamu ya kusoma masuala ya usafirishaji .
Kwa upande wake mkurugenzi wa Global Education link , AbduMalik Molell alitumia fursa hiyo kuzungumza na wazazi hao juu ya swala la bima ya wanafunzi amabo wanasoma chuo hicho katika swala zima la matibabu na majanga mengine ambayo yatawakuta wanafunzi.
Chanzo: Michuzi