Chuo cha hali ya hewa na elimu isiyotambuliwa na necta

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
Habari wasomaji wote.

Ningependa kuwashirikisha wanabodi wote hapa ya kuwa katika serikali hii ya JMT kuna mamlaka inayojishughulisha na masuala ya hali ya hewa nchini. Kuna watu wengi pengine hawajui ni sifa zipi unatakiwa kuwa nazo ili usomee utaalamu huo. Kwanza lazima uwe na elimu ya kidato cha sita na uwe umemaliza masomo ya fizikia, kemia na hesabu.Nyongeza jiografia.

Sasa, chuo kinachotoa elimu hiyo hapa nchini kipo Kigoma. Kinatoa level mbili. Kwanza level ya Technician yaani hii ni Junior technician level ya mwaka mmoja.Pili ni ni Senior level ya miaka miwili. Lakini tatizo kubwa la elimu hii ni kuwa hata usome ukafikia level zote mbili bado elimu hiyo haitambuliwi na bodi husika ya elimu kama Nacte na Tcu. Kwa hiyo hapa hupati cheti chochote unachoweza kumwonyesha mtu yeyote. Zaidi unapewa leaving certificate ambayo hutaipeleka kokote. Kabla ya chuo hiki kuanzishwa mwaka 1983, wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi katika mamlaka hii walipata elimu yao nchini kenya kutokana na kwamba secta hii ilikuwa ndani ya jumuia kama ilivyokuwa Mamlaka ya anga au simu na posta.

Baada ya jumuia kuvunjika mwaka 1977, tanzania ikajikuta haina chuo tena cha kutoa elimu hii. Wenzetu nchini Kenya chuo chao kimesajiliwa na wanafunzi wanaopata elimu hiyo wanapata vyeti vya ufaulu wao.HAPA KWETU CHUO HIKI BADO HAKIJASAJILIWA NA HII INAWAFANYA WANAFUNZI WANAOMALIZA CHUO HIKI KUENDELEA KUBAKI KAMA FORM SIX LEAVER TU.MBAYA ZAIDI HUWEZI KWENDA KUAJILIWA SEHEMU NYINGINE KWA SABABU HUNA CHETI CHA ELIMU HIYO.NI SERIKALI TU AJIRA YAKO.

SWALI KUBWA NINALOJIULIZA NI KUWA NACTE WAKO WAPI KUKIFUNGA CHUO HIKI?HUKU NI KUENDESHA MAMBO KIENYEJI SANA.WAZIRI MWAKYEMBE HIKI NI CHUO CHAKE HIVYO NAMWOMBA AKISIMAMISHE KWANZA HADI KITAKAPOSAJILIWA.

kutokana na haya wewe una maoni gani na elimu hii?Toa maoni ya kujenga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom