Chunga Sana, Matapeli Ni Wengi

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2016
Posts
2,111
Reaction score
1,494
Wandugu, poleni na maangaiko ya maisha na shughuri nyingi za mwisho wa juma.
Tupo katika kipindi chenye changamoto nyingi sana, watu wenye hekima wanapungua sana, ambao kama wangekuwepo tungewaendea na kuhojiana nao na wangetupa majibu kwa maswali mengi tulio nayo, kama ilivyo kuwa kwa Aristotle, Socrate na plato.

Tofauti na kipindi hicho, leo, tunawaamini sana watu wanaotumia Jina la YESU, kuliko hata wanao tumia jina la Moh'med.It's good! Hapa ndo penye shida, hasa watu hawa wanapo taja jina la Yes badala ya YESU, na wengine hawana hata biblia ila maneno na visa vya kukoleza kutoka kwenye biblia.

Any way, sijaja kukosoa bali kuweka tahadhari, na kukufahamisha kwahaya yafuatayo:
Matumizi ya Ndoto; Baadhi ya watu wanaodai kuwa Watumishi wa Mungu wamekuwa wakitumia njia ya Ndoto kutumiza makusudi yao maovu au kujipatia faida kutoka kwa watu wanaowahudumia, HAWA HUJA NA STAILI AU USEMI UNAOSEMA NIMEOTESHWA ; Angalia sana, mtu anasema nimeoteshwa na Mungu kuwa utakuwa mke wangu,Wakati huyo mwanamke tayari anamume wake .SWALI LAKUJIULIZA NIKWELI NDOTO HIYO IMETOKA KWA MUNGU?

Biblia inasema '' YEREMIA 23:25'' Nimesikia waliyoyasema manabii wanaotabiri uongo kwa jina langu ,wakisema nimeota ndoto. HUSIDANDANYWE NA WANAO SEMA OOOH KATIKA JICHO LA ROHO, NIMEONA. MMMMM!!!!! Maandiko yanafafanua zaidi : MHUBILI 5:3,7 Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno. Maana ndivyo ilivyo katika habari za wingi wa ndoto, na ubatili, na maneno mengi; walakini wewe umche Mungu.

Maisha taiti kila mtu anapambana na hali yake kwa njia tofauti tofauti, sasa hawa wengine wanatumia njia hii kupata MAPATO YA AIBU. TITO 1:11 Hao wanapindua nyumba nzima ,wakifundisha yasiyowapasa KWA MAPATO YA AIBU. Chunga sana husiamini kila mtu,Omba MUNGU atakusikia.
 
WEWE NI NABII NANI VILE?
 
Utawatambua kwa matunda yao,mwisho wa yote nini
maudhui ya kaz yake inampa Mungu nafasi zaidi au niyeye mwenyewe?ujumbe wake unamaslai binafsi?mana tunakoelekea hata wale walio wachache wa kweli hawaaminiki,tusipokaa na kujifunza biblia au qurwan kwa undani,niamini tuatakua tunampa shetani nafasi kubwa sana kama vile Mungu hawezi kutenda hayo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…