Chumvi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chumvi

Discussion in 'JF Doctor' started by Exaud J. Makyao, Jan 27, 2010.

 1. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wataalamu naomba kama kuna madhara ya mtu kuwa akitumia chumvi kwa wingi katika chakula.
   
 2. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wataalamu wa mambo ya tiba mko wapi kwa ufafanuzi ni kweli nilishawahi kusikia kwenye simulizi kwamba too much umunyu is catastrophic...........
   
 3. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ......Chumvi ni muhimu kwa afya yako ya mwili lakini ukizidisha inaweza kukuletea matatizo.
  Kiasi cha kawaida cha chumvi kinasaidia mwili wako kuwa na normal blood, blood pressure, nerves and muscle functions.
  ......Ukizidisha chumvi sana unaweza kupata matatizo ya moyo na damu, hivyo ni vizuri kupunguza kiasi cha chumvi kwenye mlo wako.
   
 4. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante Pretty.
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Matumizi makubwa ya chumvi ndiyo chanzo kikubwa cha magonjwa ya moyo. Utafiti uliofanyika nchini Uingereza ulionyesha asilimia 72 ya watu waliokuwa wanatumia chumvi kwa wingi walikuwa wanaogua magonjwa ya moyo au matatizo katika mishipa ya damu (cardiovascular diseases).

  Lakini madhara ya chumvi yanatofautiana kulingana na unavyoitumia. Kwa mfano kula chumvi kavu (table salt) kama ile ya kuongeza kwenye nyama choma au unayoweka kwenye parachichi, ina madhara makubwa zaidi kuliko chumvi unayoipika pamoja na mboga.

  Utafiti mwingine uliowahi kufanyika huko Astralia ulionyesha kwamba watumiaji wa chumvi nyingi hasa wanaokula nyama choma, walikuwa wana uwezekeno mkubwa wa kupata magonjwa ya mifupa pia (osteoporosis). Nafikiri daktari wa JF atatusaidia zaidi.

  So itumia kwa kiwango kidogo kwa kadri iwezekanavyo. Lakini zaidi sana epuka chumvi ya kuongeza baada ya kupika.
   
 6. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Vangi,
  Maelezo yako yamekaa vizuri sana,
  Mpaka umekumbuka PARACHICHI?
  Kumbe hata maembe.
  Tusubiri wengine mkuu.
   
 7. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wataalamu wanaema kuna madhara la madhara makubwa ni yale ambayo yanatokana na kutumia chumvi kwenye chakula mabcho kimeshapikwa na mtumiaji kutumia kwa kuongeza wakati anakula. Kwa kifupi kuna madhara kwa chumvi inapozidi kwenye chakula bra Makyao
   
 8. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  chumvi itumiwe kwa kiasi na pia usipende kula chumvi mbichi! Kuna watu wengine wanatabia ya kuongeza chumvi mezani! Hiyo tabia sio nzuri kwani chumvi ina vidudu vidogodogo ambavyo vinakufa ikipikwa!
   
 9. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Samahani kwa kuvamia mjadala. Mimi ningependa mnijulishe hapa hapa madhara chanya ya sukari nyingi kupita kiasi. Niliwahi kutaka kuanzisha sredi, lakini naona hii inatosha kuijadili sukari pia. Nazungumzia sukari ya kawaida ya kutia kwenye chai, sizungumzii glucose et al. Ni vyema pia nikajua maximum allowable amount of sugar per tea-cup
   
 10. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kuongeza kiwango cha sukauri kwa wale wenye upungufu wa sukari mwilini
   
 11. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,747
  Likes Received: 376
  Trophy Points: 180
  kanunue guyton ya physiology usome vizuri kitabu kizima halafu utusidie
   
 12. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ok, na madhara hasi ya sukari ni yapi?
   
 13. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asante Mumy kwa maelezo mazuri

  Swali la nyongeza eti chumvi ina faida gani kwenye mapenzi?
   
Loading...