Kim Jong Jr
JF-Expert Member
- Mar 15, 2014
- 10,984
- 20,396
Habari wanajamvi...
Siku za hivi karibuni kumezuka kikundi cha vijana waharifu wanaotumia mapanga, visu, fimbo na malungu kufanya unyang'anyi kwa raia wa eneo tajwa au wapita njia wasioishi eneo hilo..
Mwezi uliopita Mwanafunzi wa chuo cha ustaw wa jamii alinusurika kifo baada ya kucharangwa mapanga na kuibiwa kila kitu alipokuwa akielekea chuoni kwenye tamasha la michezo ya chuo akitokea hostel za nje mida ya alfajiri.. Tukio hilo lilitokea karibu na ofisi za Kituo cha sheria na haki za binaadamu....
Wiki jana pia Mzee mmoja anaeishi eneo la nyuma ya chuo cha ustawi wa jamii alichomwa visu tumboni na vibaka hao muda wa saa kumi na moja asubuhi wakati akielekea kusali kanisa la ROMA Mwenge... Huyu mzee kwa sasa ana hali tete sana nasikia amelazwa muhimbili japo sina uhakika sana juu ya hilo..
Juzi usiku mbele ya ofisi za ofisi ya kituo cha sheria (LHRC) dereva wa bodaboda alitekwa na kuchomwa na bomba la kutolea moshi wa pikipiki kisha akaibiwa pikipiki na kujeruhiwa kwa mapanga..
Kikundi hiki kimekuwa kikitumia pikipiki au bajaji kufanya shughuli zao... Wakiwa kwenye shighuli zao endapo wakikukuta upo peke yako wanakushambulia kwa mapanga bila kuuliza na kukuchukulia kila kitu...
Jana nimenusurika kifo nilikuwa natokea makumbusho mida ya saa tano usiku nikielekea makongo juu. Niliamua kupitia shortcut ya barabara ya nyuma ya chuo cha ustaw wa jamii kwa kuingilia njia panda ya sayansi...
Nilipofika eneo karibu na Kituo cha sheria na haki za binaadamu ambapo barabara ina mashimo mengi sana. Niliona kikundi cha watu kama ishirini yaani 20 kikiwa kimeshika mapanga na visu na wengine wakinoa mapanga kwenye lami.. Nilichanganyikiwa saaaaaaaaana... Ile barabara ni nyembamba kwa ambao wanaifahamu si rahisi kugeuza haraka haraka... Wakati najiuliza namna ya kuguza nikimbie vijana wanne wakawa wamefika hatua chache karibu na gari wakinipa ishara ya kushuka... Nilichokifanya ni kukanyaga mafuta nikijiapiza lolote liwe mpaka nikaenda kutokea kona ya bar ya hongera....
Matukio ni mengi saaaaaaana kama ukipata muda wa kuongea na wenyeji...
Nilisikia kuwa mwaka jana pia kuna mwanafunzi wa cho cha ustawi alinisurika kifo alipotekwa na kunyang'anywa tiketi za ndege za wanafunzi waliokuwa wanaenda alfajiri hiyo kupanda ndege kwenda uganda kwenye ziara ya kimasomo...
TUNAOMBA ULINZI UIMARISHWE ENEO HILO KWANI NI HATARI KWA WAPITA NJIA NA WAKAZI WA ENEO HILO