Chuki za Roy Hodgson kwa wachezaji wa Leicester city kuiondoa England mapema euro 2016

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
127,927
244,503
Sasa ni dhahiri kwamba kocha huyu kikongwe anazo chuki binafsi.

Katika hali ya kawaida huwezi kumwacha benchi Jamie Vardy kama unataka kushinda , hii ni ajabu !

Ukiangalia kwa makini Vardy kila nafasi anayopata ndani ya 18 hesabu ni goli , habahatishi , kwenye game kama hizi usitarajie kupata nafasi nyingi sana , kwahiyo unahitaji mchezaji mwenye uwezo na asiyefanya ajizi kama Vardy .

First touch yake haina mfano , sasa unamuachaje benchi ?

Alimuacha DrinkWater akaleta mshangao dunia nzima , sasa hii shilingi nyingine anayoichezea itamrudisha nyumbani mapema sana , Hakuna striker wa England wa kumuweka benchi Vardy , utake usitake .
 
Nadhani kama angekuwa hamuhitaji (kwa chuki kama ulivyoandika) basi asingemwita kabisa kikosini.

Nadhani kocha mwenyewe anajua kwanini hakumchezesha.
Hana lolote analojua , yule mzee kavurugwa mkuu .
 
nimeshangaa hata mie kwa moto wa vardy kukaa benchi ni hujuma maana jamaa ana kasi sana na namba 9 yake siyo yakusubiria mipira kama kane
 
Sasa ni dhahiri kwamba kocha huyu kikongwe anazo chuki binafsi.

Katika hali ya kawaida huwezi kumwacha benchi Jamie Vardy kama unataka kushinda , hii ni ajabu !

Ukiangalia kwa makini Vardy kila nafasi anayopata ndani ya 18 hesabu ni goli , habahatishi , kwenye game kama hizi usitarajie kupata nafasi nyingi sana , kwahiyo unahitaji mchezaji mwenye uwezo na asiyefanya ajizi kama Vardy .

First touch yake haina mfano , sasa unamuachaje benchi ?

Alimuacha DrinkWater akaleta mshangao dunia nzima , sasa hii shilingi nyingine anayoichezea itamrudisha nyumbani mapema sana , Hakuna striker wa England wa kumuweka benchi Vardy , utake usitake .
Na kingibe cha ajabu ni vile Harry Kane kawa mpiga kona na Sterling mbili kimo yupo ndani ya box.. Anyway England ni kama Taifa Stars..hawafiki mbali.
 
Wewe ungekuwa ndiyo kocha wa Uingereza, ungechezesha wachezaji gani? Tupia kikosi chako cha kwanza na akiba!
Stelling na Wilshere hata benchi wasingekaa! Kikosi mbele lazima kingekuwa na 4-4-2 mbele Vardy na Kane pmbeni Roney na Milner,kati Dier na Ali hapo full mzigo anapigwa yoyote
 
Back
Top Bottom