Chuji arejea Jangwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuji arejea Jangwani

Discussion in 'Sports' started by nngu007, Nov 12, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]


  na Dina Ismail

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  HABARI ndiyo hiyo! Mabingwa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Yanga imemsajili kiungo wa zamani wa Simba, Athuman Idd ‘Chuji’ kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo na michuano ya kimataifa, imefahamika.  Habari za kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Yanga, zinasema kwamba, Chuji alimwaga wino wa kuichezea timu hiyo kwa miaka miwili baada ya kukamilisha mazungumzo na viongozi wa kamati ya usajili.

  “Ni kweli Chuji tumemsainisha mkataba wa miaka miwili, baada ya kukamilika kwa mazungumzo, hivyo Chuji ni mmoja kati ya wachezaji watakaovaa uzi wa kijani na njano katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa,” alisema kiongozi mmoja wa Yanga ambaye hakupenda kutajwa jina lake.


  Hata hivyo, huenda klabu hiyo ikaingia tena katika mgogoro wa kumgombea kiungo huyo na mahasimu wao, Simba, ambao mwaka huu ilimsainisha mkataba wa miaka miwili kabla ya kumpeleka kwa mkopo Villa Squad.


  Hali ya kuuzwa kwa mkopo Villa Squad, haikumridhisha Chuji, ambaye aligoma na kudai yuko radhi kuuza karanga kuliko kwenda kuichezea timu hiyo inayosuasua kwenye ligi hiyo.


  Kama hiyo haitoshi, Chuji alitishia kuchukua sheria kwa Wekundu wa Msimbazi, ambako kupitia kwa mwanasheria wake, alitishia kusimamisha ligi iwapo asingerejeshwa Simba, lakini Simba walibaki na msimamo wa kutokubali kumtumia kiungo huyo, sambamba kudai wameishavunja naye mkataba.


  Nalo Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya msigano huo, liliendelea kusisitiza kuwa Chuji ni mali ya Simba, kwa kuwa aliingia nao mkataba wa miaka miwili, pia kuwa na leseni na ndiyo maana akapata nafasi ya kuichezea katika michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati ‘Kombe la Kagame’.


  Chuji aliwahi kuichezea Simba akitokea timu ya Polisi Dodoma, kabla ya baadaye kutimkiaYanga katika uhamisho uliozua mzozo mkubwa baina ya watani hao wa jadi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Chuji kigeugeu mara hana mara pale
   
 3. M

  Maswalala Senior Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya sasa kaaaz kwelkwel ila wacha tuone ifikapo mwishon mwa mwezi huu tutajua mbivu na mbichi, ukweli au uzush
   
 4. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 848
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Au YAnga ndio vigeugeu?​
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Kwanini asije OLJORO JKT? Hakuna mhamasishaji wake ampe ushauri wajamen? Huyu kiungo namkubali na nitamhakikishia anapata NO ya kudumu.
   
Loading...