Hbr zza usku wajameni ninaumwa kichwa ambacho hakiskii dawa wala chochote hadi sa nyingne nashindwa kuongea wala kula mnisaidie, sjui tatizo n nn? Msaada nifanyeje ama nina ugonjwa unaosababisha hv sjui, yaan kinaweza kufululiza hata sku tano tu. Sa hv mpaka nishaacha kunywa pain killer kabisa. Nkinywa maji sasa yaan nkienda kukojoa inabdi nishikilie mishipa ya kichwa ndo kinazdi kabisa
Mambo mhimu ya kuzingatia:
1: Fika kituo cha afya/hospitali.
2: Onana na daktari ukiweza kumwona daktari bingwa wa magonjwa ya ndani/physician itakuwa vyema zaidi.
3: Utahitajika kutoa historia ya ugonjwa wako kikamilifu. Jinsi kichwa kinavyouma, ukali wa maumivu unaongeka kadri siku zinavyopita au kiko vilevile?
4: Utatakiwa kuonyesha mahusiano ya maumivu ya kichwa na hali za kimaisha kama stress, kukaa na njaa mda mrefu, kusafiri, kelele, mabadiliko kwenye upataji usingizi, unywaji wako wa maji nk.
5: Utatakiwa kuelezea vitu au hali zinazoambatana na maumivu ya kichwa: kutopenda kelele, kutopenda mwanga au kichefuchefu?
6: Utatakiwa kuonyesha ni maeneo gani hasa kichwa huuma na jinsi kinavyouma?
7: Utatakiwa kuonyesha mahusiano ya kichwa na unaposimama au kukaa au kuinama?
8: Mahusiano na baadhi ya vyakula kama mtindi, chokoleti, perfume na vyakula vya kusindika?
9: Daktari ataomba ufanye vipimo kulingana na mtakapofikia na maswali hapo juu.
10: Msingi wa yote hapo juu ni kujua tatizo na jinsi ya kukushauri ili lisikutokee mara kwa mara kwa kuzuia visababishi au kuzuia ukali wa tatizo linapokuwa limeanza.
Nakutakia tiba njema.