dm2000inter
Member
- Oct 27, 2010
- 29
- 10
Wana JF,
Kama mtakumbuka, Jumamosi ya tarehe 18.4.2015 kada wa CCM Moshi mjini, Buni Athman Ramole aliingia katika mkutano wa CCM kata ya Pasua kwa mbwembwe na kudai ameilipia helkopta hiyo hadi Oktoba.
Jana kwenye mkutano mwingine wa hadhara amekanusha helkopta ile sio ya Mzee Ndesamburo bali ni ya kampuni ya General Aviation Services na kutoa nyaraka kwenye mkutano wa hadhara aliyodai ameilipia helkopta hiyo hadi Oktoba.
Imethibitika rasmi kuwa Helkopta hiyo ni ya Mzee Ndesamburo na General Aviation ina mkataba wa kukodi Helkopta hiyo toka kwa Ndesa kila wanapopata mteja. Je, hiyo inamuondoa Ndesamburo kuwa mmiliki wa Helkopta?
Pili hebu tazameni nyaraka aliyoisambaza kwa wananchi kama ni uthibitisho wa malipo au aliomba tu bei ya kukodi helkopta?.
Tazameni uongo huu wa kada anaywtaka kuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa tiketi ya CCM.
Hivi anafikiri wananchi wa Moshi ni mbulula?