Chopa ya Chadema yamchefua Godfrey Zambi

Chopa ya Chadema yamchefua Godfrey Zambi

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
[h=2][/h]
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi amekerwa na hatua ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutumia helikopta na kupandikiza maneno ya uongo kwa wananchi kuhusu mchakato wa Katiba Mpya. Kutokana na hali hiyo, amewataka wanachama wa CCM kutotishika na vitisho vinavyotolewa na wanasiasa kutoka CHADEMA, ambao hutumia muda mwingi kueneza propaganda dhidi ya CCM.

Kauli hiyo ameitoa jana, kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa, ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa inajadili ajenda ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Zambi, ambaye pia ni Mbunge wa Mbozi Mashariki (CCM), alisema kumekuwepo na vitisho vinavyotolewa na baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani na kudai kuwa CCM imeteka mchakato wa mabaraza ya Katiba Mpya ikiwa na lengo la kupitisha mapendekezo ya chama hicho.

“Vyama vya upinzani hasa CHADEMA kimekuwa kikizunguka na helikopta na kufanya mikutano mbalimbali ikiwa na lengo la kueneza chuki kwa wananchi wakatae mabaraza haya na kushindwa kutoa mapendekezo yao,” alisema.

Alisema, utoaji maoni kwenye mabaraza umekuwa ukifuata taratibu na mifumo iliyowekwa na Tume ya Katiba, hivyo CCM ni moja ya Taasisi ambayo nayo ina haki ya kutoa maoni yake kwa mujibu wa sheria.

“Tume ya Katiba inapaswa kufuata taratibu zake zile zile na kupuuza maneno yanayotolewa na wanasiasa kwenye majukwaa ambao muda mwingi wamekuwa wakisema uongo kwa wananchi,” alisema Zambi.

Alisema, CCM bado ina nafasi kubwa ya kutoa maoni yake kuhusu mapendekezo ya rasimu ya Katiba, kwani asilimia kubwa ya wapinzani wanazungumzia juu ya kuvunja Muungano uliopo sasa.

Hata hivyo aliwataka wanachama wa chama hicho kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao, ikiwemo kuvunja makundi yote na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka 2014.
 
mbona sijaona hay
o alisema yamepotoshwa na chadema? Au anasema bila kuonesha huo uwongo wa chadema. Habari haijakamilika!
 
mbona sijaona hay
o alisema yamepotoshwa na chadema? Au anasema bila kuonesha huo uwongo wa chadema. Habari haijakamilika!
Tangu lini akili za ki ccm zimewai eleweka? Nadhani alichanganyikiwa na ile nyomi
ya watu na bado.
 
Godfrey Zambi, ana dhambi sana, yaani mpaka anakerwa na choper, punguza dhambi Mr Zambi, uende kutubu, sijui kuungama, whatever na imani yako.
 
anapaswa kutoa mifano ya uongo unaosemwa na Chadema vinginevyo ataonekana ni mla sembe anayopinga Mwakyembe.

Atabishaje kuwa CCM imengilia mchakato wa katiba mpya ili hali imeshinikiza 80/ ya wajumbe wa mabaraza hayo ni CCM. Tutegemee nini hapa

Warioba ameona mbali sana kuruhusu rasimu ya katiba kujadiliwa nje ya mabaraza ya katiba ambayo hayana maana kwa sasa
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi amekerwa na hatua ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kutumia helikopta na kupandikiza maneno ya uongo kwa wananchi kuhusu mchakato wa Katiba Mpya. Kutokana na hali hiyo, amewataka wanachama wa CCM kutotishika na vitisho vinavyotolewa na wanasiasa kutoka CHADEMA, ambao hutumia muda mwingi kueneza propaganda dhidi ya CCM.

Kauli hiyo ameitoa jana, kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa, ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa inajadili ajenda ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Zambi, ambaye pia ni Mbunge wa Mbozi Mashariki (CCM), alisema kumekuwepo na vitisho vinavyotolewa na baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani na kudai kuwa CCM imeteka mchakato wa mabaraza ya Katiba Mpya ikiwa na lengo la kupitisha mapendekezo ya chama hicho.

"Vyama vya upinzani hasa CHADEMA kimekuwa kikizunguka na helikopta na kufanya mikutano mbalimbali ikiwa na lengo la kueneza chuki kwa wananchi wakatae mabaraza haya na kushindwa kutoa mapendekezo yao," alisema.

Alisema, utoaji maoni kwenye mabaraza umekuwa ukifuata taratibu na mifumo iliyowekwa na Tume ya Katiba, hivyo CCM ni moja ya Taasisi ambayo nayo ina haki ya kutoa maoni yake kwa mujibu wa sheria.

"Tume ya Katiba inapaswa kufuata taratibu zake zile zile na kupuuza maneno yanayotolewa na wanasiasa kwenye majukwaa ambao muda mwingi wamekuwa wakisema uongo kwa wananchi," alisema Zambi.

Alisema, CCM bado ina nafasi kubwa ya kutoa maoni yake kuhusu mapendekezo ya rasimu ya Katiba, kwani asilimia kubwa ya wapinzani wanazungumzia juu ya kuvunja Muungano uliopo sasa.

Hata hivyo aliwataka wanachama wa chama hicho kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao, ikiwemo kuvunja makundi yote na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwaka 2014.

enhee!...na kuhusu kupeleka umeme kijiji cha ivugula? hilo amelisemeaje? manake wote tunajua ilani ya ccm ilisema vijiji vyoooote umeme lazima. iyula tayari umefika. ivugula je,? na ndolezi? au anataka kwanza aupeleke kwa mfazili wake pale ichesa!.... hili chopa limechelewa sana kutua ivugula!!!!! chonde chonde chonde dr. slaa pelekeni chopa ivugula. huyu jamaa atumtaki kabisa uku.
 
'Alisema, utoaji maoni kwenye mabaraza umekuwa ukifuata taratibu na mifumo iliyowekwa na Tume ya Katiba, hivyo CCM ni moja ya Taasisi ambayo nayo ina haki ya kutoa maoni yake kwa mujibu wa sheria.'

CDM sio taasisi??? mbona yenyewe kupita kukusanya maoni imekuwa uongo na upotoshaji kwenu nyie magamba?
 
hana lolote kaogopa baada ya kuona watu ni wengi sana mpaka kieleweke anadhani hii nchi wao wana hati miliki
 
Godfrey dhambi gamba linafukuta,linamuwasha mbaya kabisa....
 
Zambi amechanganyikiwa baada ya kugundua CCM haina chake Mbeya,kilichomchanganya zaidi ni ule umati uliohudhuria kwenye mkutano wa maoni ya chadema!
 
Chadema wawe makini,hawa mafisadi wanaweza kuwaambush wakiwa kwenye chopa yao kuwapunguza nguvu...
 
Zambi fanya yako iv kwanin ccm wanatetemeka kila chadema wakiwa kwenye ziara zao? Ndo maana nch haiendelei kwan ccm wanatumia nguvu na hela kupambana na chadema na siyo maendeleo ya nchi
 
mbona sijaona hay
o alisema yamepotoshwa na chadema? Au anasema bila kuonesha huo uwongo wa chadema. Habari haijakamilika!
Kwao chochote wanachosema CHADEMA, hata kama ni kizuri namna gani kinatafsiriwa kuwa ni kueneza chuki na uchochezi kwa wananchi, hasa kama kina ukweli unaowaumbua!
 
kama vipi nayeye Zambi atafute chopa maana nihiari, kama hawezi bora akae kimya aendee na misafara mireefu ya hizo V8........
 
Tunamlaum Mwampamba kwa kumuuzia jimbo huyo Zambi, Kwani Chadema ilishinda kabisa ila tu udhaifu na tamaa za kijinga za Mwampamba tukapoteza.!!
 
Siku hizi mwanaCCM kuzungumza bila kuitaja CHADEMA habari yako haipewi kipaumbele.
 
Back
Top Bottom