Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Hii Katiba tuliyonayo ndiyo itakayotuletea maendeleo ya haraka nchini mwetu, na ndiyo najua mtanikodolea mimacho, naongelea madaraka makubwa ya Raisi kwa kifupi Raisi ambaye ni Mungu mtu, kwamba anachoongea kinafanyika bila ya kupingwa popote!
Ikumbukwe kwamba sababu hasa ya vyama vya upinzani kulilia hii wanayoita Katiba mpya wala haiko kwenye maendeleo ya nchi yetu bali iko hasa kwenye ubinafsi zaidi, wanataka kuwa na Katiba ambayo itawawezesha kuingia madarakani kwa njia yoyote ile isipokuwa ya kura!
Hii Katiba yetu kwa jinsi ilivyo hakuna jinsi wanavyoweza kutumia mbinu zao kuingia madarakani kwani Raisi anaweza kuzizima na kuwacrash mara moja, lkn tukishaleta mambo ya Katiba kama ya Kenya au AK huwo ndiyo mwisho wa nchi yetu na hata hawa Wapinzania wenyewe kama wangekuwa wao ndiyo wako madarakani na Katiba hii wala wasingeigusa!
Hivyo chonde chonde, Hakuna kuigusa Katiba yetu, ibakie jinsi ilivyo kwani kwa nchi changa na masikini kama TanZania tunahitaji Raisi mwenye nguvu na aliye juu ya Sheria!

Anayetaka Katiba mpya ahamie Kenya, kwetu ni Nope!