Chokochoko dhidi ya Bunge ni uchochezi-Amani Forum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chokochoko dhidi ya Bunge ni uchochezi-Amani Forum

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Feb 22, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mabalozi wa amani ambao mwezi uliopita waliunda umoja ujulikanao kama Amani Forum wamewakosoa wanaharakati wanaoandaa maandamano dhidi ya Bunge kwa kusema kitendo hicho ni choko choko zinazoashiria uvunjifu wa amani unaofanywa na watu wenye maslahi binafsi.

  Mabalozi wa Amani Forum ambayo Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Afrika Mashariki, Dk Walid Kabourou, Augustine Mrema, Gilbert Ngua, Mariam Tawfik na Risasi Mwaulanga(katibu) walisema tamko hilo la wanaharakati ni miongoni mwa viashiria ambavyo vimeanza kuonekana yakiwemo maneno ya chini chini ya kuvunja amani ya nchi.

  Wamesema katika kuhakikisha kuwa umma unaelewa ukweli wa mambo juu ya suala zima la kulinda amani, Amani Forum kesho itafanya mkutano wake wa hadhara katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke, mwezi ujao AF itafanya mikutano mingine miwili Dar es Salaam katika maeneo ya Manzese na Buguruni kabla ya kuhamia kwenye mikoa waliyoitaja kwamba ni yenye utata waliitaja mikoa hiyo kuwa ni Mara, Arusha, Mwanza, Mbeya na ya Kusini.

  Mrema alisema, "unaposema ni maandamano nchi nzima, ni dalili kwamba yanapinga serikali nzima,” Hizi choko choko ni za nini?,” alihoji Mrema na kukumbushia kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere huku akisisitiza kwamba watu wanaohamasisha chuki lazima umoja wao ukemee vinginevyo nchi itasambaratika.

  Mrema alisema maeneo mengine ambayo mikutano yao itayazungumzia, ni juu ya maneno ya chini chini kuhusu masuala ya dini ambayo yanaashiria kuleta mgawanyiko. Alisema suala la Mahakama ya Kadhi na mchakato wa Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) ni miongoni mwa mambo ambayo watayatolea ufafanuzi zaidi ili kuondoa hali ya kukinzana miongoni mwa wakristo, waislamu na Serikali.

  Alisema kitendo cha kumwondoa Rais kabla ya muda wake ambao Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilijiwekea, kinaweza kikaleta vita. “Rais hachezewi. Kikwete mkimtishia nyau mnadhani hawezi kukitosa CCM? Katiba inampa madaraka makubwa, akitangaza.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,916
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Huu ni ujinga ...so what?
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hawa watakuwa wanalao jambo.Si bure siwaache wenyewe wafanye maandamano yao?aliyesema kuandamana ni kultea uvunjifu wa amani ni nani?aargh
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Hawa wanaojiita Amani Forum ni mamluki waliokodishwa na CCm kuvuruga hoja za msingi zinazolenga kumkomboa mtanzania toka kwenye lindi la umaskini. Tukianza na huyu walid Kaborou, mtakumbuka huyu ndio yule yule aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Chadema aliyenunuliwa na CCm halafu wakamhonga ubunge wa Afrika Mashariki! Kaborou ni mamluki ambaye CCM wanaijua bei yake hata huko kwenye bunge la Afrika Mashariki nadhani kazi kubwa anayofanya ni kuuza nchi yetu kwa the highest bidder; sasa kwa vile uchaguzi karibu unakaribia na uwezekano wa yeye kuchagulkiwa tena kuwa mdogo ndio maana wamejiunga na Lyatonga ili kujipendekeza kwa ccm ili waweze kufanikiwa kulinda maslahi yao. Juzi juzi tu Mrema amelipiwa nauli na matibabu kwenda India na muungwana ili apatenguvu za kuja kumpigia debe na sasa hivi ndio wapambe wameanza kwa kuwapiga vita wazalendo wanaotaka kuandamana kudai haki za msingi za wananchi.! Hawa ni watu wa kuwaogopa kama ukoma na aslani Mungu atawalaani hawatafanikiwa na malengo yao.
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hawa kina Kabourou na Mrema wamesahau mwaka 1995 walivyokuwa wanatuhamasisha pale jangwani kuandamana kwenda ikulu kupinga serikali wamesahau tulivyokuwa tunapigwa mabomu ya machozi leo anasema kuandamana ni uchochezi kweli pesa mwanaharamu
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...