Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya watu wa china Guo Yezhou ambaye pia ni mjumbe wa chama cha Kikomunisti cha nchini humo ametembelea makao makuu ya chama cha mapinduzi CCM Mkoani Dodoma ambacho ni chama rafiki huku akisema nchi yake inafurahishwa na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli katika kukabiliana na matumizi mabaya ya fedha za umma rushwa na ufisadi
Akizungumza mara baada ya kuwasili mjini Dodoma Naibu waziri huyo wa mambo ya nje kutoka nchini China amesema Serikali ya China na Tanzania zimekuwa zikifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ambapo pia ametumia fursa hiyo kumtaka raisi magufuli kufanya kazi kwa kufuata misingi iliyoachwa na mwasisi wa taifa hili Hayati Mwalimu Julius Nyerere ili tanzania iweze kupiga hatua kimaendeo na kiuchumi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Alhadji Adam Kimbisa ambaye ndie aliyekuwa mwenyeji wa kiongozi huyo kutoka uchina amesema chama cha mapinduzi na Serikali yake kitaendelea kudumisha ushirikiano kati ya Mataifa hayo mawili ambao umedumu kwa muda mrefu.
Tanzania na china zina urafiki wa kudumuumedumu kwa mrefu ambapo mpaka sasa ni miaka zaidi ya miaka 49 zikishirikiana katika mambo mbalimbali yakiwemo kiuchumi,siasa, jamii na usalama.
Chanzo: itv