China yakataa kutambulika kama ni Nchi iliyoendelea kiuchumi/Developed Economic Status,yasema yenyewe ni developing country.

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729
Hili linanishangaza sana,inakuwaje China ikatae status ya kuitwa Developed Economic wakati ni ya pili kwa ukubwa kiuchumi Duniani,je kuna advantages zipi anazopata kwa kuwa na status ya developing country na hasara gani anapata akiitwa Developed County.

NB:kuna Nchi fulani ipo East Africa Rais wake aliwatangazia Wananchi wake kuwa Nchi yake kwa sasa ni Donor Country/Developed County,je anayajua madhara yake maana hawa wachina wafadhili wake wanalialia hivi.View attachment 1216664
Screenshot_20190926-190321.jpeg
Screenshot_20190926-190339.jpeg
 
Marekani ni wazi kila uchao anaona China anaisogelea nafasi yake ya Economic Superpower status. Najiuliza sana kwanini siku za nyuma hatukuona US analialia? Hii ni ishara ya wazi kuwa hali ni mbaya kwa US. Akicheza ataanza kuiabudu China.
 
Siku ambayo China ataipiku Marekani najilipua na gurnet....

China ni mchuuzi tu ni sawa na mtu mwenye genge la nyanya, huku Marekani akiwa muuza duka la hardware
 
Jiwe ni kichaa. Eti donor kwa gdp ya $400!? CCM washenzi sana. Kwa resources tulizonazo tulipaswa kuwa na GDP kubwa kuliko China, lakini kwa ujinga na upuuzi wa viongozi wa CCM bado tupo hapa tulipo.

Resources gani mlizonazo za kuizidi China? Hivi unaifahamu china vizuri? Hizi porojo tunazopiga mara sijui tuna dhahabu,Almasi ooh sijui gas zimetuharibu na kufikiri labda sisi ndio nchi pekee yenye natural resources nyingi kuliko nchi yeyote duniani. Na tatizo ni kwamba hatupendi kufanya utafiti kujua nafasi ya Tanzania miongoni mwa nchi zenye resources nyingi.
Kwa taarifa yako Tanzania haimo hata kwenye top ten ya top gold producers duniani .Huyo china unayemdharau ndiye anayeongoza kwa uzalishaji wa dhahabu duniani .Kiasi anachozalisha ni karibu ya mara kumi ya kinachozalishwa Tanzania.Wanazalisha tani 400 kwa mwaka sisi tani 40.
Wao wanachimba wenyewe sisi tunachimbiwa
https://www.gold.org/goldhub/data/historical-mine-production

http://www.usfunds.com/investor-library/frank-talk/top-10-gold-producing-countries/#.XYz36UYzbIU

Hatumo hata kwenye top ten ya Almasi, Gas ,Oil nk .Hizi kelele sijui sisi ni matajiri sana ni wendawazimu tu.Yaani hata kwa Africa tupo mbali sana kulinganisha na nchi zenye resources nyingi Africa.
 
Jiwe ni kichaa. Eti donor kwa gdp ya $400!? CCM washenzi sana. Kwa resources tulizonazo tulipaswa kuwa na GDP kubwa kuliko China, lakini kwa ujinga na upuuzi wa viongozi wa CCM bado tupo hapa tulipo.
Tanzania haina GDP ya $400, labda ulitaka kusema GDP per capita ila ata yenyewe siyo $400. Ni vizuri kuikosoa serikali ila tuwe tunaweka data za ukweli au tukosoe maeneo tunayoyajua vizuri. Tofauti na hivyo tunakua kama tunapiga makelele kwenye kikao ili watu wasisikilizane.
 
Jiwe ni kichaa. Eti donor kwa gdp ya $400!? CCM washenzi sana. Kwa resources tulizonazo tulipaswa kuwa na GDP kubwa kuliko China, lakini kwa ujinga na upuuzi wa viongozi wa CCM bado tupo hapa tulipo.
Nyie hamkumwelewa JPM! Yeye alisema kwa rasilimali tulizonazo tungetakiwa kuwa 'dona country" lakini kutokana na mafisadi tumeendelea kuwa masikini wa kutupwa! Nyie mnaoendelea kumtukana rais wetu Mungu anawaona! Kama mnaona mnakerwa na juhudi za JPM hama nchi!
 
Sijasoma content nitakujibu kwa kichwa cha habari, China haijafikia status ya "developed country" per definition, na Trump kusema "they are gaming the system" kiuchumi yuko sawa (nitaelezea hapo chini baadae)

China ni superpower ikiwa ni ya pili kwa uchumi wa mkubwa duniani, ikiwa na matajiri (billionaires) wengi zaidi duniani (na maskiniwakutosha pia hata mita chache tu kutoka majiji yao makubwa na hasa vijijini--mliokaa kaa china mnanielewa), ikiwa na GDP kubwa tenashara kuliko developed countries zingine(mfano GDP ya China developing $14.2Trillion, Australia ambayo ni developed $1.5Trillion) ikienda kwenye majukwaa ya kimataifa ya uchumi na biashara bado inaangaliwa katika kundi sawa na nchi kama Zimbabwe na Bongo.

Kwanza kabisa hakuna clear cut ya definitions ya "developed country " na developing country" bara na maeneo tofauti yana maelezo yake tofauti.....hata Kigoma ujiji inaeza kuwa developed ukipenda kuiita....ingawa kutokana na WTO definitions pamoja na wachumi (maburyati) wa dunia...wameliweka hili kama ifuatavyo....

Nchi zinazo "boom" au kujikita na kutambulika katika uchumi wa viwanda huwa zinawekwa katika kundi la developing countries badala ya nchi zilizoendelea....China ikiwemo ingawa ni kama ilishagradute au inaendelea kusimama zaidi (kumbuka hapa tunaongelea viwanda kweli kweli na yenye bidhaa timilifu.

Sasa basi, kitu kinachoangaliwa zaidi kuclassify hili ni GDP per capita ama GNI per capita (WB), yaani Wastani wa utajiri wa raia mmoja mmoja ukigawanya utajiri wa nchi na idadi ya watu, roughly china GDP per capita ni $10,153 wakati angalau nchi iwe developed inahitaji GDP per capita $25,000 ama zaidi...US ina $59,484!!. Kwa hiyo idadi ya watu zaidi ya billion 1.2 inaiweka China nafasi finyu.....

Idadi ya uzazi na vifo pia inachangia vikiwa juu zaidi unakuwa nje ya mstari kuliko vikiwa chini (waliokaa china mnanielewa.

Nirudi kwenye point yangu ya kwanza kuhitimisha ..."gaming the system" ukisoma uchumi wa China haswa na kufunishwa na wao haswa utaelewa kwamba regime pia wanafurahia hiyo position ya developing na wala sio developed reason behind ni kwamba wanamkimbiza mwizi kimya kimya....hawa jamaa waliweka mkakati toka Mao era ku overtake US....,kila kitu walichokua wanafanya walikua wanataka sio wawe kama US Bali wampite kabisa wawe super power...na target yao iko by 2050 ila statics za "I wachumi" inaeza isikatize 2030! Nilishaiandikia Makala hii 2009 predicting the same na nikashawishika hadi kwenda kuusoma kwa vitendo uchumi wa hawa jamaa...mfano jana wamefungua Daxin airport ambayo ni the largest so far na wanataka by 2025 wawe wana traffics nyingi za ndege kuliko US( yako mengi....

Gaming the system Trump anaongelea mambo mengi ikiwemo reserve kubwa na foreign currency ya China iliyoko US ambayo ni kubwa kuliko yao, anaongelea devaluation/kushusha thamani ya yuan ¥ makusudi ili awe na advantage ya kuuza bidhaa nje kwa gharama kuliko anavoingiza nunua(kumbuka karibu theluthi ya bidhaa zote dunian zinatengenezewa china)

Trump na US washaona kama ni Marathon wanapumulia mashine.

Aisee mambo ni mengi nikomee hapa inakua ndefu kama Kuna swali nitakujibu, niulize lolote uchumi wa China hata ukitaka kujua kwanini walituzidi wakati tulikua pamoja na utaratibu mmoja na tukakomea njiani.

RIP Mao RIP Nyerere
 
Resources gani mlizonazo za kuizidi China? Hivi unaifahamu china vizuri? Hizi porojo tunazopiga mara sijui tuna dhahabu,Almasi ooh sijui gas zimetuharibu na kufikiri labda sisi ndio nchi pekee yenye natural resources nyingi kuliko nchi yeyote duniani. Na tatizo ni kwamba hatupendi kufanya utafiti kujua nafasi ya Tanzania miongoni mwa nchi zenye resources nyingi.
Kwa taarifa yako Tanzania haimo hata kwenye top ten ya top gold producers duniani .Huyo china unayemdharau ndiye anayeongoza kwa uzalishaji wa dhahabu duniani .Kiasi anachozalisha ni karibu ya mara kumi ya kinachozalishwa Tanzania.Wanazalisha tani 400 kwa mwaka sisi tani 40.
Wao wanachimba wenyewe sisi tunachimbiwa
https://www.gold.org/goldhub/data/historical-mine-production

http://www.usfunds.com/investor-library/frank-talk/top-10-gold-producing-countries/#.XYz36UYzbIU

Hatumo hata kwenye top ten ya Almasi, Gas ,Oil nk .Hizi kelele sijui sisi ni matajiri sana ni wendawazimu tu.Yaani hata kwa Africa tupo mbali sana kulinganisha na nchi zenye resources nyingi Africa.
Uko sahihi
Screenshot_20190926-221840_Chrome.jpeg
 
Kuna mvunjiko mkubwa sana kwa sasa unaendelea kwenye shirika la biashara duniani (WTO) world trade organisation

Ambacho kinasababisha mvunjiko huo ni Marekani anablock panelists wote wanaochaguliwa kwa ajili ya mahakama kuu ya rufaa (WTO appellate board) mpaka sasa amebakiwa panelist mmoja tu ambaye mda wake unaisha very soon. Kama hali itaendelea hivi, basi mda si mrefu WTO itaanza kufanya kazi bila mahakama ya rufaa.

Marekani inafanya hivi ili kushinikiza mabadiliko ya kimfumo na uendeshaji wa shirika hilo. Moja mabadiliko hao ni swala la categorization ya developing country.

WTO kuna category ya nchi tatu Developed, Developing na Least Developed Country (LDC). LDC ni wale ambao wapo kwenye least ya UN ya LDC, Developing ni nchi yenyewe inachagua kuwa Developing inapokuwa inajiunga. China mwanzo wa miaka ya 2000 wakati akijiunga na WTO alijdeclare kuwa yeye atawekwa kwenye kundi la Developing.

Developing country na LDC wanapata favor kwenye makubaliano mbalimbali ndani ya makubaliano ya WTO. kama vile, baadhi ya vifungu haviapply kwao, baadhi inachukua mda mrefu mpaka vianze kuapply kwao (mfano kwenye mambo ya Hati miliki na udhalishaji wa "generic drugs"), lakini pia kuna vifungu ambavyo viapply kwa wote lakini LDC na Developing countries kunakuwa na waiver visiapply kwao. Pia nchi zilizoendelea zinahitajika kuzisaidia nchi Developing countries kwa ajili ya capacity building.

hivyo kwa hizo benefits Marekani anaumia sana zinapoenda kwa China.
 
Hahahahahahhaa mkuu nimecheka sana apo mwisho
Hili linanishangaza sana,inakuwaje China ikatae status ya kuitwa Developed Economic wakati ni ya pili kwa ukubwa kiuchumi Duniani,je kuna advantages zipi anazopata kwa kuwa na status ya developing country na hasara gani anapata akiitwa Developed County.

NB:kuna Nchi fulani ipo East Africa Rais wake aliwatangazia Wananchi wake kuwa Nchi yake kwa sasa ni Donor Country/Developed County,je anayajua madhara yake maana hawa wachina wafadhili wake wanalialia hivi.View attachment 1216664View attachment 1216665View attachment 1216666
 
Back
Top Bottom