China yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,504
130726025900_cn_li_kim_pyongyang_640x360_ap.jpg


China imeiwekea vikwazo vya kibiashara Korea Kaskazini ikitangaza marufuku ya kuingiza dhahabu na mkaa pamoja na kuliuzia taifa hilo mafuta ya ndege sambamba na masharti ya Umoja wa Mataifa.

Wizara ya biashara pia imepiga marufuku uingizaji wa vyuma adimu duniani vinavyotumiwa katika bidhaa za kiufundi.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura mwezi Machi ya kuongeza vikwazo hivyo dhidi ya Korea Kaskazini.

Uamuzi huo wa pamoja unajiri baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la silaha zake za kinyuklia mnamo mwezi Januari na kuzindua kombora jingine la masafa marefu mwezi uliofuatia.

Mwandishi wa BBC huko Shanghai anasema kuwa hatua hiyo inakaribia uidhinishaji wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa ambavyo China iliunga mkono.

Wengine wana wasiwasi kwamba Beijing haifuatilii vikwazo hivyo.


Chanzo: BBC
 
duhhh korea kaskazini inakoelekea sasa siko.
tusubiri mmatokeo maana walivyovipanda ndo wanavivuna,.........
 
Mshirika mkuu anapokugeuka....Mwisho mwa utawala wa Korea Kaskazini umewadia
 
Hili saga mbona linaanza kuchanganya sasa, sababu China ndo alikuwa mshirika mkuu huko NK, something big is going down ngoja tusubiri. Ila NK naye mbishi sana nadhani alikuwa keshaandaa exit plan, sasa nadhani kabakia na Russia.
 
China anakawaida ya kupuuzia hivo vikwazo kwa kifupi haaminiki
 
Back
Top Bottom