CHINA: Uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa huru na wa haki, yaahidi kuendelea kutoa misaada

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,641
22,017
Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing amefanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mh. January Makamba Ofisini kwa Waziri huyo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao Balozi wa China amesema kuwa Serikali ya China inaamini kwamba uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika mwishoni wa wiki iliyopita ulikuwa huru na haki.

Balozi Youqing amesema kuwa Makamu wa Rais wa China ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kwake na kwa watu wa Zanzibar kwa kuendesha uchaguzi huo katika misingi ya haki na uhuru.

“Alikuwepo shuhuda wetu katika kushuhudia uchaguzi huo na alituambia kuwa ulikuwa wa haki na uhuru,” alisema Balozi huyo.

Katika mazungumzo hayo Balozi Youqing alisema Serikali ya China itaendelea kutoa misaada na kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwani huo ni wajibu wa mataifa makubwa kwa nchi zinazoendelea.

Alimhakikishia Mheshimiwa Makamba kwamba China ina mipango mingi ya ushirikiano na Tanzania, ikiwemo kwenye sekta ya umeme na itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania, ikiwemo kupitia makampuni ya China, ili kuhakikisha malengo ya Tanzania kwenye sekta ya umeme yanatimia.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Makamba alimshukuru Balozi Youqing pamoja na Serikali ya China kwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

“Ujumbe na salamu ulizotoa leo umetupa faraja Watanzania. Urafiki baina ya nchi zetu, na baina ya vyama vyetu vya CCM na CCP, ni wa muda mrefu, ni wa majira yote, na umejengwa kwenye misingi ya kuheshimiana na hauna budi kuendelezwa”, alisema Mheshimiwa Makamba.

Pia Waziri Makamba na Balozi Youqing walikubaliana kutembelea Pemba na Unguja kwa pamoja mwezi Aprili ili kukagua na kutengeneza miradi ya maendeleo kati ya China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Vilevile, walikubaliana kuhusu kutengeneza mradi mkubwa wa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na China kwenye teknolojia zitakazosaidia kupunguza matumizi ya mkaa, hivyo kuhifadhi mazingira.

Waziri Makamba pia amemueleza Balozi Youqing kuhusu hitaji na umuhimu wa ushirikiano katika kuiwezesha Tanzania kumiliki teknolojia ya uzalishaji wa nishati kwa kutumia taka ngumu zinazozagaa katika miji ya Tanzania ambapo Balozi Youqing aliahidi kulifuatilia suala hilo.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
OFISI YA MAKAMU WA RAIS.
 
BALOZI wa chin KUMBUKENI KATI YA WATU WAGENI WANAO ONGOZ KWA MATUKIO YAKIJINGA NA WIZI NCHINI MWETU NI raia wa CJHINA lazima ajipendekeze, kuna wachina wengi magerezani kwetu ni wajibu wke ajipendekeze, uchaguzi gani ulikuwa huru na haki? hata vijana wenzangu wa umoja wa viajana ccm wanajua kuwa pale mzee nkwere na njecha walicheza figisu figisu
 
Kwa tenda zote wanazopata wachina kwa rushwa unategemea watatofautiana na serikali?,sidhani..
 
Habari imetolewa na kitengo cha mawasiliano Ofisi ya makamu wa Rais kwa kauli za balozi wa China?
Mbona tamko kama hilo litolewe na ubalozi wenyewe? Ngoja tutasikia, yawrza kuwa kweli kuna kilichosemwa ila chumvi ni nyingi mno
 
Hiyo misaada wanayotaka kuitoa ni lazima tuwe macho. Ukweli ni huu hata kama baadhi ya wachangiaji humu hawatataka kuamini, Dunia hii hakuna kitu cha bure. Ukiona mtu anajileta kwako kwa kutaka kukupa vya bure ni lazima utafakari sana kabla ya kwenda kichwa kichwa ili kuvipokea, vinginevyo vya bure kuna siku vitatutokea puani.
 
China Yasema Uchaguzi wa Zanzibar Ulikuwa Huru na Wa Haki.....Yaahidi Kuendelea Kutoa Misaada na Kushirikiana na Tanzania

Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing amefanya mazungumzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mh. January Makamba Ofisini kwa Waziri huyo Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao Balozi wa China amesema kuwa Serikali ya China inaamini kwamba uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika mwishoni wa wiki iliyopita ulikuwa huru na haki.

Balozi Youqing amesema kuwa Makamu wa Rais wa China ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kwake na kwa watu wa Zanzibar kwa kuendesha uchaguzi huo katika misingi ya haki na uhuru.

“Alikuwepo shuhuda wetu katika kushuhudia uchaguzi huo na alituambia kuwa ulikuwa wa haki na uhuru,” alisema Balozi huyo.

Katika mazungumzo hayo Balozi Youqing alisema Serikali ya China itaendelea kutoa misaada na kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwani huo ni wajibu wa mataifa makubwa kwa nchi zinazoendelea.

Alimhakikishia Mheshimiwa Makamba kwamba China ina mipango mingi ya ushirikiano na Tanzania, ikiwemo kwenye sekta ya umeme na itaendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania, ikiwemo kupitia makampuni ya China, ili kuhakikisha malengo ya Tanzania kwenye sekta ya umeme yanatimia.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Makamba alimshukuru Balozi Youqing pamoja na Serikali ya China kwa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

“Ujumbe na salamu ulizotoa leo umetupa faraja Watanzania. Urafiki baina ya nchi zetu, na baina ya vyama vyetu vya CCM na CCP, ni wa muda mrefu, ni wa majira yote, na umejengwa kwenye misingi ya kuheshimiana na hauna budi kuendelezwa”, alisema Mheshimiwa Makamba.

Pia Waziri Makamba na Balozi Youqing walikubaliana kutembelea Pemba na Unguja kwa pamoja mwezi Aprili ili kukagua na kutengeneza miradi ya maendeleo kati ya China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Vilevile, walikubaliana kuhusu kutengeneza mradi mkubwa wa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na China kwenye teknolojia zitakazosaidia kupunguza matumizi ya mkaa, hivyo kuhifadhi mazingira.

Waziri Makamba pia amemueleza Balozi Youqing kuhusu hitaji na umuhimu wa ushirikiano katika kuiwezesha Tanzania kumiliki teknolojia ya uzalishaji wa nishati kwa kutumia taka ngumu zinazozagaa katika miji ya Tanzania ambapo Balozi Youqing aliahidi kulifuatilia suala hilo.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI,
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
 
Kwa hiyo CCM mnatumia wachina kuhalalisha ubazazi na ubakaji wenu wa demokrasia siyo??

How pathetic!!
 
Hata wale wachina wanaotoa fotokopi ya jero jero zetu wako ktk haki hivyo wawe huru.
 
Safi china nachowapendea mnajua kusema ukweli tu hakuna uongo wala undumila kuwili.
 
kwani walishatoa tamko kuhusu changuzi nyingine??? kama ule wa oktoba??? naomba referensi pls
 
Habari imetolewa na kitengo cha mawasiliano Ofisi ya makamu wa Rais kwa kauli za balozi wa China?
Mbona tamko kama hilo litolewe na ubalozi wenyewe? Ngoja tutasikia, yawrza kuwa kweli kuna kilichosemwa ila chumvi ni nyingi mno
MIMI nilifikiri sasa ni muda wa sisi kama taifa kujitegemea na kukataa misaada kumbe tuliyokataa ni ya wazungu wanaotutaka tusimamie demokrasia lakini tunaendelea kupokea ya wachota pembe za ndovu!!!! haya basi sawa
 
Kuna rafiki yangu mmoja anayejua sana mambo ya kiuchumi ya dunia, aliniambia kwamba nchi nyingi za magharibi zinategemea China katika maendeleo yao.
 
Kumbe kujitegemea ni kwa MCC peke yake lakini kwa uchina bado hatujaweza kujitegemea!!ccm bwana kama wamelaaniwa vile!
 
Back
Top Bottom