China na Korea Kusini zimeionya kuiadhibu Pyongyang iwapo itarusha kombora lolote

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_95571058_nkmissile.jpg

Mataifa mawili ya bara Asia, yametoa onyo kali dhidi ya utawala wa Pyongyang, kwamba itaadhibiwa vikali, iwapo itadhubutu tena kufanyia majaribio zana zake za kinuklia.

Mataifa hayo, Korea Kusini na China, yamekiri kuchukua hatua kali dhidi ya Korea Kaskazini, ikiwa tena itafanyia majaribio zana zake za kitonoradi zinazovuka mipaka ya kimataifa.

China na Korea Kusini, na hatua ya Marekani ya kutumameli za kivita hadi katika maeneo ya maji kwenye rasi ya Korea.

Taifa la Korea Kaskazini mara kwa mara limekuwa likiimarisha uwezo wake wa kivita, licha ya kuwekewa vikwazo na Umoja wa mataifa.

Kwa kweli, majaribio hayo ya mara kwa mara, yameongezeka sana chini ya utawala wa Rais Kim Jong-un.

Rais Trump wa Marekani, ameahidi "kutanzua" Korea Kaskazini bila ya kusaidiwa na China, mshirika wa pekee wa Pyongyang.

Chanzo: BBC
 
Baada ya mazungumzo ya Rais Xi na Trump, China walisema mazungumzo yalikua mazuri sana hasa kwenye mambo ya biashara.Pia ukizingatia Onyo la Trump kwamba anaweza kumchapa kiduku bila msaada kutok China, naona China kaamua amdhibiti mwanae kabla mambo hayajaharibika.
 
Wekeni akiba za maneno hao korea kaskazini watafanya hilo jaribio na hakuna kitachotokea. Je mnamuamini china mara ngapi anakiuka maadhimio dhidi ya huyo swahiba wake. Je mnafikiria kuwa china anafurahi THAAD kuwekwa korea kusini?? muda ndio utaongea
 
Mnyoa kiduku hana cha kupoteza alishawekewa vikwazo mpaka waweka vikwazo wakalala wakaamka mnyoa viduku ndiyo kwanza hana habari nao alishatengwa na dunia zamani anaishi dunia yake na siku wakimgusa huyu akili zake zinamtosha mwenyewe ni mwendo wa kushambulia tu Japan na S korea bila kujali bomu la Nyuklia litatua wapi yeye alishasema anatengeza nyuklia kwa ajili ya kujilinda na hana ugomvi na nchi ila akichokozwa kabla hashambuliwa pale Seuol na Tokyo ndiyo halali yake hana cha kupoteza
 
Sipendi kushuhudia vita kati ya Russia na USA ila kwa hawa wakorea acha watwangane ili tujionee mambo yatakavyoenda.
Hata Russia na yenyewe ikizingua inakula kipondo tuu. Muda wa kuchekeana umekwisha. Siria imegongwa na America kuonyesha kwamba sisi awa Urusi akuna kitu, sasa ile meli ya USA ilivyo kuwa inakwenda North Korea, wenyewe wameona apa ishakuwa ishu.
Sasa isitokeee Iran ikaongea chochote maana hasira zote watamalizia kwao, maana wao Iran wanataka waitoe Israel katika ramani ya Dunia
 
Hv kati ya North Korea na US nani kila siku anatoa vitisho vya kumshambulia mwenzke?!
Huyo kiduku alitoa had video jinsi atakavyoishambulia White house kwa makombora .Swali la kujiuliza hilo kombora lake litapitia wap mpk lifike US.
Anafanya majaribio ya kujilinda dhidi ya wavamizi na anasubiria avamiwe ili awashe moto. Swali la kizushi marekani ni lini mlianza kushambuliwa??? zaidi ya nyinyi kuanzisha mashambulizi
 
Wekeni akiba za maneno hao korea kaskazini watafanya hilo jaribio na hakuna kitachotokea. Je mnamuamini china mara ngapi anakiuka maadhimio dhidi ya huyo swahiba wake. Je mnafikiria kuwa china anafurahi THAAD kuwekwa korea kusini?? muda ndio utaongea
Kama mnyoa pank ana uwezo Marekani ameishapeleka manowari sasa aanze kwa kuzishambulia hizo kuliko alivyokua anaangaika kupata kombora la masafa marefu kuifikia Marekani, amerahisishiwa kazi kaletewa karibu
 
Back
Top Bottom