chimbuvu 30 hours zisha expire!

Maiti haisifiwi,
mgema akisifiwa ,tembo hilitia maji,
meli kupata pancha ndo wasubiri,
basi na miguu itaota magimbi,
chokochoko za hayawani,
pweza kaota magimbi




Bichi koko ya mbwa koko
Sijaanza okota makopo
Juzi, jana, wala leo

Sitaki mwenye mapepe
Wala mwenye marere
Hata mwenye kiherehere

Mzuka wanipanda
Taire taire najisemea
Mashua ya mtu mmoja
Iweje wapande mia?
 
hodi hodi naingia
kungwi mwalimu wao
manyakanga wanijua
kwangu hawatii neno

nawashangaa mafahali Nyani Ngabu na Bishanga
vijembe mwatupiana
pembe kutunishiana.
Chimbuvu kasia watia
chombo kisije enda mrama
ukasahau ya wahenga
jani halirudi mtini.

bishanga waelewa
kungwi nimehitimu
mwali nimemfunda
sasa angojea posa.
snowhite andaa hina
shurti umrembe kigori cacico somoe
ndani amkalizie.

komando achukue mchuma
amiliki mali adimu
mv mapenzi aiendeshe
yarabi safari salama.
 
Wewe ni kungwi hasa

 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…