Chikwete kawafunga vibwebwe hawa kwa miaka ishirini

Chikwete kawafunga vibwebwe hawa kwa miaka ishirini

October 2pm

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2023
Posts
1,124
Reaction score
1,983
Chikwete kawafunga vibwebwe hawa kwa miaka ishirini na sijui mwishowe lini Kama si mile. Na alivyopandikiza vigingi vyake, si kazi ya mlo mmoja kuving’oa, wallahi. Hata akija mwenye jina, hukuta kiti kimeshikwa kwa nanga!

We ukijifanya mnoko akufunika kama leso la Chokoraa. Alianza na Gowasa huyo alifikiria kavuka, kumbe bado yu mtoni. Kisha akamleta Nyembe, naye akachezwa kama bao la kiswahili. Akarudi kwa Fuguo, akaigeuza meza, na sasa hii round anamchamba hadi kiwambo Katani wa Bulibuli.

Yule Katani, roho yake ilianza kumsogeza kwenye meza ya Chikwete. Meza imetandikwa vyema nyama, wali, mamlaka, hata misosi ya kisiasa. Lakini Mzee Baba ah, si mtu wa mchezo huyo. Akasema: 'Hawa watoto wa mtaani wasinijazie meza, nami nina wa kwangu. Kwani Hirizimbili anashida gani. Bi Mdashi mwenyewe yuaongoza, sembuse kijana wangu Mwanaume kamili huyu!'

Unasikia? Wanaume wanapigwa chini kiroho safi, lakini cha kufanya hawana. Wamebaki wanapiga pingu za moyo kimyakimya. Na bado, mdundo haujaisha."
 
Muda ni mwamuzi wa haki atatuambia na kila kitu kitakuwa peupe
 
Hizi rafu zote mwisho ni 2025,

2026 nyikani tutashukiwa nchi mpya na mbingu mpya kabisa.
 
Back
Top Bottom