Chiku Abwao wa CDM aapa kumng'oa Lukuvi jimbo la Ismani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chiku Abwao wa CDM aapa kumng'oa Lukuvi jimbo la Ismani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Apr 27, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Viti Maalum mkoani Iringa, Chiku Abwao, ametangaza rasmi kwamba kazi ya kulitwaa Jimbo la Isimani linaloshikiliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, kuelekea uchaguzi mkuu ujao, itaongozwa na Operesheni Sangara ya chama chake.

  Abwao ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Iringa, amesema Bunge limemalizika na kazi iliyobaki ni kuanza kukijenga chama chake katika mkoa huu.

  Aliliambia NIPASHE jana katika mahojiano maalumu kuwa jimbo hilo litatwaliwa na kuongozwa na Chadema katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 kutokana na ukweli kwamba tangu Lukuvi aliongoze jimbo hilo kwa kipindi kirefu, hakuna jitihada zozote anazozifanya kuwanasua wananchi katika lindi la umaskini.

  "Kama unavyojua, sasa hivi tuna kazi ya kuyakomboa majimbo yote yanayoongozwa na vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mimi nina kazi moja tu ya kumng'oa Waziri Lukuvi kwa sababu tunataka kuirejesha Isimani katika sura ya kitaifa iliyokuwa nayo miaka ya nyuma...Amekaa katika jimbo hilo kwa muda mrefu na bado wananchi wake wanafikia mahali wanaomba chakula cha msaada. Hii ni aibu," alisema Abwao.

  Akifafanua nia yake ya kutaka kuwania ubunge katika jimbo hilo, Abwao alisema Isimani ndilo eneo maarufu linalofahamika kitaifa kwa uzalishaji wa chakula kwa miaka mingi, lakini kutokana na kukosa fursa na mipango ya ushawishi kwa wananchi ili wajikwamue na umaskini, ndio sababu kuu iliyomfanya aamue kutangaza rasmi kuliwania jimbo hilo.

  "Isimani itarejea tena na kuuinua mkoa wa Iringa kuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula katika ile mikoa minne itakayokuwa ghala la taifa la chakula iwapo wananchi wataacha kasumba ya kuwabeba CCM na viongozi wao ambao kila kukicha wanakuja na mipango mibovu isiyolenga ukombozi wa mkulima," alisema.

  Kwa mujibu wa Abwao, kazi ya kukijenga chama hicho katika jimbo hilo la Waziri Lukuvi, itaanza rasmi baada ya yeye kurejea kutoka jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa dharura wa Kamati Kuu ya Chadema ambao unakwenda sambamba na mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la chama hicho.

  Source:Nipashe Ijumaa
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli hadhi ya Isimani imeshuka sana na inahitaji mabadiliko. Leo Isimani njaa tupu? Mng'oeni kwa spidi.
   
 3. k

  kwamagombe Senior Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukitaka kufanikiwa kwa jambo lolote lile uwe na wazo, mipango na nk, hivyo kama umeanza mapema hivyo ni vizuri zaidi, nakutakia mafanikio katika harakati zako na Mungu akutangulie
   
 4. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Huyu mama ni jembe la ukweli. Kaza buti mama , pia msisahau Kilolo na majimbo yote ya mkoa wa Iringa. Mbeya tumepiga hatua kubwa sana ya ukombozi, moto tunauwasha Lupa, Rungwe na Kyela. 2015 Mbeya yote itakuwa CDM.
   
 5. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nitafadhili pikipiki yangu kwa ajili ya kampeni ya kumg'oa huyu bwana
   
 6. P

  PJS Senior Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana mama,wewe ni mpigania haki na utu wa mwanadamu,tunakutakia kila la heri tupo nyuma yako ktk mapambano haya.
   
 7. blackberry m

  blackberry m JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 542
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 80
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Mbunge wa Viti Maalum mkoani Iringa, Chiku Abwao, ametangaza rasmi kwamba kazi ya kulitwaa Jimbo la Isimani linaloshikiliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, kuelekea uchaguzi mkuu ujao, itaongozwa na Operesheni Sangara ya chama chake.

  Abwao ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Iringa, amesema Bunge limemalizika na kazi iliyobaki ni kuanza kukijenga chama chake katika mkoa huu.

  Aliliambia NIPASHE jana katika mahojiano maalumu kuwa jimbo hilo litatwaliwa na kuongozwa na Chadema katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 kutokana na ukweli kwamba tangu Lukuvi aliongoze jimbo hilo kwa kipindi kirefu, hakuna jitihada zozote anazozifanya kuwanasua wananchi katika lindi la umaskini.

  "Kama unavyojua, sasa hivi tuna kazi ya kuyakomboa majimbo yote yanayoongozwa na vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mimi nina kazi moja tu ya kumng'oa Waziri Lukuvi kwa sababu tunataka kuirejesha Isimani katika sura ya kitaifa iliyokuwa nayo miaka ya nyuma...Amekaa katika jimbo hilo kwa muda mrefu na bado wananchi wake wanafikia mahali wanaomba chakula cha msaada. Hii ni aibu," alisema Abwao.

  Akifafanua nia yake ya kutaka kuwania ubunge katika jimbo hilo, Abwao alisema Isimani ndilo eneo maarufu linalofahamika kitaifa kwa uzalishaji wa chakula kwa miaka mingi, lakini kutokana na kukosa fursa na mipango ya ushawishi kwa wananchi ili wajikwamue na umaskini, ndio sababu kuu iliyomfanya aamue kutangaza rasmi kuliwania jimbo hilo.

  "Isimani itarejea tena na kuuinua mkoa wa Iringa kuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula katika ile mikoa minne itakayokuwa ghala la taifa la chakula iwapo wananchi wataacha kasumba ya kuwabeba CCM na viongozi wao ambao kila kukicha wanakuja na mipango mibovu isiyolenga ukombozi wa mkulima," alisema.

  Kwa mujibu wa Abwao, kazi ya kukijenga chama hicho katika jimbo hilo la Waziri Lukuvi, itaanza rasmi baada ya yeye kurejea kutoka jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa dharura wa Kamati Kuu ya Chadema ambao unakwenda sambamba na mkutano wa Baraza Kuu la Taifa la chama hicho.

  Source:Nipashe Jumatatu  pamoja kamanda Abwao
   
 8. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nashangaa, wakati walikuwa wanasifika sana kwa kilimo
   
 9. A

  A revolutionist Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kamanda kwa jimbo la kilolo kuna kijana mmoja anaitwa BARAKA MFILINGE ni jembe mwisho na ameazimia kuchukua jimbo 2015 na mpaka sasa aliniambia ametembelea kata za ukumbi,ihimbo,mtitu,udekwa,ilula,nyalumbu,mahenge,ruaha mbuyuni,lulanzi,ng'uruhe, mlafu,ng'ang'ange nk na anakubalika mwisho licha ya kupigwa vita na mjinga mmoja anayejiita m.kiti wa chadema clay mwitula. Naamini mhe. abwao anamfahamu huyu ndg na lazima atamsaidia ili atizime azma yake hatimaye kati ya majimbo 10/11 yaliyochukuliwa na magamba 2010 yabebwe na vijana hawa wa cdm na makini kwelikweli. Nb mhe abwao mtumieni sana jembe huyu hakika mtafika mbali kwani kijana ni jembe mno na anauwezo mkubwa wa kujieleza.
   
 10. P

  Panda Kapesi JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 284
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  Duh! naona kampeni zimeanza!
   
 11. W

  Wangama guy Senior Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Safi sana mama! Tuko pamoja
   
 12. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  Dah! huyo mama ananidai ! simpendi Lukuvi!
   
 13. RUV ACTVIST.

  RUV ACTVIST. JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 471
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli simpendi Lukuvi! ni mbabe, anakiburi, anawaona watu wengine wote kama hawana aikili, fisadi wa elimu huyu yani simpendi kwa kweli. Big up mama, nitakuja kusaidia harakati. Lukuvi lazima angoke, Ombi kwa wanaisimani HUMAN RESOURCE zilizopo kwenye kila kata zimpe support.
   
 14. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  All the best mh. Chiku. Hii style ndio tunaitaka, wakati wao wakijiuliza watarudije majimboni kwao kuwadanganya tena wananchi, sisi CDM tunapiga kazi.
  Afu umshtaki huyu lukuvi kwa wananchi wa ismani kuwa huku mjini kazi yake kubwa ni kuwa-malima wanafunzi wa IFM.
   
 15. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 882
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Kwenye katiba mpya, kura za maoni ziratibiwe na Kamisheni ya uchaguzi ya ukweli (siyo hii ya CCM)

  Kwa jinsi CDM na CCM zilivyojijengea mvuto, ni lazima iwepo taasisi itayozuia watu kupata tiketi za vyama hivi kwa kutumia hongo. Vile vile hii ni chalenji mpya kwa CDM 2015. CCM walishaizoea
   
 16. Jaji

  Jaji Senior Member

  #16
  May 1, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninakutakia harakati njema na zenye mafanikio.
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  na atamng'oa tu safari hii akapumzike kama kina masilingi
   
 18. Manywele.

  Manywele. Member

  #18
  May 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna vijana wanaharakati wasomi Frays sanga na mohamed Hamza pamoja na wengineo walishapanga kuchukua jimbo kwa kuwa ushatia nia karibu sana mama 2takupa support ya kutosha na kukufichulia madudu ya viongozi wa ccm kuanzia wenyeviti wa vijiji watendaji wao madiwani hadi huyo lukuvi karibu sana.
   
Loading...