GE2025 Chifu Wanzagi: Tumeridhishwa na uchapakazi wa Rais Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Chifu wa kabila la Wazanaki na Mwenyekiti wa Ukoo wa Burito ulio Ukoo wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere amesema kwaniaba ya Machifu wenzake na Ukoo wa Berito wanaridhika na uchapakazi wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha miaka minne madarakani, akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025 kumpa kura za ushindi.

Chifu Japhet Wanzagi amebainisha hayo leo Ijumaa Oktoba 10, 2025 wakati wa Kampeni za Mgombea Urais huyo kwenye Viwanja vya Mwenge, Butiama Mkoani Mara, akimpongeza pia kwa kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kuwa mwanamke wa kwanza kuwania nafasi hiyo katika historia ya Chama hicho.

"Umefanya kazi kubwa na nzuri sana na kwa ujumla wake unalitendea kazi Taifa hili, unachapa kazi, umepokea miradi mingi ya kimkakati kutoka kwa mtangulizi wako ambayo ilikuwa kwa asilimia ndogo sana na leo umeikamilisha. Watanzania tunaridhika sana na kazi kubwa unayoifanya." Amesena Chifu Wanzagi.

Katika hatua nyingine Kiongozi huyo wa kabila la Wazanaki amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, mshikamano na upendo uliopo kwenye jamii wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu, akisema mambo hayo ni tunu muhimu za kulindwa na zilizoachwa na waasisi wa Chama Cha Mapinduzi na waasisi wa Tanzania.
Your browser is not able to display this video.
 
Hivi mkiwa pale kwenye kijiwechenu cha kahawa hua maongezi yanafanana hivi hivi au ndio ule unaa wa Wanasii hasa?
 
1bil au zaidi ?? Kazi sanaa.....kama ndugu yenu kule Foundation ametembezewa....sembuse wewe...
 
Huyu naye ku zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…