Chifu Mangungu atangazwe mtawala bora Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chifu Mangungu atangazwe mtawala bora Afrika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RICHEST, Jul 1, 2011.

 1. RICHEST

  RICHEST Member

  #1
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chifu Mangungu wale msiomjua alikuwa ni Chifu wa Msowero,Usagara kule maeneo ya Morogoro.Hakusoma na hakuwahi kusafiri kwenda Ulaya,Marekani wala Uarabuni kutafuta wawekezaji.Aliamini kuwa kama una chema watakufuata wenyewe maana chema chajiuza.Walipita wengi kwa Chifu Mangungu wakiwemo waarabu lakini Chifu Mangungu hakusaini nao mkataba wowote wa kukabidhi nchi chini .

  Alipokuja Karl Peters Mjerumani kutoka uwekezaji la lililosajiliwa kampuni la Germany East Africa (GEA) la toka Ujerumani alikaa chini akajadiliana nao akiwa na wasaidizi wake ambao hawakusoma kabisa lakini waliosheheni busara na hekima za kujali maslahi waliokuwa makini sana katika mjadala ule.Akasaini mkataba ambao hadi leo unainufaisha Tanzania kuliko mikataba mingi ya uwekezaji iliyosainiwa na wasomi koko na vibaraka wao wa kisiasa na wapiga filimbi wa hamelini yaani wabunge koko wa Afrika wasio na roho ya huzuni kuingia mikataba nyau ya kulalia wananchi.


  Wajerumani wale wakaja wakajenga reli inayofaidisha wananchi hadi leo reli kama hiyo toka mjerumani atoke hata serikali ya Tanzania haijawahi jenga reli kama hiyo..

  Sera ya Kilimo kwanza cha kibiashara ililetwa na Chifu Mangungu kwani aliposaini tu huo mkataba kilimo cha kahawa,pamba,chai a katani kilipamba moto vijijini na wananchi wengi vijijini wa mikoa mingi ikiwemo Kilimanjaro,kagera,mbeya ,tanga,n.k

  Uchumi wao ukafunguka kwa ujio wa wajerumani ambao chifu Mangungu alisaini mkatataba nao.Kiburi cha maendeleo ya wachaga,wahaya,wanyakyusa kinatokana na mkataba wa Chifu Mangungu uliowaleta wajerumani uiowaletea shule,dini ya kilutheri,mazao ya chain a kahawa ambayo ndio asili ya jeuri zao hadi leo.


  Katika mikataba yote iliyosaininwa nchi hii hakuna uliowanufaisha wananchi kama ule wa chifu Mangungu.Kwani hata maraisi wote wa Tanzania wameufaidi kwa kufanya kazi na kulala kwenye Ikulu iliyojengwa na wajerumani walioletwa na chifu Mangungu.


  Uchumi wa Tanzania unategemea vitu kama chain a kahawa hadi leo.Maelfu ya pesa za kigeni zimeingia kupitia Mazao ya ujio wa wawekezaji hao walioletwa na mkataba wa Chifu MANGUNGU.Mkataba wa Dole gumba la mtu ambaye hata shule hakwenda kwangu naona ulikuwa mkataba bora kuliko mikataba inayosainiwa kwa mbwembwe washington,london,paris n.k leo na kalamu za pesa nyingi na masuti, kwa sahihi za kunyooka na mihuri ya bei mbaya,na mikataba iliyoandikwa kwa kiingereza au kifaransa kigumu kilichojaa uongo na ufisadi.


  Kwa heshima ya hali ya juu naomba Umoja wa Afrika umtangaze Chifu Mangungu kuwa ni Mtawala kiongozi bora Afrika wa kuigwa Afrika na pale Msowero pajengwe Chuo kikuu cha kufundisha Wabunge,mawaziri na maraisi wa Afrika Jinsi ya kusimamia mikataba ya uwekezaji Afrika.


  Sasa hivi naenda Msowero kutafuta kaburi la Chifu Mangungu kama lipo nikaliwekee shada la maua la kuheshimu mifupa yake na kuwapa pole wananchi wa Msowero kwa kufiwa na shujaa huyu miaka hiyo kabla . Anayejua lilipo kaburi la mzee huyo anijulishe jinsi ya kufika huko.


  Naomba kutoa hoja
   
 2. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,593
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  He kumbe Uwekezaji umeanza toka zamani!....
   
Loading...