SI KWELI Chid Benz afariki

SI KWELI Chid Benz afariki

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
HEADLINES RIP 😭 KING KONG

Rapa na mSanii mkongwe wa Hiphop apa nchini Chidd Benz amefariki dunia mapema jioni ya Leo kwenye hospital ya rufaa ya Muhimbiri .. Kwa ugonjwa wa Kansa ya Koo.
Vyombo mbalimbali vya habali ikiwemo WASAFI Media wamedhibitisha na kulipoti taarifa hii..

RIP Chidd Benz tutakukumbuka Kwa nyimbo zako Kali na kuzienzi .💔💔🙏😭

Dotcome Dotcome.

SIKWELICHID6JUN25.jpg
 
Tunachokijua
Madai

Juni 4, 2025 baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walisambaza grafiki yenye utambulisho wa Wasafi radio/TV ikiwa na ujumbe unaosomeka “CHID BENZ AFARIKI DUNIA”. Taarifa hiyo imefifadhiwa hapa na hapa

Uhalisia wa taarifa hiyo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli na haijachapishwa wala kutolewa na Wasafi News. Aidha hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo.

JamiiCheck imebaini kumekuwa na machapisho ya mara kwa mara yanayosambazwa na watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii kuueleza kuwa Chid amefariki bila kuwa na uthibitisho wa kutosha kuhusu madai hayo. Mfano Mei 19, 2025 taarifa hiyo ilisambazwa pia

Kituo cha Bogo FM kilichapisha kipande cha video April 14, 2025 wakihoji ni wapi alipo Chid Benz, Je anaumwa? Taarifa hiyo ilieleza kuwa Chid yupo kwenye nyumba za matibabu ya kuachana na uraibu wa dawa za kulevya ambapo anaendelea na matibabu ambapo amepelekwa na baraza la sanaa Tanzania.

Mara baada ya taarifa hizo JamiiCheck imefuatilia na kubaini hakuna taarifa nyingine zinazoelezea Chdi Benz kuumwa Kansa ya koo wala kifo chake ambayo imechapishwa katika vyanzo vya kuaminika ikiwemo wasanii wenzake.
Duh aisee kama ni kweli pole yetu site.noma sana
 
HEADLINES RIP 😭 KING KONG

Rapa na mSanii mkongwe wa Hiphop apa nchini Chidd Benz amefariki dunia mapema jioni ya Leo kwenye hospital ya rufaa ya Muhimbiri .. Kwa ugonjwa wa Kansa ya Koo.
Vyombo mbalimbali vya habali ikiwemo WASAFI Media wamedhibitisha na kulipoti taarifa hii..

RIP Chidd Benz tutakukumbuka Kwa nyimbo zako Kali na kuzienzi .💔💔🙏😭

Dotcome Dotcome.

Duh hilo jina la Hospital imenibidi nicheke tu.. japo habari inasikitisha... Mleta news ni Mtu wa Musoma? Mura !
 
Watoto wa Ilala magorofani tungejua kitambo kama ni kweli.....
 
Chid hapa ndiyo turning point ya utajiri ki maakama .wafungulie kesi upige B zako 2
 
Free tundu Lissu.
No reform No election.
No reform No election.
No reform No election.
 
Back
Top Bottom