Chenge, Dkt. Kijaji ‘wapambana’ na Mnyika matumizi ya Tsh. Bilioni 976

“Hebu nisaidie sheria ya bajeti kuhusu kuhamisha fedha inasemaje, ni Bunge linafanya au mamlaka husika.”
Sasa kama hivyo ndivyo, bunge lipo kufanya nini? Yaani bunge lipitishe matumizi, halafu kumbe kuna sheria pembeni inayoruhusu kupangua matumizi yalivyopitishwa na Bunge?
Mbona hili halieleweki?
Hiyo sheria inasemaje, labda inaweza kufafanua ni kwa sababu zipi na kiasi gani kinachoweza kuhamishwa. Vinginevyo, Bunge litakuwa linafanya kazi hewa.
 
kwanini Mh.Chenge hamlazimishi Naibu Waziri kueleza ts 980++ million zimetumika wapi, badala yake anambana mbunge anayehoji kwenye masuala ya kanuni?
hii haikuwa hoja bali Mnyika alikuwa anataka kuleta uswahili bila kufuata kanuni za Bunge na sheria ya nchi (Bajeti). Mnyika angekuwa na hoja iwapo matumizi ya bilioni hizo yangekuwa yamekiuka sheria. Kwa hiyo, Mnyika alikuwa anajibaragua tu ili apate fursa/upenyo wa kutaja madai yao ya kijinga ya 1.5/-t. Anayetaka kujua mchanganuo wa matumizi ya kiasi hicho cha fedha basi asubiri riporti ijayo ya CAG. .
 
Hizo ndio hizo pesa zinazogaiwa kama njugu majiani.hazina maelezo hizo chenge na bunge linamzonga tu Huyo mnyika lakini ukweli wanaujuwa.
 
Watahangaika sana kupata pa kutokea. Jambo moja lililo wazi kabisa, bunge letu ni dhaifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…