Chenge, Dkt. Kijaji ‘wapambana’ na Mnyika matumizi ya Tsh. Bilioni 976

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,172
5,906
Leo Mh. Mnyika amebanwa na Mwenyekiti wa Bunge aeleze kama hakuhusika na hajui kwamba ipo sheria ya bajeti/fedha inayotoa ruhusa na ukomo wa mamlaka kuhamisha fedha bila kuhitaji kibali cha Bunge? akataka kupotezea kuwa asingependa kuendelea na suala hilo kwa sababu linampotezea mda!

----------
Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amelazimika kuomba kumbukumbu rasmi za bunge (Hansard) ili kufuatilia na kutoa majibu ya hoja ya Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika aliyeitaka ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kueleza matumizi ya Sh976.96 bilioni.

Amechukua uamuzi huo leo kutokana na mbunge huyo kuibua sakata hilo huko akikumbushia sintofahamu ya matumizi ya Sh1.5 trilioni yaliyoibuliwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad katika ripoti ya ukaguzi ya mwaka 2016/17.

Mbunge wa Kibamba, John Mnyika akichangia
Mbunge wa Kibamba, John Mnyika akichangia bungeni mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais (Tamisemi) na Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha 2019/2020, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Mnyika alikuwa akijadili bajeti ya Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Utata wa matumizi ya Sh1.5 trilioni uliibuliwa na Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe wakati akichambua ripoti ya CAG.

Tangu suala hilo lilipoibuliwa Aprili mwaka jana kumekuwa na mijadala mara kadhaa ndani na nje ya Bunge hasa kutoka kwa upinzani uliokuwa ukitaka maelezo ya kuwapo kwa tofauti ya uwiano wa mapato na matumizi ya kiasi hicho cha fedha ambacho Zitto alidai hakionekani jinsi kilivyotumika katika ripoti ya CAG.

“Nitaomba kupata ufafanuzi kutoka ofisi ya Rais, ripoti iliyopita ya CAG iliibua madudu mengi katika sekta na wizara mbalimbali na kati ya mambo yaliyoibuliwa ni pamoja na Sh1.5 trilioni na kupanda hadi 2.4 trilioni.”

“Katika ufafanuzi wa Serikali kuna taarifa zilitolewa kwamba Sh976.96 bilioni zilihamishwa kwenye mafungu mbalimbali zikapelekwa kwenye fungu la 20 la bajeti ambalo ni sehemu ya hotuba yetu ya leo ya ofisi ya Rais Ikulu.”

“Kama mbunge naamini Bunge halikupitisha uamuzi wa kuhamisha fedha hizo kupeleka Ikulu,” amesema Mnyika.

Baada ya kauli hiyo, Chenge aliingilia kati, “Hebu nisaidie sheria ya bajeti kuhusu kuhamisha fedha inasemaje, ni Bunge linafanya au mamlaka husika.”

Katika majibu yake Mnyika amesema: “Kwa ajili ya muda naomba nijikite katika hoja yangu tukitaka kulijadili hilo tutachukua muda.”

Chenge alizidi kumbana Mnyika akimtaka kutojumuisha mambo ambayo hawezi kuyatolea majibu.

“Sisi wote tumeshiriki katika utungaji wa sheria hiyo (ya bajeti), kiwango kilichotajwa na sheria ya bajet kama kuna mbunge anatakiwa kupinga hilo, uhamishaji wa fedha ukiwekwa na Serikali hapa wewe (mbunge) unatakiwa useme uhamishaji huo unazidi kiwango kilichowekwa na Bunge (ukomo) lakini hatuwezi kufanya majumuisho tu,” amesema.

Alipotakiwa kujibu Mnyika amesema, “Ili tuondoe utata kuhusu jambo hili la Sh Sh976.96 bilioni, kwa kuwa CAG anabanwa kukagua Ikulu ofisi ya Rais wakiwa wanajibu (hoja za wabunge) watueleze hizi fedha zimetumikaje?"

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji akiomba muongozo wa Mwenyekiti Wabunge alipokuwa akitaka Mbunge wa Kibamba, John Mnyika afute baadhi ya kauli zake alizozitoa wakati akichangia bungeni mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais (Tamisemi) na Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha 2019/2020, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Naibu Waziri wa Fedha, Dk Ashantu Kijaji naye alitolea ufafanuzi hoja ya Mnyika akibainisha kuwa ni lazima suala hilo lijibiwe leo na si siku ambayo mawaziri kwa pamoja watajibu hoja zote za wawakilishi hao wa wananchi walizozitoa wakati wakichangia bajeti hiyo.

“Mnyika athibitishe kwamba CAG anabanwa kukagua fungu 20 la ofisi ya Rais kwa sababu kinachofahamika kila fungu lina resident auditor kutoka ofisi ya CAG likiwamo fungu 20.”

“Hakuna fungu hata moja ambalo CAG anazuiwa kukagua na fungu hili lilikaguliwa, hoja zake (Mnyika) anawadanganya Watanzania, anamchafua Rais bila sababu za msingi,” amesema Dk Kijaji.

Alipotakiwa kuendelea kuchangia Mnyika amesisitiza, “Naomba katika majumuisho ofisi ya Rais ilete mchanganuo hizi fedha zimetumika kwenye kitu gani.”

Mbunge wa Uranga (CCM), Goodluck Mlinga (CCM) aliomba kuhusu utaratibu akitumia kanunia ya 64 (a) ya Bunge.

“Suala la Sh1.5trilioni limeendelea kuzungumzwa bungeni kwa uongo, ripoti ya PAC (Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali) ambayo mwenyekiti wake ni mpinzani (Naghenjwa Kaboyoka) wa Chadema katika ukurasa wa 35 inasema kuwa tofauti ya Sh1.5trilioni haikuwapo baada ya mahesabu kurekebishwa.”

“ Ila hili suala limeendelea kuzungumzwa na Bunge linakaa kimya, suala hili likemewe na (Chenge) utoe maelekezo.”

Katika ufafanuzi wake Chenge amesema: “Kwa mujibu wa kanuni zetu kwa sababu ya uamuzi wa kamati ya PAC kwa hayo uliyoyasema unatakiwa kuthibitisha ni kweli au si kweli, kwanza kufuta kauli yako kuhusu Sh2.4 trilioni kwa maana kwamba 1.5 trilioni kujumlisha hizi bilioni.”

“Maelezo ya Sh1.5 trilioni yapo katika ripoti ya CAG, sasa futa kauli yako au uthibitishe hapa bungeni, nikupe muda uthibitishe, chagua moja,” amesema Chenge.

Mnyika amesema, “Naomba kuweka rekodi sawa, nimesema nataka maelezo ya Serikali bungeni juu ya Sh 976.96 bilioni zimetumika kwa matumizi gani na hii ndio inasababisha mjadala wa Sh 1.5trilioni na Sh 2.4trilioni kuendelea. Kama ni uthibitisho basi ni Sh 976.96 bilioni za fungu 20 za Ikulu.”

Kutokana na Mnyika kuendelea kushikilia hoja yake, Chenge alisema mbunge huyo ni kama anawapotezea muda na kuagiza kupata taarifa za kumbukumbu za Bunge ili kufuatilia vyema hoja yake na kutoa uamuzi leo saa 7:00 mchana kabla ya kuahirishwa kikao hadi saa 11:00 jioni.

Hata hivyo, ilipofika muda huo Chenge aliahirisha kikao hicho bila kutoa ufafanuzi wa hoja hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
Unamshukuru chenge kwa lipi?.au wewe ni mmja wa hayawani,watu wengine mnakera sana nakuombea upigwe kibao gizani leo.
Chenge alizidi kumbana Mnyika akimtaka kutojumuisha mambo ambayo hawezi kuyatolea majibu.
 
Sasa kama swali lilikuwa linampotezea muda na yeye ana mambo mengi ya kujadili kwanini asilipptezee.

Sent using Jamii Forums mobile app
“Kama mbunge naamini Bunge halikupitisha uamuzi wa kuhamisha fedha hizo kupeleka Ikulu,” amesema Mnyika.

Baada ya kauli hiyo, Chenge aliingilia kati, “Hebu nisaidie sheria ya bajeti kuhusu kuhamisha fedha inasemaje, ni Bunge linafanya au mamlaka husika.”

Katika majibu yake Mnyika amesema: “Kwa ajili ya muda naomba nijikite katika hoja yangu tukitaka kulijadili hilo tutachukua muda.”
 
Mungu mbariki Mnyika
“Kama mbunge naamini Bunge halikupitisha uamuzi wa kuhamisha fedha hizo kupeleka Ikulu,” amesema Mnyika.

Baada ya kauli hiyo, Chenge aliingilia kati, “Hebu nisaidie sheria ya bajeti kuhusu kuhamisha fedha inasemaje, ni Bunge linafanya au mamlaka husika.”

Katika majibu yake Mnyika amesema: “Kwa ajili ya muda naomba nijikite katika hoja yangu tukitaka kulijadili hilo tutachukua muda.”
 
Leo Mh. Mnyika amebanwa na Mwenyekiti wa Bunge aeleze kama hakuhusika na hajui kwamba ipo sheria ya bajeti/fedha inayotoa ruhusa na ukomo wa mamlaka kuhamisha fedha bila kuhitaji kibali cha Bunge? akataka kupotezea kuwa asingependa kuendelea na suala hilo kwa sababu linampotezea mda!

----------
Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amelazimika kuomba kumbukumbu rasmi za bunge (Hansard) ili kufuatilia na kutoa majibu ya hoja ya Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika aliyeitaka ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kueleza matumizi ya Sh976.96 bilioni.

Mbunge wa Kibamba, John Mnyika akichangia bungeni mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais (Tamisemi) na Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha 2019/2020, jijini Dodoma leo.

“Katika ufafanuzi wa Serikali kuna taarifa zilitolewa kwamba Sh976.96 bilioni zilihamishwa kwenye mafungu mbalimbali zikapelekwa kwenye fungu la 20 la bajeti ambalo ni sehemu ya hotuba yetu ya leo ya ofisi ya Rais Ikulu.”

“Kama mbunge naamini Bunge halikupitisha uamuzi wa kuhamisha fedha hizo kupeleka Ikulu,” amesema Mnyika.

Baada ya kauli hiyo, Chenge aliingilia kati, “Hebu nisaidie sheria ya bajeti kuhusu kuhamisha fedha inasemaje, ni Bunge linafanya au mamlaka husika.”

Katika majibu yake Mnyika amesema: “Kwa ajili ya muda naomba nijikite katika hoja yangu tukitaka kulijadili hilo tutachukua muda.”

Chenge alizidi kumbana Mnyika akimtaka kutojumuisha mambo ambayo hawezi kuyatolea majibu.

“Sisi wote tumeshiriki katika utungaji wa sheria hiyo (ya bajeti), kiwango kilichotajwa na sheria ya bajet kama kuna mbunge anatakiwa kupinga hilo, uhamishaji wa fedha ukiwekwa na Serikali hapa wewe (mbunge) unatakiwa useme uhamishaji huo unazidi kiwango kilichowekwa na Bunge (ukomo) lakini hatuwezi kufanya majumuisho tu,” amesema.

Alipotakiwa kujibu Mnyika amesema, “Ili tuondoe utata kuhusu jambo hili la Sh Sh976.96 bilioni, kwa kuwa CAG anabanwa kukagua Ikulu ofisi ya Rais wakiwa wanajibu (hoja za wabunge) watueleze hizi fedha zimetumikaje?"

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji akiomba muongozo wa Mwenyekiti Wabunge alipokuwa akitaka Mbunge wa Kibamba, John Mnyika afute baadhi ya kauli zake alizozitoa wakati akichangia bungeni mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Rais (Tamisemi) na Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) kwa mwaka wa fedha 2019/2020, jijini Dodoma Leo.

Naibu Waziri wa Fedha, Dk Ashantu Kijaji naye alitolea ufafanuzi hoja ya Mnyika akibainisha kuwa ni lazima suala hilo lijibiwe leo na si siku ambayo mawaziri kwa pamoja watajibu hoja zote za wawakilishi hao wa wananchi walizozitoa wakati wakichangia bajeti hiyo.

“Mnyika athibitishe kwamba CAG anabanwa kukagua fungu 20 la ofisi ya Rais kwa sababu kinachofahamika kila fungu lina resident auditor kutoka ofisi ya CAG likiwamo fungu 20.”

“Hakuna fungu hata moja ambalo CAG anazuiwa kukagua na fungu hili lilikaguliwa, hoja zake (Mnyika) anawadanganya Watanzania, anamchafua Rais bila sababu za msingi,” amesema Dk Kijaji.

Alipotakiwa kuendelea kuchangia Mnyika amesisitiza, “Naomba katika majumuisho ofisi ya Rais ilete mchanganuo hizi fedha zimetumika kwenye kitu gani.”

“Suala la Sh1.5trilioni limeendelea kuzungumzwa bungeni kwa uongo, ripoti ya PAC (Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali) ambayo mwenyekiti wake ni mpinzani (Naghenjwa Kaboyoka) wa Chadema katika ukurasa wa 35 inasema kuwa tofauti ya Sh1.5trilioni haikuwapo baada ya mahesabu kurekebishwa.”

“ Ila hili suala limeendelea kuzungumzwa na Bunge linakaa kimya, suala hili likemewe na (Chenge) utoe maelekezo.”

Katika ufafanuzi wake Chenge amesema: “Kwa mujibu wa kanuni zetu kwa sababu ya uamuzi wa kamati ya PAC kwa hayo uliyoyasema unatakiwa kuthibitisha ni kweli au si kweli, kwanza kufuta kauli yako kuhusu Sh2.4 trilioni kwa maana kwamba 1.5 trilioni kujumlisha hizi bilioni.”

“Maelezo ya Sh1.5 trilioni yapo katika ripoti ya CAG, sasa futa kauli yako au uthibitishe hapa bungeni, nikupe muda uthibitishe, chagua moja,” amesema Chenge.

Mnyika amesema, “Naomba kuweka rekodi sawa, nimesema nataka maelezo ya Serikali bungeni juu ya Sh 976.96 bilioni zimetumika kwa matumizi gani na hii ndio inasababisha mjadala wa Sh 1.5trilioni na Sh 2.4trilioni kuendelea. Kama ni uthibitisho basi ni Sh 976.96 bilioni za fungu 20 za Ikulu.”

Kutokana na Mnyika kuendelea kushikilia hoja yake, Chenge alisema mbunge huyo ni kama anawapotezea muda na kuagiza kupata taarifa za kumbukumbu za Bunge ili kufuatilia vyema hoja yake na kutoa uamuzi leo saa 7:00 mchana kabla ya kuahirishwa kikao hadi saa 11:00 jioni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabunge wazalendo...CHADEMA, Mnyika, Zitto, Halima Mdee, Ester Matiko, Ester Bulaya

Wanajeshi au Mapolisi wametoka kwa wananchi...wana Dada zao, Kaka zao, Baba Zao, shangazi zao, wajomba zao, mama mkwe, baba mkwe, shemeji etc

Upofu wa watawala ndio hujidanganya kuwa unaweza kutumia Polisi kupiga shangazi zao, au kipigo cha mbwa koko, au kupigwa hadi kuchakaa..au kulazimisha gesi itoke mtwara JWTZ - Ni vitendo vya muda mfupi tuu

Iko siku polisi/mwanajeshi atasikia ndugu yake au mama yake kanyanyaswa na Jeshi au polisi....eee maeneo fulani na yeye yko mkoa fulani, nae anapewa amri apige, ua....Formula itagoma.

Maandamano yanayogusa Taifa zima, maana yake jamii nzima inaguswa..hata ndugu za wanajeshi/Polisi watamwagiwa maji ya kuwasha...Je wataendelea kutii?

Kinachoshindikana Tanzania ni kuwa maandamano yanakuwa ni ya mkoa mmoja tu, au mji mmoja...na Wananchi kukosa elimu/muamko wa kujua sababu ya maandamano...Kwa Tanzania bado, hasa itokee Uchumi mbaya....

Watch out..Uchumi wa tanzania umeshuka hadi % we not far from there...
 
Ila hayajawahi kufanyika MKOANI KILIMANJARO NA MJINI MOSHI- YAKIANZIA MKOANI KILIMANJARO NA MJINI MOSH YATAFANIKIWA TU
 
thetallest ,

..hoja yako ingekuwa na maana kama Mh.Chenge angekuwa siyo mwana-ccm na hafanyi kazi ya kuilinda na kuitetea serekali ya ccm.

..kwanini Mh.Chenge hamlazimishi Naibu Waziri kueleza ts 980++ million zimetumika wapi, badala yake anambana mbunge anayehoji kwenye masuala ya kanuni?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom