TANZANNIA
JF-Expert Member
- Sep 29, 2015
- 1,047
- 384
mama mmoja mlemavu wa mguu kaja jijini kumtembelea bintiye ambaye ni mkurugenzi wa kampuni fulani,binti hakufurahishwa na ujio wa mamaye kwani kwa hadhi aliyonayo aliona kama fedheha kuwa na mama kama yule kiasi cha kushindwa kumtambulisha kwa rafiki zake.siku moja akamwambia'mama,taja gharama zako zote ulizotumia kunilea nikulipe ili usiwe mama yangu'mama kwa uchungu akajibu sawa ila nitakutajia kesho asubuhi,
usiku wakati wa kulala yule mama akawa akiumwa haja iwe kubwa au ndogo anajisaidia kitandani na kujipaka mwilini,kulipokucha bintiye akaja chumbani kwa mama ili kuchukua jibu lake na kumkuta mama amepakaa kinyesi na mkojo mwili mzima.bint akamuuliza mama kwa hasira,ndio tabia gani hii uliofanya?mama akajibu kwa upole'haya ndio malipo ninayotaka unilipe, unisafishe kama mimi nilivyokuwa nikikusafisha wewe,na hii si leo tu,nitafanya hivi kila siku kwa miaka mitano.binti akalia na kumwomba msamaha mama yake