Check milestone za maisha, uko wapi kwa sasa na umetimiza kulingana na umri ulionao?

Boloyoung

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
682
652
20 - 25 = iwe kama ni kielimu hujafikia malengo yako, sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya, pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.

25 - 30 = Hakikisha uwe na angalau SHUGHULI RASMI kama umeajiriwa au umejiajiri kama Medical rep supervisor au shughuli nyingine ya kukuingizia kipato.

30 - 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja, tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa kama sio kuishi nae, tena si mbaya ukawa umeshatengeneza familia, kwa maana ya kuwa na watoto kama Mungu kakuwezesha.

35 - 40 = ni umri wa kama kiwanja kiwe kimejengwa na kama ni tayari basi nenda step nyingine ya kumiliki kama ni Gari au kuongeza nyumba na hakikisha vinaenda sambamba na ongezeko la familia. Hapa inabidi upambane sana kuweka misingi.

40 - 45 = Ni umri wa masahihisho, kama hukuwahi kununua kiwanja, kama hukujenga basi hapa pambana afe kipa afe beki, ni umri wa masahihisho. Ila kwa wale ambao wameenda vizuri huko nyuma basi hapa watoto wapo kwenye level tofauti za elimu, kwahiyo ni muda wa kuwawekea malengo ya kimasomo watoto wao.

45 - 50 = Kwa yule ambae hakukosea huko nyuma basi umri huu ni wa kuanza kuwatengenezea mazingira watoto wako, kama ni shughuli zako ni kuanza kuwahusisha, huku wewe ukijiweka pembeni taratibu na kuangalia fursa za umri wako. Lakini kwa wale waliokosea hapa ni kupitia zile hatua za 35 - 40.

50 - 60 = Ni kujiandaa na maisha mapya ya kustaafu au kujiweka mbali na shughuli za shulba na kama ulijitenga na msikiti/kanisa huu ndo muda wako.

60 - 70 = Kula matunda yako huku ukiangalia misingi ya wanao inaendaje.

70 - 80 = Kula matunda

80 - nk = Unamsikilizia Mungu anasemaje.

07ecac61ba8e3f4e8e77c43890198638.jpg
 
Mkuu ujui kiasi gani Uzi wako umenitia nguvu kubwa ya kuendelea kuboresha maisha yangu nipo kwenye 30 huku mwanZon mwanzon lakini kuanzia Leo nazidisha juhud kama Niko 40-45 natumia huo mfumo wa afe kipa afe beki,Big up mkuu kwa Uzi huu murua
 
Daah!Huu mpangilio ni mzuri sana na kinachonifurahisha na kunipa moyo ni kwamba mambo yangu yanaenda kama ulivyoainisha hapo juu.Asante sana maana nimegundua kwamba nina future nzuri coz maisha yangu yanaenda kwampangilio maalum na kwamda sahihi
 
Hahah naona wengine tuko 20s lakini tunafanya mambo 40s hili linaubaya mkuu?
Kuna ubaya tena mkubwa sana. ...

ukifika 50 au 60's basi jiandae kufanya mambo ya 20's ikiwamo kugongagonga au kugongwagongwa na vitoto vidogo....kuhangaika na madisco na ma nightclubs....

na tutakuita mtu mzima hovyoooooo.

in every action there is equal and opposite reaction....

ukikopa lazima utalipa tuu.
 
Kuna ubaya tena mkubwa sana. ...

ukifika 50 au 60's basi jiandae kufanya mambo ya 20's ikiwamo kugongagonga au kugongwagongwa na vitoto vidogo....kuhangaika na madisco na ma nightclubs....

na tutakuita mtu mzima hovyoooooo.

in every action there is equal and opposite reaction....

ukikopa lazima utalipa tuu.
Wat if anafanya mambo ya 40s na still bata anakula vyema kabisa? life has no fomula son!
 
OK am 25-30yrs nina kiwanja, cjapata shughuli maalum kwa sababu ya sirikali kuleta milegezo kwenye ajira, mkuu niko kwenye point of best winner au ndo best loser
Acha uoga ...life haina formulae...just muombe mungu atleast ukiwa kwenye umri huo tajwa hayo uwe ushayafanya.

tunaongeleaje kuhusu babu wa loliondo...kids milionea kwenye umri as miaka 70.

tunaongeleaje mabilionea kama Mark zuckerber wa Facebook kuwa bilionea kabla hajaoa na umri chini ya miaka 20.
 
Ha ha haleta uzi bhana una visa kwel,,mbona hutuambii umri ni nini?? Mbona kama hujatutendea haki watu wasiojua nini maana ya muda? Mbona umesahau kwa yyte mwenye mwili na pumzi anaweza kuset mambo yake bila kigezo hata kimona hapo,,ila nmeipenda sana japo sijapitia hata moja
 
Wat if anafanya mambo ya 40s na still bata anakula vyema kabisa? life has no fomula son!
NDIO nasema pia hayo yaliyoandikwa sio lazima yawe kama yalivyopangwa na pia society zinatofautiana....anaongelea miaka 70 na 80 wakati kitaaluma life Span ya mtanzania ni miaka 58 sijui....baada ya hapo UNATAKIWA UWE ushakufa.

hii post ya mdau inaweza kuwatia watu uchizi au kuwafanya watu waone wapo mbali sana kimaisha wakati maisha ni mapambano ya kila siku na refarii mkuu ni MUNGU
 
Yani
Kuna ubaya tena mkubwa sana. ...

ukifika 50 au 60's basi jiandae kufanya mambo ya 20's ikiwamo kugongagonga au kugongwagongwa na vitoto vidogo....kuhangaika na madisco na ma nightclubs....

na tutakuita mtu mzima hovyoooooo.

in every action there is equal and opposite reaction....

ukikopa lazima utalipa tuu.
Yani utakuwa anafanya mambo kama anayoyafanya mzee wa mishati mikubwa kubwa tofauti na umri wake
 
Boloyoung

Sijaona mahali popote ulipoweka msisitizo watu wamtafute Mungu.. nafikiri unadhani kufanikiwa kimaisha ni kuwa na kiwanja/nyumba au gari.. au kuoa na kuolewa..

Nafikiri ndio maana hatuendelei.. malengo yetu mengi ni kuwa na material possessions.. ndio maana umemuweka Mungu mwisho wa maisha (miaka 80) wakati yeye kasema tumtafute wakati wa ujana tukiwa na nguvu za kumtumikia..

Ikiwa nina miaka 20 na nina vyote hivyo je unanishaurije?? Umesahau kuwa formula ya maisha haipo universal.. kuna watakaofanikiwa mapema wengine watachelewa..

Ume assume kuwa kila mtu atafika miaka 80.. ila ukweli kwa thinking capacity uliyoionyesha kufika miaka 80 itakuwa ngumu sana..

Adiós..
 
Acha uoga ...life haina formulae...just muombe mungu atleast ukiwa kwenye umri huo tajwa hayo uwe ushayafanya.

tunaongeleaje kuhusu babu wa loliondo...kids milionea kwenye umri as miaka 70.

tunaongeleaje mabilionea kama Mark zuckerber wa Facebook kuwa bilionea kabla hajaoa na umri chini ya miaka 20.
No one know tomorrow, ila mkuu kaongea vizuri sana kuna mijitu leo inakimbilia 40s lakini bado wanaishi kwa wazazi na wala hawajali lazima uwe una stepup kadri umri unavyokwenda
 
Mi ndio naingia 30 now nimepanga mwaka huu niwe na ajira ya kudumu, nipange chumba na nioe haya yote nataka niyafanye kabra sijaingia 31 naona km nimechelewa yaani lakini ndio nilikua nayasoma maisha.
NAAMINI SIKO MBALI NA UMRI WANGU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom