CHAUMMA chaumwa

daah,
hadi umeshusha na mzigo kabisa na kuamua kuwaonyesha wadau wa JF rangi ya nonsense uloitoa?
ndio kazi ulokua unaifanya wakatia wa kuandika uzi kuhusu chaumma, dah.
halafu una ujasiri wa kiwango kibaya sana gentleman, naona mshipa wa aibu ulikatika enzi za Kigaila yupo chadema right?
 
Hivi tofauti yenu na wao ni ipi
 
Hivi tofauti yenu na wao ni ipi
mnatofautiana uropokaji tu, si wote mlikua ile chadema ya utekaji kwenye kila chaguzi za ndani, kisha mkatibuana halafu wao wakaenda chaumma na nyinyi mkabaki chadema masalia,
 
mnatofautiana uropokaji tu, si wote mlikua ile chadema ya utekaji kwenye kila chaguzi za ndani, kisha mkatibuana halafu wao wakaenda chaumma na nyinyi mkabaki chadema masalia,
"Mtu mpaka nzi anatua kichwani kabisa unafikiri huo ubongo unanini zaidi ya...

Kutoka inbox😂😂😂
 
"Mtu mpaka nzi anatua kichwani kabisa unafikiri huo ubongo unanini zaidi ya...View attachment 3531267

Kutoka inbox😂😂😂
huyo nzi atakua kavutiwa kile kilichokua kwenye ile tishu uloiweka hapa jukwaani muda mfupi ulopita ndugu yangu timu Kitima & ruwaichi,

naona Lucy Miko anawachakata mioyo haswaaa
 
Waliotoka Chadema kwenda Chaumma walisema walienda kwa sababu wanataka kugombea uchaguzi. Wakagombea na sasa wana wabunge watatu na ruzuku ya kuendesha chama chao. Kabla ya hapo hawakuwa na mbunge wala ruzuku. Hatujasikia wakigombana au chama chao kuvunjika bali tunawaona wabunge wao wakitimiza wajibu wao. Waacheni wajipange upya na wafanye siasa kwa namna wanavyotaka. Wengine endeleeni na vyama vyenu, achaneni na Chaumma.

Amandla..
 
sasa ina maana Mrema siku hizi ndio hapati ile RUZUKU iliyomfanya ageuke MSALITI wa Wanamageuzi?
 
"Mtu mpaka nzi anatua kichwani kabisa unafikiri huo ubongo unanini zaidi ya...

Kutoka inbox😂😂😂
Hivi Msigwa (mchungaji) bado yuko CCM? Siku hizi kapoa sana. Bado nakumbuka ile picha yake akiwa amebebeshwa picha ya Samia kama watoto enzi hizo za zamani walipokuwa wanabeba picha za wanandoa wakati wa harusi.
 
Hivi Msigwa (mchungaji) bado yuko CCM? Siku hizi kapoa sana. Bado nakumbuka ile picha yake akiwa amebebeshwa picha ya Samia kama watoto enzi hizo za zamani walipokuwa wanabeba picha za wanandoa wakati wa harusi.
Alisema atazunguka nchi nzima kuyaanika mabaya ya CHADEMA😂
 
Mwenye kuuza cheni feki kapewa hela bandia. Ngoma droo wote wanataabika.
 
Anaandika Martin Maranja Masese

Wanaharakati hawajatufikisha hapa. Tumefika hapa kwa kuwa kikundi kidogo cha watu kiliamua kufanya siasa za UDALALI na kutumika na MaCCM – wakahamia CHAUMMA kwa kupewa ahadi za uongo za madiwani, wabunge na halmashauri. Hizo ni siasa za UDALALI.

CHADEMA sasa inashtakiwa na wahuni ambao wamewahi kuwa viongozi waandamizi. Maombi ya wahuni ndiyo yametumiwa na Mahakama kuzuia shughuli za CDM. Hao ndiyo wanatumika na MaCCM kutaka kupoteza tunu ya wananchi, CHADEMA.

Kama kweli ungelikuwa unampenda Tundu Lissu kuliko hao wanaharakati, usingemkimbia wakati anachagiza ‘No Reforms, No Election’ kwa wananchi ili waelewe somo. Ulikimbilia CHAUMMA, ukagombea ubunge na husemi ulipewa kura ngapi. AROBAINI?

Kama wewe na wenzako mngelikuwa mnampenda Tundu Lissu kuliko hao wanaharakati, ungejaribu kutenga muda wako hata mara moja, kwenda Mahakamani, kumsalimia na kumuunga mkono katika kesi zake. Hujawahi kufika hata kwa bahati mbaya

Wanaomshtaki Tundu Lissu ni Serikali ya CCM. Hawa ni mabosi zenu. Hao ndiyo ambao wananufaika na TAL kuendelea kuwepo gerezani kwa makosa ya uongo na ulaghai ya uhaini. Tundu Lissu anajitetea mwenyewe na ameeleza Mahakamani anashtakiwa na CCM

CHAUMMA mlishindwa kumtaja mgombea wa CCM katika utapeli wenu wa kampeni. Mmeshindwa kutoa pole baada ya mashosti zenu (CCM) kufanya mauaji ya kutisha, mkahudhuria uapisho kambi ya Jeshi – tunaelewa, huwezi kusema CCM wanamuonea TAL

Wanaharakati wanatengeneza vipi pesa kupitia Tundu Lissu kuwepo gerezani? Michango? Familia ya Tundu Lissu imetoka hadharani na kufafanua aliyefanya utapeli ni nani na wametoa taarifa polisi, amekamatwa na hadi sasa yupo mahabusu. Hakuna agenda hapo.

Katika uchaguzi ndani ya CHADEMA tulipoamua kumuunga mkono FAM, tuliamini wagombea wote ni CHADEMA na atakayeshindwa, ataponya maumivu haraka na kuendelea na harakati. Imekuwa kinyume chake. MADALALI mmekuwa zaidi ya KIBAJAJI na NAPE

Mnafanya kazi ambayo MaCCM wamekuwa wakiifanya wakati wote, kushambulia CHADEMA na viongozi wake. Hii inatia mashaka kama mlikuwa wapinzani kweli wa MaCCM au mlikuwa marafiki wa maCCM katika rangi za CHADEMA. Ni kushindwa uchaguzi tu?

Mzee Freeman Mbowe akiwa gerezani kwa makosa ya uongo ya ugaidi, tulitenga muda, tukahudhuria na kuripoti kesi kwa miezi nane mfululizo. Tuliamini FAM siyo GAIDI. Alipotoka, alikwenda moja kwa moja IKULU. Alitukwaza. Lakini tuliamua kumuelewa.

Unafikiri hayapo ambayo mzee FAM alitukwaza? Yapo, lakini tuliamua kumuelewa kama kiongozi. Mfano, maridhiano tuliyapinga. Hata kumleta Mwenyekiti wa CCM katika mkutano wa BAWACHA siku ya wanawake Duniani, haikuwa sawa. Lakini tulimuelewa.

Kama ambavyo tulisimama kidete na kulinda jina la CHADEMA na viongozi wake wakati Mzee Freeman Mbowe, akiwa kiongozi wetu, ndivyo tutasimama, kutetea taswira ya CHADEMA na kuwalinda viongozi. CHADEMA ni UHURU na MABADILIKO ya KWELI

Mnamchoresha sana Mzee MBOWE, sana. #TunduLissuSioMhaini #JusticeForTAL ✊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…