Mwenyekiti wa CHASO (CHADEMA Student Organization) mkoa wa Dar es Salaam Martin Samson Abduli ametoa tamko kwa waandishi wa habari akilalamikia mwenendo wa Rais wa TAHILISO Geofrey Kiliba akidai kuwa unakiuka misingi ya Katiba ya umoja huo wa wanafunzi wa vyuo na vyio vikuu nchini
Akizungumza jijini Dar es Salaam Abduli amesema kuwa Rais wa TAHILISO anatakiwa kutumia majukwaa yake kuzungumzia changamoto zinazowakabili wanafunzi badala ya kujihusisha na siasa za upande wowote au vyama, jambo ambalo linaenda kinyume na Katiba ya umoja huo
"Wanafunzi wanapitia changamoto nyingi kwenye masomo na maisha ya kila siku, hizo ndizo angekuwa anazizungumza badala ya mambo ya kisiasa" -Abduli
Aidha, Abduli amebainisha kuwa tayari mchakato umeanza wa kufungua kesi ya Kikatiba Mahakamani dhidi ya Rais huyo wa TAHILISO, huku akitoa wito kwa wanafunzi kote nchini kuunga mkono jitihada hizo
Soma pia GE2025 - Katibu Mkuu, TAHLISO: Malalamiko ya ukiukwaji wa Maadili ya Uongozi na Katiba dhidi ya Rais Geofrey Kiliba kwa upendeleo wa Kisiasa
Chanzo: Jambo TV