Charles Taylor kikaangoni?

Hukumu ya kwanza ya aina yake kumkabili Rais wa nchi katika bara la Afrika itatolewa leo majira ya sita kamili mchana kwa saa za Afrika Mashariki katika mahakama maalumu ya Sierra Leone mjini the Hague.

Charles Taylor anakabiliwa na mashtaka kumi na moja, na leo Majaji wanatarajiwa kutoa uamuzi iwapo Charles Taylor amepatikana na makosa mangapi ama hapana na baada ya mwezi mmoja hukumu kamili itatolewa ambapo itajulikana kama mzee mzima atatumikia kifungo ama la.

kwa takribani wiki kadhaa sasa Mjini Freetown, hususa ni katika Mahakama maalumu ya Sierra Leone kumekuwa na pilikapilika za maandalizi kuhusiana na hukumu hii. kunatarajiwa wageni wapatao elfu moja kutoka hapa nchini na Liberia watahudhuria/kushuhudia tukio hili moja kwa moja kutoka the Hague ambapo sehemu mbalimbali ndani ya eneo la mahakama zimeandaliwa kuhakikisha watu wanashuhudia tukio hili la kihistoria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…