CHAPTER ONE: Ewe Mwanadamu amka.! Acha Kushupaza Shingo,Mungu yupo,na Siku ya hukumu ipo.!

Heart Wood.

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
972
1,150
EWE MWANADAMU AMKA ! ACHA KUSHUPAZA SHINGO, MUNGU YUPO , NA SIKU YA HUKUMU IPO.!

UTANGULIZI: UWEPO WA MUNGU.!
Hatma ya Mwanadamu imefanywa kuwa siri kubwa, isipo kuwa kwa wachache wenye Imani juu ya Uwepo wa Mungu. Wenye kumjua na kumwamini Mungu tunaifahamu hatma ya Maisha yetu, tunafahamu kwa nini tupo Duniani, tunafahamu chanzo cha Ulimwengu na tunakoelekea. Tunafahamu na kuamii kuwa Maisha ya hapa Duniani si mwisho wa Masha halisi ya Mwanadamu,bali kuna Maisha mengine katika ulimwengu wa Roho yataendelea. Tunaamini kuwa katika maisha ya Ulimwengu wa Roho huko Mbinguni, watakaopata nafasi ya kushiriki Maisha hayo ni wale waliofanikiwa kuwa watiifu na kuwa Wacha Mungu hapa Duniani. Kisha wale wasiomjua na kumtii Mungu mwisho wao ni kwenye ziwa la Moto, yaani ule Moto wa Milele usiozimika.​

Kama nilivyogusia hapo mwanzo kuwa, kuna Watu wachache wasioamini habari za uwepo wa Mungu, wengi wao ni Watu waliosoma sana na kuelimika katika masuala ya Elimu ya Ulimwengu/ Dunia hii tuliyopo. Watu hao ni Wasomi wakubwa hasa katika nyanja za Sayansi na Historia. Kwakweli, watu hao wamefikia hatua ya kusema kuwa ni Mwanadamu ndiye aliyemuumba Mungu katika Fikra zake na wala hakuna Mungu aliyemuumba Mwanadamu. Ofcourse, licha ya udhihirisho wa kazi za Mungu kupitia Watumishi wake yaani Wanadamu, kwa kuwa Mungu hawezi kuonekana kwa hali ya macho yetu, bali Mungu hudhihirika kupitia kwa Wnadamu kama ilivyo tangu hapo mwanzo enzi za akina Adam, Nuhu, Ibrahimu, Isaka, yakobo, Musa, Yoshua n.k, bado watu hao hawaamini lolote katika hayo yanayofanyika. Husema kuwa hayo ni maigizo na Sayansi ya Sanaa, ambayo Mtu yeyote anaweza kuifanya. Husema kuwa yote yanayofanyika ni masuala tu ya Kisaikolojia na mauza uza ya Ulimwengu huu.

Licha ya kuwepo ushahidi mpaka sasa wa mahali ambako Biblia imetaja kuwako Wanadamu wa Awali hapo Mwanzo, mahali ambako babu zetu katika Imani mfano akina Abrahamu,Isaka na Yakobo walikuwako,kama vile baadhi ya sehemu za Mashariki ya Kati (Middle East) Yaani kama vile Yerusalemu, Jordani,Lebanon,Damascus, n.k pamoja na sehemu za Ulaya kama Greece na Italy ambako Mtume Paulo alifika kuhubiri INJILI, pamoja na sehemu mojawapo Africa yaani Misri ambako YESU alitajwa kufika wakati Yusufu na Maria walitorokea ili kuepusha kifo cha YESU na ambako wana wa Israel walikombolewa kutoka utumwani mikononi mwa Farao, lakini bado Wanadamu hawa wanaopinga uwepo wa Mungu huishia kusema sisi tunaosema Mungu yupo tulete Ushahidi wa Kisayansi kuthibitisha kama kweli Mungu yupo. Ndio maana Mungu huwaita watu hawa ni VIPOFU, wana macho lakini hawawezi kutazama.

ULIMWENGU WA ROHO.

Siku ya Leo, ntajikita katika kuelezea maana ya Ulimwengu wa Roho kwa kutumia mifano rahisi ya Kidunia. Sitatumia references nyingi za Biblia na endapo itabidii iwe hivyo, basi sitakuwa na namna nyingine kwa maaana naamini kuwa ni Roho Mtakatifu ndiye anayeniwezesha kuandika mtiririko huu wa Mawazo na ndiye atakayekuwa amekusudia iwe hivyo.

KUHUSU MAZINGAOMBWE.!

Bila shaka huko nyuma, hata sasa japokuwa mambo haya yamepungua kiasi chake maana si kama ilivyokuwa zamani, kulikuwa na hawa watu walio julikana kama Wana Mazingaombwe, Waliruhusiwa kuonesha sanaa zao hasa Mashuleni kwa kile kinachoaminika kuwa kazi zao ni sehemu moja wapo ya kuendeleza Sanaa Mashuleni. Hakika walijitahidi kutuonesha kila aina ya mambo kwa Ubunifu wao kadiri walivyojaaliwa na roho wao.

Swali la Msingi hapa la kujiuliza ni kuwa, kulikuwa na ubunifu gani katika hali ya kawaida ya Kibinadamu ilyiokuwa inapelekea mara pesa inabadilika na kuwa karatasi, mara Mtu anameza kijiti na kubadilika kuwa kalamu, mara Mtu analazwa Usingizi fofofo bila ya kujitambua ili hali dakika mbili zilizopita alikuwa katika hali ya kawaida tu. Mara soda inakuwa maji au kinyume chake, mara kokoto zinakuwa pipi n.k Hakika tulishuhudia mambo mengi tu ila hapa nimetaja kwa uchache kama mifano.

Bila kupepesa macho na kupindisha pindisha mambo, ule ulikuwa ni Ulimwengu wa Rohoni, yaani mojawapo ya Uchawi. Mimi naamini kabisa kuwa yale Mazingaombwe ilikuwa ni sehemu ya Uchawi kama uchawi mwingine wa kuruka na ungo, kuroga n.k. Ila tu ule ulitafutiwa jina zuri na kuitwa sanaa.

Sasa basi, kama utakuwa nami na kuamini kuwa mambo hayo yalitokea kwa mgongo wa sanaa, bila shaka utakubaliana nami kuwa kuna mambo mengine huweza kufanyika sirini na yasionekane katika Ulimwengu wa macho haya ya kawaida. Ndiyo,upo Ulimwengu unaitwa Ulimwengu wa Roho. Hapa Duniani/Ulimwenguni, kuna maisha ya kawaida yanayoendelea katika macho yetu haya ya kawaida na kuitwa Ulimwengu wa Mwili, hali kadhalika, kuna Masiha mengine zaidi yanaendelea katika Ulimwengu mwingine ambao hauonekani yaani ulimwengu wa Rohoni.

Katika Ulimwengu wa Mwili ndio kuna Mwanadamu, Viumbe hai wanaoonekana, Magari, Nyumba, Barabara,Mito, Maziwa, Bahari, mifumo ya Utawala ya Wanadamu, Nchi n.k. Katika Ulimwengu wa Roho, yupo Mungu na Ufalme wake, yaani Malaika, vilevile yupo Shetani na Ufalme wake ukihusisha Majini,Mapepo, Vimbwengo, Wachawi wa kila namna n.k.

Ukweli ni kwamba, japokuwa Ulimwengu wa Roho umepewa kisogo na Mwanadamu na kutokupewa kipaumbele kwa kile tu jkuwa eti ni masuala yasioonekana, hivyo kumfanya Mwanadamu kuwa busy zaidi na masula yanayoonekana katika Ulimwengu wa Mwili katika hii Dunia kwa zaidi, lakini ukweli halisi ni kwamba, Maisha katika Ulimwengu wa Roho, ndiyo maisha ya kipekee tena yenye uwezo mkubwa zaidi ya ule Ulimwengu wa Roho. Kila kinachofanyika katika Ulimwengu wa Roho kina Impact kubwa katika Ulimwengu wa Mwili. Maisha katika Ulimwengu wa Mwili kwa kiasi kikubwa au kwa utoshelevu wake yanakuwa coordinated zaidi na kuongozwa na Maisha katika Ulimwengu wa Roho. Kama hujui hili basi ni kwa sababu tu ya ufahamu wako kutokuwa well informed kuhusu Elimu hii ya Ulimwengu wa Roho kwa Utoshelevu wake.

Labda tuwaulize hawa waliosoma na kuelimika sana katika maairifa ya Maisha ya hapa Duniani na kusema kuwa hakuna Mungu. Je, hamuoni kuwa mlipokuwa wadogo mlikuwa watupu kichwani, na Elimu iliyowafanya muone hakuna Mungu ni Elimu ya Upande mmoja pekee? Je, mna kiwango gani/ mmefanya bidii gani kupata Ufahamu wa Maisha katika upande mwingine yaani Ulimwengu wa Roho ? Mbona kuna watu wengine wasomi kama ninyi lakini wanamuamini Mungu.? Ni dhahiri kuwa hata Wasomi wanapopata elimu ya Ulimwengu wa Roho, huamini kuwa Mungu yupo. Ni vigumu sana na mara chache sana kukuta Mtu aliyekwisha pata elimu kuhusu Mungu baadae apinge uwepo wa Mungu.

UCHAWI NA UGANGA.
Mfano mwinghine ulio rahisi kuweza kuyathibitisha Maisha ya Ulimwengu wa Roho ni masuala ya Uchawi na Uganga. Kwa bahati mbaya pia kuna Watu wachache husema hakuna Uchawi, lakini hili si tatizo lao wenyewe, bali ni kutokana na sababu ya Ufahamu wao kutokuwa na taarifa za kutosha kuhusu masula haya.

UTHIBITISHO;
Mara nyingi Mwanadamu hawezi kufanya kitu bila ya kuwa na ufahamu wa jambo fulani. Bila shaka umewahi kuona hata Waigizaji wa Filamu huigiza namna Shughuli za Kichawi na Waganga zinavyofanyika. Kama Uchawi na Uganga usingelikuwepo basi isingelikuwa rahisi kwa Waigizaji kubuni jambo la Kichawi na Uganga bila ya kuwa na tone la Ufahamu wa uwepo wa mambo hayo. Kuigiza kwao vile ni ushahidi mwingine juu ya uwepo wa shughuli za Kichawi na Kiganga. Kule kupandisha kwa Waganga ni Majini yanakuwa yamemuingia Mganga na kuyaruhusu kusema masuala kadha wa kadha, Kabla sijamjua Mungu sawa sawa, niliwahi kupelekwa kwa Mganga mmoja kutokana na matatizo yaliyokuwa yakinisibu, kwa kweli nilishangaa sana jinsi ambavyo Mganga yule aliweza kuzungumzia kuhusu maisha yangu na kuzungumzia mambo yaliyofanyika Nyumbani kwetu wakati sikumsimulia chochote na wala hatukuwahi kufahamiana hapo awali, Leo hii baada ya kumjua Mungu, nimebaini kuwa yale yalikuwa ni Majini katika Ulimwengu wa Roho, Majini ni sehemu ya Ufalme wa Ulimwengu wa Roho. Shetani ana uwezo wa kufahamu chochote kuhusu Mwanadamu. Mambo yote yanayo fanyika katika Uganga na Uchawi ni masula ya Ulimwengu wa Roho. Hivyo huu pia ni ushahidi kuwa kuna maisha ya Ulimwengu wa Roho.

Mifano mingine ni ile ambayo umewahi kusikia kuwa Mchawi fulani alianguka kwa kuishiwa nguvu akiwa katika harakati zake za Kichawi. Je, umewahi kusikia juu ya kupigwa marufuku kuhusu Ramli chonganishi? Ile ni kazi mojawapo ya Kiganga/ Kichawi ila imetafutiwa jina zuri na kuitwa Ramli chonganishi. Ilitakiwa tu kuitwa kazi za Kichawi. Katika Mifumo yetu ya Sheria, suala la Kichawi halitambuliki kwa kile tu kuwa hauwezi kuthibitisha juu ya uwepo wa Uchawi kwa macho. Lakini masula haya yapo. Kwa msingi huo, huo ni ushahidi mwingine wa kuthibitisha masula yanayofanyika katika Ulimwengu ule usioweza kuonekana kwa macho, yaani Ulimwengu wa Roho.

KUTOLEWA/ KUFUKUZWAKWA MAJINI/ MAPEPO KATIKA MIKUTANO YA INJILI.
Mfano mwinginme ni huu, Je, umewahi kuona Katika Mikutano ya Injili namna ambavyo mapepo hukemewa na watu kuanguka na wengine kuanza kutamka maneno yanayoashiria kupagawa? Ile ni hali ambayo hudhihirisha Ulimwengu wa Roho pia. Kwa bahati mbaya sana Watu wengine husema yale ni maigizo au kupagawa Kisaikolojia. Sasa kama ni maigizo, iweje Ulaya, Marekani, Asia, South Afrika, Nigeria na kwingineko kote Waigize na matendo yote hufanana? Yaani uigizaji au matatizo ya Kisaikolojia yafanane Duniani kote.? Ni Chuo gani au mtu gani ambaye huwafundisha watu kufanya maigizo kiasi kile Duniani kote.? Hali ile ni halisi.Hii hutokea Makanisani na kwenye Mikutano ya Injili. Mie wakati nasoma Sekondari, wakati bado nilikuwa pia nina mashaka juu ya ukweli wa jambo hili, kulikuwa na kikundi cha Maombezi cha Wanafunzi wenzetu, basi siku moja kukafanyika Maombi ya pamoja wakaalikwa Wanafunzi wenzetu kutoka Shule moja ya Wasichana, Maombi yalipoanza tu, kuna Wanafunzi wadada wakaanza kupagawa na Mapepo na kuanza kujirusha rusha na kisha kuanguka chini kisha kuombewa na Mapepo yakafukuzwa na kuwaachia. Waliokuwa wakiendesha Maombi yale walikuwa ni Wanafunzi wenzetu, ingekuiwa ni Watu nisio wajua ningeendelea kuamini kuwa ni maigizo tu yaliyopangwa kama wasemavyo Watu wengine leo hii.

UHUSIANO WA UMISIONARI ENZI ZA UKOLONI NA UENEZI WA INJILI.

Fact nyigine ambayo baadhi ya watu husema kuwa hizi Dini tulizonazo yaani Uislamu na Ukristo ni Dini za Kiarabu na Kizungu, yaani zililetwa kwa mantiki ya kututawala enzi za Ukoloni, eti zilikuja ili kutupumbaza tu ili wakoloni wajichukulie Mali zetu Waafrika. Swali la kujiuliza, kama kweli Dini hizi ni Uongo na zilikuja ili kututawala,iweje na wao huko Ulaya, Asia, Amerika na kwingineko waendelee kushiriiki mpaka leo hii katika Imani hizo hizo tulizonazo huku Afrika. Nikupe tu taarifa kuwa, kwa sasa hata huko Ulaya, Marekani na Asia kuna Waafrika na wengine ni Watanzania wanashiriki kueneza habari za Mungu. Wengine hudiriki kusema kuwa Ukristo ni wa Wazungu. Huku ni kutojua Historia ya Ukristo. Ukristio haukuanzia Ulaya. Ukristo ulianzia Mashariki ya Kati yaani Israel, huko ndiko Chimbuko la Ukristo baada ya YESU KRISTO kuwako Duniani katika hali ya Kimwili yapata miaka 2017 sasa iliyopita.Yawezekana kweli baadhi ya Wamisionari waliitumia Dini kama sehemu ya kujitwalia mali za Waafrika, lakini Injili ya Mungu inaweza kuenezwa either katika hali ya Ubaya au Wema.

UHUSIANO WA ALAMA ZA TAIFA NA UDHIHIRISHO WA UWEPO WA MUNGU.

Tazama Wimbo wetu wa Taifa, maudhui yake ni kuomba rehema kwa Mungu, tazama Dua ya kuliombea Bunge, maudhui yake ni kumtaja Mungu aweze kuibariki Nchi na Viongozi wake. Tazama viapo vya Viongozi kuanzia Rais hadi Viongozi wengine. Viapo vyote vile hufanyika kwa kumuomba Mungu huku muhusika akiwa ameshika kitabu Kitakatifu kulingana na Imani yake. Yote hiyo ni kudhihirisha kuwa hata Nchi yenyewe inatambua uwepo wa Mungu. Sasa kama ndugu yangu wewe umezaliwa na kuikuta hata Nchi yenyewe inatambua uwepo wa Mungu, iweje wewe unayejiita msomi mwenye umri sijui wa mika 40 au 50 ukatae kuwa Mungu hayupo.? Wakristo tunaamini kuwa YESU alikuwapo miaka 2017 sasa iliyopita. Tangu hapo watu wamekuwa wakiamini kuwa YESUalikuwapo,ila wewe ndugu mwenye miaka 40, 50 au 60 unapinga mambo haya uliyoyakuta na kuwepo zaidi ya Miaka 2000 iliyopita. Bila shaka watu kama ninyi mnaopinga hamuwezi kukosekana, maana hata Israel aliko zaliwa Yesu mpaka sasa kuna Watu bado hawaamini kama YESU alishakuja na kwamba ndiye aliyetabiriwa tangu enzi za mababu zetu wa Imani kuwa atakuja Mwokozi wa Ulimwengu.

Mifano ipo mingi ila kueleza kwa uchache, kwa leo naomba kuhitimishia hapo. Lengo kubwa la andiko hili ni kuweka msingi mzuri wa wewe kuelewa na kuamini kuwa Yote yasemwayo kuhusu Mungu ni kweli na dhahiri. Baada ya andiko hili la Msingi, itafuatia maandiko mengine ya namna bora na sahihi ya kuweza kufahamu kwa nini tupo Duniani na ni nini Mungu amekusudia kuhusu Maisha ya Mwanadamu.

Kama andiko hili litakuwa sehemu ya Mwanzo wako mpya wa Maisha hasa katika kumuamini Mungu, basi tuungane pamoja na nitaandaa Ujumbe mwingine kwa ajili yako ili kukuongoza katika ile kweli kadiri Roho wa Mungu atakavyonijalia. Mungu akubariki sana na karibu tuendelee kujifunza kuhusu Mahusiano yetu na Mungu aliye muumba wetu.
 
Unatuchosha bana. hakuna atakayesoma upuuzi huu...umeandikaaaaaaa unadhani unapata thawabu
 
Mkuu embu jaribu kufupisha ili imvutie msomaji na apate cha kujifunza... weka hata chapter 10 lakini ziwe fupifupi
 
Refu sana hii ngoja kwanza ninywe chai ya kutosha ndo nirudi
 
Naomba unitumie kwa e mail
.... Naomba sana mkuu niweze kuusoma kwa utaratibu
 
Binadamu wengi wametingwa na mahangaiko na shughuli za kila siku amazo zimefanya wasilisome neno LA Mungu. Imeandikwa na narejea "Watu wangu wanakufa kwa kokosa maarifa" wanakosa maarifa kwa sababu hawalisomi neno LA Mungu. Ni vigumu sana kwa kizazi hiki kusoma Uzi huu ambao ni mrefu kiasi hicho.Kwa sababu hats Biblia takatifu ni ngumu sana kwa kuisoma. Mungu akubariki we we ambaye bado unaupako wa kuhubiri neno uendelee kufanya hivyo. Usikatishwe tamaa na comments zinazotolewa kwani wote tumeitiwa kwa kazi ya kusifu, kutukuza na kuhubiri kazi njema ya injili ya Bwana.
 
Unatuchosha bana. hakuna atakayesoma upuuzi huu...umeandikaaaaaaa unadhani unapata thawabu



kwanini unatusemea ujumbe mfupi hivyoo ata nusu saa haipiti. unasema unachosha wewe unakila dalili ya kuwa ni mvivu.

ingekuwa ni story za free mason ungesoma zote na coment zote.

sikuhukumu lakini penda kuapreciate jambo mwenzako anafanya. ungekuwa nakauwezo kidogo cha kufikiri naungepima alichoandika ungejua Muda aliotumia kuandika hayaa aliyoyaandika inawezekana ni mara tano ya muda utakao soma.
 
kwanini unatusemea ujumbe mfupi hivyoo ata nusu saa haipiti. unasema unachosha wewe unakila dalili ya kuwa ni mvivu.

ingekuwa ni story za free mason ungesoma zote na coment zote.

sikuhukumu lakini penda kuapreciate jambo mwenzako anafanya. ungekuwa nakauwezo kidogo cha kufikiri naungepima alichoandika ungejua Muda aliotumia kuandika hayaa aliyoyaandika inawezekana ni mara tano ya muda utakao soma.
Fact. Be Blessed.!
 
Binadamu wengi wametingwa na mahangaiko na shughuli za kila siku amazo zimefanya wasilisome neno LA Mungu. Imeandikwa na narejea "Watu wangu wanakufa kwa kokosa maarifa" wanakosa maarifa kwa sababu hawalisomi neno LA Mungu. Ni vigumu sana kwa kizazi hiki kusoma Uzi huu ambao ni mrefu kiasi hicho.Kwa sababu hats Biblia takatifu ni ngumu sana kwa kuisoma. Mungu akubariki we we ambaye bado unaupako wa kuhubiri neno uendelee kufanya hivyo. Usikatishwe tamaa na comments zinazotolewa kwani wote tumeitiwa kwa kazi ya kusifu, kutukuza na kuhubiri kazi njema ya injili ya Bwana.
Amen, be Blessed too.!
 
Back
Top Bottom