Chapa na mihuri ya kichawi

Chapa na mihuri ya kichawi

Fandre

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2013
Posts
320
Reaction score
225
Askofu Dr. Josephat Gwajima
Ufufuo na Uzima-Headquarters
Dar es Salaam, Tanzania
03/05/2015

Maandiko:
Ufunuo Wa Yohana 13:17
Mwanzo 4:5
Wagalaatia 6:16
Ufunuo 9:4
Yoshua 2:15

Chapa ni alama anazowekewa mtu au kitu na kukitambulisha kuhusiana na jambo husika.

Dunia ina chapa nyingi kadhalika katika ulimwengu wa Kiroho yaani ule usiionekana kuna chapa za Mungu na chapa za Shetani yaani Chapa za Kichawi.

"Anything Satanic is witchcraft"

Upande wa pili:

Muhuri ni mchoro wa maandishi yanayoonyesha mwenye alama inayothibitisha uhalali wa jambo au mtu juu ya jambo fulani!

Sasa kwa maarifa haya ya Chapa na Mihuri ndivyo ilivyo hata kwa ulimwengu ule usioonekana(Rohoni) nao unaendeshwa na mambo haya muhimu.

Kuna mifano kadhaa ya watu waliowahi kuwekewa Chapa na mihuri katika Biblia ambao waliwekewa na Mungu:
1. Paulo
2. Kaini

Hivyo basi wachawi nao wanayo maarifa ya kuwawekea watu mihuri au chapa ambazo zitawafanya watu hao kuteseka kwa kulingana na mihuri waliowawekea.

Wapo waliowekewa mihuri ya:
1. Mihuri ya Kifo
2. Mihuri ya Magonjwa
3. Mihuri ya Umasikini
4. Mihuri ya Kukataliwa n.k.

Hivyo basi, mihuri ya kichawi huwafanya watu waliowekewa mihuri hii kufuatiliwa na kila matatizo na laana kulingana na muhuri aliowekewa mtu katika maisha yake.

Mihuri ina maana sana kwa sababu pasipo muhuri watu hawawezi kuamini uhalali Wa jambo hilo kwahiyo kwa kila tatizo linalompata mtu kuna muhuri ulikwishawekwa katika maisha ya mtu huyo katika ulimwengu wa roho ama na wachawi au waganga au warozi pasipo yeye kujua.

Familia/Kaya nyingi zimekua na matatizo ya kufuatana na yasiyoisha na zimekosa majibu na matatizo yamekua na kufuata kila mtu katika ukoo na wengi wamejaribu kujitoa katika maisha hayo lakini wameshindwa kujitoa na wamekosa majibu nini kilichopelekea kukutwa na shida au matatizo yao!

Kwahiyo ni jambo la kuaminika kabisa ya kuwa wapo watu wengi duniani na familia nyingi zimewekewa mihuri na chapa ambazo zinawafanya kuwa katika mazingira ya kuonewa na nguvu za Giza pamoja na wachawi kwani chapa hizo zinawapa wachawi Uhuru wa kuwatesa kulingana na chapa hizo!

Katika vitabu vya Ufunuo Wa mambo yajayo tunajifunza ya kuwa...."Watu watawekewa chapa ya mpinga Kristo ambayo itawafanya wawe na uwezo wa kununua au kutokununua"

Shetani anao uwezo wa kuweka chapa ambazo ni za mangamizi kwenye maisha ya watu.

Kwa lugha nyepesi CHAPA ni ile mipaka ambayo watu huwekewa katika maisha wasiweze kufikia malengo yao na mambo muhimu katika maisha.

Watu wengi waliowekewa chapa na mihuri ya umasikini wamefungwa akili zao ili wasijue nini cha kufanya ili kuendelea mbele.

Kuna watu hupata mishahara au pesa lakini mwisho wa siku hawajui pesa zimepotea namna gani kwani huisha pasipo kufanya jambo lolote la msingi!

Kadharika Taifa nalo linawez kuwekewa Chapa na mashetani kutokana na misingi ya viongozi Wa Taifa. Mfano: Tanzania inaweza kuwa imewekewa Chapa za Umasikini na kudolola kwa uchumi kutokana na misingi ya kichawi ya viongozi wa Taifa.

Watu wengi wana chapa wamewekewa wao ni kulogwa tu katika maisha yaani kila unapojitahidi kuwakimbia wachawi au matatizo bado yana wewe tu!

Kwahiyo ni jukumu la kila mwanadamu kuwa na maarifa ya kutosha juu ya namna ambavyo wachawi na shetani hutumia kuwaharibia watu maisha na kujua huku kitakusaidia kujua namna ya kumshinda shetani na wachawi.

**********Mwisho ***********

NB:
Kwa mafundisho zaidi ya Askofu Gwajima kwa mfumo wa DVD, MP3, Vitabu na maombezi kutoka katika vifungo vya kichawi na kishetani.
+ 255 673 848428
 
Waambie Gwajima waambieeeeeeeeeee!! Yaani kuna watu wamepigwa muhuri wa ujinga pia!!!badala ya kufanya kazi kwa bidii na kuweka mipango mikakati ya kuboresha uchumi na afya zao wao wanaishia kusombea pesa na muda wao mwingi kwa hawa matapeli wa imani wanaohubiri maji huku wanakunywa wine!!wanousifu umasikini wa muumini kuwa ni kigezo cha kumpeleka mbinguni huku yeye mwenyewe akiwa ni kati ya manabii wenye ukwasi wa kutisha!!waambie mazee!!waambie wachoropoe mimba tu,siku kizazi kikigoma waje kwako utawapatia uzazi kwa gharama nafuu tu!!waambie babaaaaaaaa ngwajimaaa
 
Amen kubwa kutoka kwa mtumishi wa Mungu,hakika tunajifunza mengi kutoka kwake.
 
Gwajima anaongeaga complex isues lakin ni fact aisee jamaa amesema kweli sana hongera gwakima tunakuelewa sasa
 
Duuh, kumbe huwa ana mafundisho mazuri hivi? nimemjua huyu mtumishi wa Mungu kupitia matusi yaleee! ila anautumia vema ulimi wake, kwenye matusi yumo na hekima imo. Stay Blessed Servant Of God , Gwajima.
 
Mbona hujawahi kutuwekea mahubiri ya Kadinal Pengo walau tupate mafundisho yake maana kila uja hapa ni Gwajima
 
Mimi naona mafundisho ya Pengo ungekua unatuletea wewe kwani kila mtu anaweka anachokipenda
 
Askofu Dr. Josephat Gwajima
Ufufuo na Uzima-Headquarters
Dar es Salaam, Tanzania
03/05/2015

Maandiko:
Ufunuo Wa Yohana 13:17
Mwanzo 4:5
Wagalaatia 6:16
Ufunuo 9:4
Yoshua 2:15

Chapa ni alama anazowekewa mtu au kitu na kukitambulisha kuhusiana na jambo husika.

Dunia ina chapa nyingi kadhalika katika ulimwengu wa Kiroho yaani ule usiionekana kuna chapa za Mungu na chapa za Shetani yaani Chapa za Kichawi.

"Anything Satanic is witchcraft"

Upande wa pili:

Muhuri ni mchoro wa maandishi yanayoonyesha mwenye alama inayothibitisha uhalali wa jambo au mtu juu ya jambo fulani!

Sasa kwa maarifa haya ya Chapa na Mihuri ndivyo ilivyo hata kwa ulimwengu ule usioonekana(Rohoni) nao unaendeshwa na mambo haya muhimu.

Kuna mifano kadhaa ya watu waliowahi kuwekewa Chapa na mihuri katika Biblia ambao waliwekewa na Mungu:
1. Paulo
2. Kaini

Hivyo basi wachawi nao wanayo maarifa ya kuwawekea watu mihuri au chapa ambazo zitawafanya watu hao kuteseka kwa kulingana na mihuri waliowawekea.

Wapo waliowekewa mihuri ya:
1. Mihuri ya Kifo
2. Mihuri ya Magonjwa
3. Mihuri ya Umasikini
4. Mihuri ya Kukataliwa n.k.

Hivyo basi, mihuri ya kichawi huwafanya watu waliowekewa mihuri hii kufuatiliwa na kila matatizo na laana kulingana na muhuri aliowekewa mtu katika maisha yake.

Mihuri ina maana sana kwa sababu pasipo muhuri watu hawawezi kuamini uhalali Wa jambo hilo kwahiyo kwa kila tatizo linalompata mtu kuna muhuri ulikwishawekwa katika maisha ya mtu huyo katika ulimwengu wa roho ama na wachawi au waganga au warozi pasipo yeye kujua.

Familia/Kaya nyingi zimekua na matatizo ya kufuatana na yasiyoisha na zimekosa majibu na matatizo yamekua na kufuata kila mtu katika ukoo na wengi wamejaribu kujitoa katika maisha hayo lakini wameshindwa kujitoa na wamekosa majibu nini kilichopelekea kukutwa na shida au matatizo yao!

Kwahiyo ni jambo la kuaminika kabisa ya kuwa wapo watu wengi duniani na familia nyingi zimewekewa mihuri na chapa ambazo zinawafanya kuwa katika mazingira ya kuonewa na nguvu za Giza pamoja na wachawi kwani chapa hizo zinawapa wachawi Uhuru wa kuwatesa kulingana na chapa hizo!

Katika vitabu vya Ufunuo Wa mambo yajayo tunajifunza ya kuwa...."Watu watawekewa chapa ya mpinga Kristo ambayo itawafanya wawe na uwezo wa kununua au kutokununua"

Shetani anao uwezo wa kuweka chapa ambazo ni za mangamizi kwenye maisha ya watu.

Kwa lugha nyepesi CHAPA ni ile mipaka ambayo watu huwekewa katika maisha wasiweze kufikia malengo yao na mambo muhimu katika maisha.

Watu wengi waliowekewa chapa na mihuri ya umasikini wamefungwa akili zao ili wasijue nini cha kufanya ili kuendelea mbele.

Kuna watu hupata mishahara au pesa lakini mwisho wa siku hawajui pesa zimepotea namna gani kwani huisha pasipo kufanya jambo lolote la msingi!

Kadharika Taifa nalo linawez kuwekewa Chapa na mashetani kutokana na misingi ya viongozi Wa Taifa. Mfano: Tanzania inaweza kuwa imewekewa Chapa za Umasikini na kudolola kwa uchumi kutokana na misingi ya kichawi ya viongozi wa Taifa.

Watu wengi wana chapa wamewekewa wao ni kulogwa tu katika maisha yaani kila unapojitahidi kuwakimbia wachawi au matatizo bado yana wewe tu!

Kwahiyo ni jukumu la kila mwanadamu kuwa na maarifa ya kutosha juu ya namna ambavyo wachawi na shetani hutumia kuwaharibia watu maisha na kujua huku kitakusaidia kujua namna ya kumshinda shetani na wachawi.

**********Mwisho ***********

NB:
Kwa mafundisho zaidi ya Askofu Gwajima kwa mfumo wa DVD, MP3, Vitabu na maombezi kutoka katika vifungo vya kichawi na kishetani.
+ 255 673 848428

Hii chapa ya kuwezesha kununua itakuwa ya Mungu au shetani? Italenga kumnufaisha nani? Na kumkandamiza nani?
 
umetolea mfano wa Paulo na Abeli ktk kupigwa chapa..
kwaiyo hao walipigwa chapa ya MUNGU au shetani ?
 
gwajima gan aliyezaa na flora mbasha ndo anaongea haya?
cjui amekula maharage ya wap
 
Mbez mwisho stend hakuna gar wasafir kibao tunatoa macho tu na kuchungulia barabara kama linakuja kumbe haliji duuuh
 
Back
Top Bottom