Chanzo kingine cha mapato ya serikali

mtzmweusi

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
8,658
8,994
Wakuu habari zenu baada ya hawa wanaoitwa wahisani kusepa na misaada yao nimekaa nikafikiri chanzo kingine ambacho serikali inaweza kukitumia kupata pesa za maendeleo na ningependa hizi ziingie moja kwa moja ktk mfuko wa maendeleo, chanzo chenyewe ni ktk simu tunazotumia mf kila mmiliki wa simu akichangia tsh 1000/= kwa mwezi kwa kadirio la kawaida kuna watumiaji wa simu takribani mil 5 hapo tutapata bil 5 kwa mwezi hivyo kupelekea kupata trilioni 6 kwa mwaka tukifunga mkanda tunaweza tuanze kufikiri nje ya box Tanzania bila misaada inawezekana
Mtzmweusi
 
Hv mbona mnakimbilia triliom,yaani kila anayeleta hesabu anataka afike tu trilion hata kama haijafika.

Haya mapendekezo ya namna ya kupata fedha sasa ni kero,haya amueni kila mtz alipe 5000 kila mwaka!
 
Usikute huyu mleta mada ni mkuu wa idara fulani serikalini.hii ni kutokana na serikali yetu kupeana vyeo bila sifa stahiki.sasa bilion 5 kwa mwezi inafikaje trilion 6 kwa mwaka?
 
mtzmweusi, bilioni moja ni 1,000,000,000 na trilioni moja ni 1,000,000,000,000. Kama unakusanya bilioni tano kwa mwezi, itakuchukua miezi 1000 kukusanya trilioni sita. Miezi 1000 ni sawa na miaka miaka zaidi ya 80! Je wewe utakuwepo wakati huo uweze kuzifaidi hizo kodi?
 
Hakuna cha kufikiri nje ya box hapo! Hilo suala ilibaki kidogo tu liwe implemented awamu iliyopita lakini wananchi tukapinga... hayo mambo ya kodi ya kichwa yalishapitwa na wakati!
 
Unatuaibisha kwa kujiita mtz mweusi huku hujui kuzidisha,bora ungekuwa mtz mhindi. Kufikiri nje ya box ndoivyo? Mbona umefikiri nje ya ubongo...mizigo tuliyonayo nimingi hatutaki serikali izidi kutukatakata kama nikodi tunalipa kibao. Pole lakini jifunze magazijuto.
 
Bilion sita mara miezi 12 unapata trilioni ngapi??? Elimu elimu elimu. Sema m nimeishia la pili B ngoja wenye phd waje.
Masikini Watanzania tulio wengi tuna nia nzuri lakini maarifa ndio madogo au hakuna kabisa. Wataalamu wanadai kuwa huwezi kufanya endeleo lolote bila elimu ya hesabu ambayo ndio sayansi yenyewe.
Mleta mada ana hoja nzuri lakini hajui billioni 6 x 12 ni ngapi, kweli huyu anaweza kuyajua matatizo ya nchi hii!? Je, huyu anaweza kuelewa uchumi wa viwanda unajengwaje!?
Mlivyoambiwa serikali imeua elimu mkabisha basi pitieni huku tuililie nchi yetu pamoja.
 
wengi mnaotoa mawazo ya kodi ni yale ya kodi za kuwanyonya wanyonge.
Kuna sekta ambazo zikisimamia vizuri hatutalia njaa
Ni kweli bro.ukisemacho.
Humu ndani yaonekana watu hawajui wakisemacho, na hupendekeza vitu ambayo huenda hawajavifanyia utafiti na huenda kuumiza tu wana nchi, kitu ambacho ht mkuu wa nchi unataka kuondokana nacho vile vile, lkn siwezi kuwalaumu sana, ni aina ya elimu na malezi ya kitanzania yaliyokaa kikandamizaji zaidi.

Miaka hii si ya kufungishana mikanda kinguvunguvu ghafla namna hii!! Kilichopaswa kufanya ni Ku mobilize resources zetu vyema, na kucheza na diplomasia vzr na hao waitwao wafadhili.
Msicheze na hao watu, wana kampuni mbaya mno, mi america anaweza kwenda kwa wanunuzi wa mazao yenu nje wote, kiisha yy akawanunua wale ili wasinunue chochote kitokacho tz, na ana uwezo wa kuwashauri na kuagiza watalii soote weupe wasitembelee mbuga zenu, dollar mtazipata wapi, kwa kodi za ndani??! Nyooh!!

Mkiishakukosa dollar, hizo Boeing mnazotaka kununua 5 ndani ya miaka mitano, DSM kuwa km Hong Kong, ferries kila ziwa, na DSM - bagamoyo, lami kila mkoa na wilaya, madaraja km Yale ya Manhattan, nchi ya JPM ya viwanda, mtaweza wapi bila kuwa boosted?? M nadhani mtaweza wkt hamjajiandaa kuondokana na kuwa taiga LA wachuuzi wa bidhaa za Kenya, na wachina?? Pole sana.
 
Wakuu habari zenu baada ya hawa wanaoitwa wahisani kusepa na misaada yao nimekaa nikafikiri chanzo kingine ambacho serikali inaweza kukitumia kupata pesa za maendeleo na ningependa hizi ziingie moja kwa moja ktk mfuko wa maendeleo, chanzo chenyewe ni ktk simu tunazotumia mf kila mmiliki wa simu akichangia tsh 1000/= kwa mwezi kwa kadirio la kawaida kuna watumiaji wa simu takribani mil 5 hapo tutapata bil 5 kwa mwezi hivyo kupelekea kupata trilioni 6 kwa mwaka tukifunga mkanda tunaweza tuanze kufikiri nje ya box Tanzania bila misaada inawezekana
Mtzmweusi
Wewe ni ma.ta.ko ya nokho! Hivi mnafikri trillion 1 nichezo? Hiyo imekula kwetu kwa ujinga wa ccm!
 
wengi mnaotoa mawazo ya kodi ni yale ya kodi za kuwanyonya wanyonge.
Kuna sekta ambazo zikisimamia vizuri hatutalia njaa

Makampuni ya simu haya Vodacom,Tigo, Airtel , Zantel na sasa Halotel hawa hawalipi kodi wanayotakiwa kulipa kwani wanatuibia sana sisi wateja na kutengeneza faida sana lakini hawalipi kodi stahiki!!! Enzi ya Kikwete wakina Rostam na Ngeleja walikuwa wanatumia influence yao na vodacom wakawa wanapeta tu!!!
 
Tanzania tuna vyanzo vingi sana vya kodi yani mapato mfano
  1. Madini; yapo ya kila aina mf dhahabu,almasi,green tomerine,ruby nk
  2. Usafirishaji; tunaweza kupata kodi kwenye magari,pikipiki na vyombo vingine vya usafirishaji
  3. Mawasiliano;Hapa kuna kodi nyingi sana pia kwasababu watanzania wengi hivi sasa wanatumia simu kwahiyo tunaweza kupata mapato kupitia kampuni za simu mf;tigo,vodacom,halotel,zantel,smart,airtel etc
  4. Utalii;tuna bunga nyingi sana za wanyama na vivutio vya kutosha ambavyo vinaweza kutuingizia pesa nyingi sana
  5. Bahari na Maziwa yetu tunaweza kupata pesa kupitia shughuliza uvuvi kuna pesa nyingi sana huko zinapotea kusiko julikana mpaka meli kutoka china zinaingia kwenye bahari yetu ya hindi kufanya shughuli za uvuvi huku wenye mali tumelala
  6. Misitu yetu inayopatika na Tanzania
  7. Bandarini na Mipaka ya inchi yetu kuna kodi nyingi sana zinaweza kupatikana huko kama tukiwa makini
 
Wakuu habari zenu baada ya hawa wanaoitwa wahisani kusepa na misaada yao nimekaa nikafikiri chanzo kingine ambacho serikali inaweza kukitumia kupata pesa za maendeleo na ningependa hizi ziingie moja kwa moja ktk mfuko wa maendeleo, chanzo chenyewe ni ktk simu tunazotumia mf kila mmiliki wa simu akichangia tsh 1000/= kwa mwezi kwa kadirio la kawaida kuna watumiaji wa simu takribani mil 5 hapo tutapata bil 5 kwa mwezi hivyo kupelekea kupata trilioni 6 kwa mwaka tukifunga mkanda tunaweza tuanze kufikiri nje ya box Tanzania bila misaada inawezekana
Mtzmweusi
Angalieni na nje ya box basi. Misaada ya fedha tu. Serikali haiwezi kuwa haitendi haki halafu dunia ikae kimya. Kuna watu wanafikiria ukishapata fedha za kutosheleza bajiti ya nchi basi utaweza kufanya unavyotaka. Vikwazo viko vingi kwani utegemezi wetu na mkubwa. Kuna matibabu, teknolojia usafiri nk
 
Back
Top Bottom